RTO Arusha hii T500 AVE ni matokeo ya rushwa ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,906
Tanzania kila mara utasikia ajali zimetokea watu wamekufa , ama dereva kaacha njia kisa speed ama mtu kasababisha na wengi wao wakiwa hawana sifa za kuendesha magari .Leo hii nimeshangazwa sana sana kuona mtoto wa miaka 14 aliyeko form 2 anaendesha gari na akiwa na leseni sijui kapata wapi .Mtoto Abdallah Malima , ambaye Baba yake ni Boss wa Pride Tanzania analitumia gari hilo mjini Arusha kwenda shule na kurudi na hata kukata mbuga hadi mikoa ya jirani .Tatizo langu mie Lunyungu si mtoto wa shule kuendesha gari ila Umri wa mtoto huyu na kupewa leseni ya kuendesha gari .Wajuvi naomba kujua kama sheria ya Tanzania sasa ilisha badilishwa hadi mtoto wa miaka 14 kupewa leseni .

Nawasilisha .
 
Mh,sidhani kama sheria imebadilishwa. Hayo ni matokeo ya RUSHWA!! Traffic police wanatoa leseni bila hata kumjua mwenye leseni, cha maana uwe na mshiko!!!!...Ndio Tanzania hiyo
 
Nimeona gari hadi kadi ya gari na mtoto mwenyewe yuko form 2 na umri wake nikawa sina la kusema nikasema wacha nije JF niulize na labda wahusika watajali kwenda kuipitia leseni yake .Miaka 14 kweli anapewa leseni na ikitokea ajali sijui polisi watasemaje .Kisa Baba yake anazo na anafahamika
 
that is very serious...hata hapa dar kuna wakati wageni walikuwa wananunua pasport hata kabla hawajajua kuendesha magari..ilikuwa ni fashion kwa wachina wa kampuni moja hapa dar kununua leseni kama soda..yupo mmoja alimnunulia mkewe kabla hata hajafika bongo...shame to our system and shame to us...na kitu kama hiki kinafanyika pia kwenye work permits...

we can not blame the system as it is clear on the procedures and regulations....but people in the system are so corrupt...
 
Kila kona kumeoza, yote sababu ya wale tuliowapa madaraka tokea uhuru wametufanya mabwege. Kama aliyekuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri aliweza endesha gari ambayo haina bima unategemea nini?
 
Traffic police wanatoa leseni bila hata kumjua mwenye leseni, cha maana uwe na mshiko!!!!...Ndio Tanzania hiyo

Very true, kuna jamaa yangu anayo leseni aliipata kimazabemazabe bila hata ya kupita driving school, mwanangu akiwa kwenye usukani lazima ushike roho yaani ni mzito wa vitu vidogo tu hata reverse yeye ni msala. Rushwa trafiki imefikia pabaya mno.
 
Kila kona kumeoza, yote sababu ya wale tuliowapa madaraka tokea uhuru wametufanya mabwege. Kama aliyekuwa Mwanasheria Mkuu na Waziri aliweza endesha gari ambayo haina bima unategemea nini?

Mzee wa tujisenti-Chenge au mwingine?
 
Tatizo la Lunyungu habari zake huwa zinatia mashaka. Hope this time u got it right ngosha...
 
Shauri yako, siku moja nilisema hii ni nchi ovyo... watu wananijia juu...

Si bora ungesema ya hovyo, you just called it a bullshit country simply because Fisadi papa Rostamu Azizi aliguswa!
 
Duh, Kama Baba anarudishwa nyumbani na wahudumu wa baa hajiwezi, watoto unategemea watakuaje?
 
Very true, kuna jamaa yangu anayo leseni aliipata kimazabemazabe bila hata ya kupita driving school .Rushwa trafiki imefikia pabaya mno.

Killuminati unayosema ni kweli kabisa,napofanya kazi aliwahi kuja traffic mmoja nikamsaidia matatizo yake,baada ya hapo nilipokuja kugundua kuwa ni traffic nikamwambia nahitaji Leseni unajua aliniambiaje,nipe 40000 tshs baada ya wiki leseni yako itakuwa tayari,na wala hakuniuliza kama nimepitia driving school au bado,nilitafakari later nikawaeleza wazazi wangu wakanishauri nisimpe hiyo pesa na kama nataka Leseni its better nikaipata kwa njia halali,Traffic wa bongo njaa kali inawasumbua.
 
Unaona sasa watu wameacha kujadili hili swala la muhimu na la kwanza kama kufichua ufisadi nyie mnang'ang'ani juu badala ya kuanzia chini. Huyu mtoto tayari anatoa rushwa na anaishi katika mazingira ya rushwa huyu huyu tutegemee baadae atakuwa kigogo.
Alafu kingine na cha kushangaza watu wanaona kama ni haki yake alafu mtoto huyu huyu siku atelezee na gari lake hilo na kuleta maafa watu mnaanza kuunda tume....Tanzania nchi yangu ovyo sana.
 
Kwa data nilizonazo - ni asilimia 4 (4%) ya watu wote wanaondesha magari hapa TANZANIA walipata mafuzo RASMI ya kuendesha magari. Hii aitokana na ma ofisa wa usalama wa barabarani (traffic police) kuwa na njaa kali, bali ni mfumo mzima kuazia juu hadi chini na chini hadi juu

- Askari anapofunzwa pale CCP Moshi, ikifikia wakati wa kuwa assigned kazi ndani ya wizara ya usalama wa raia, wanaopelekwa usalama wa barabarani ni lazima watoe hongo kupata nafasi hiyo (trust me!) - Hiyo ni juu chini - Kwa maana kuwa huyu askari akishapangiwa kuwa usalama barabarani anaamini kwa dhati kuwa maisha yake yote lazima apokee rushwa!

- Mzazi akishakwiba pesa za walipa-kodi ananunua "magari 10 ya kutembelea" na wakati huohuo watoto wake wana miaka chini ya kumi, kwa mantiki hiyo the next birthday gift ya mtoto ni gari, kwa nini asiendeshe gari akiwa na miaka 10? Kwa mzazi inaonekana kama ni sifa na hata majirani wamsifu kwa kuwa na "mtoto" anayeweza kuendesha gari - hiyo ni chini-juu

- NI MATOKEO YA JAMII CORRUPT -
 
Tanzania hasa Dar sinauhakika kama kuna watu wanatest siku hizi ili kupata driving licence especially class E. Mtu akishajifunza na kujua kusogeza gari then anatoa 60,000 baada ya siku mbili wale walimu wa vyuo vya udereva wanamletea licence.

Nchi imeoza kila sehemu na ndio maana vurugu barabarani haziishi kwani hakuna usimamizi kila sehemu, na wakubwa wao wanajua hilo kwani kuna incidence ambazo zinaonyesha kuwa nao wanajua.

Unakamatwa na RTO perhaps kwa wrong parking, anakukabidhi kwa junior mnegitiate kiasi cha kumpam yeye anaendelea na shuguli zake. Hata kama hakukwambia moja kwa moja yeye mwenyewe lakini kwa kukukabidhi kwa mtu mwingine anayekuomba rushwa inaonyesha huyo anatumwa mmalizane nae kwani kama hajui angemuuliza mtu niliyemkamata yuko wapi.

In real sense rushwa Tanzania hipo kila sehemu na haiwezi kuisha kwani mishahara inayolipwa haiendani na gharama za maisha, hivyo mtu anatafuta extra income kwa ajiri ya familia yake.

Ili inabidi tuangalie source yake tusiangalie rushwa tu tuangalie pia kwanini watu wanakula rushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…