Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi na Mkurugenzi wa Ruangwa Pride Hotel, Mparuka Hashim Mtopela amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Ruangwa.
Mparuka amekabidhiwa fomu na Katibu wa CCM wilaya ya Ruangwa, Abas Mkweta.
Hatua hii imekuja baada ya Mbunge wa Ruangwa anayemaliza muda wake na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kuripotiwa kuwa amepumzika Ubunge.
Kinachoendelea kwa sasa ni mchakato wa uteuzi wa vyama siyo wa tume. Suala la kupita bila kupingwa japo halipo kwasasa ungeliongelea wakati wa mchakato wa uchaguzi(mchakato wa Tume)