RT yasimama na Simbu: Nyuma ya Pazia kuenguliwa Uchaguzi TOC

RT yasimama na Simbu: Nyuma ya Pazia kuenguliwa Uchaguzi TOC

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limeeleza kusikitishwa na hatua ya kumuengua mwanariadha Alphonce Simbu katika uchaguzi wa Kamisheni ya Wachezaji ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kwa madai ya usaliti.

Rais wa RT, Silas Isangi, akizungumza na TBC Digital jijini Mwanza, amesema sakata hilo lilipaswa kujadiliwa na viongozi wa TOC pamoja na RT badala ya kuchukua hatua za kumuadhibu mchezaji moja kwa moja.

Isangi pia amefafanua kuwa Simbu hakuwa na mamlaka ya kuamua mavazi yanayopaswa kutumiwa na wachezaji wa Tanzania kwenye mashindano ya Olimpiki, hivyo suala hilo lilihitaji maelewano zaidi kati ya pande husika.

Simbu alikuwa anagombea nafasi ya Uenyekiti Kamisheni ya Wachezaji (KAWATA) ya TOC katika uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Msimamizi wa uchaguzi huo, Henry Tandau, ambaye ni Makamu wa Rais TOC, alimwengua Simbu ukumbini mbele ya wapigakura, huku akimtuhumu kwamba ni muasi aliyechochea wachezaji kutokuvaa vifaa vya Kampuni ya Asics vilivyokuwa vimeandaliwa na kamati hiyo, wakati wa michezo ya Olimpiki Paris iliyofanyika Julai 26-Agosti 11, mwaka huu, badala yake wakatumia vya Xtep, ambao ni wadhamini wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Licha ya mchakato wa usaili kufanyika, Simbu hakupewa taarifa kwamba ameenguliwa, hivyo kufika hadi mbele ya wajumbe akiamini anaenda kuomba kura, lakini Tandau hakutaja jina lake.

Akizungumzia tukio hilo, Simbu alieleza kusikitishwa na kitendo hicho alichokiita si cha kiuanamichezo na kisichofuata taratibu, kwani mbali ya kumyima haki yake ya msingi, kimemdhalilisha mbele ya wapigakura na jamii kwa ujumla.

Pia, Soma:

Simbu akatwa jina na Henry Tandau na Ghulam kwenye uchaguzi wa kamisheni
Kufutwa kwa Mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania ( TOC)
 
Wameona baadae atataka kugombea kiti cha urais cha milele cha Filbert Bayi......kiufupi makamu wa Raisi wa TOC amefuata maagizo ya boss wake.
 
Huo uongozi wote unatakiwa kufutwa
 
Wala rushwa na matapeli hao watu wa rt na toc..ila hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Back
Top Bottom