Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Mkoa Ruvuma katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kipindi cha Mwezi Septemba 01.2023 hadi Oktoba 25,2023 limeendesha Opereseheni, misako na doria mbalimbali maeneo yote ya Mkoa wa Ruvuma na kukamata watuhumiwa watatu (03) wakiwa nyara za Serikali, Meno ya tembo vipande 10, Nyama ya Nyati vipande 17 na Mnyama Kuro vipande 20.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilya amesema wamekamata watuhumiwa kumi (10) wakiwa na bhangi kavu iliyokuwa imehifadhi kwenye salfeti na kete 176, watuhumiwa watatu (03) wakiwa na Pombe moshi (Gongo) lita 180, Mtuhimiwa mmoja (1) akiwa na Pikipiki 01 aina ya Houjue yenye namba za Usajili MC.815 CDK aliyoiiba katika kijiji cha mikalanga – Mbinga.