TANZIA Rubani wa Ndege iliyotekwa 1982 kushinikiza Nyerere ajiuzulu afariki dunia

Ni familia iliyokua inajiweza baba yao alikua na uwezo ndio mana watoto wake walipata elimu bora,pia kulikua na mdogo wao captain wa meli ya mv victoria
 
Kwahiyo wale abiria mateka waliruhusiwa kuingia mitaani London baada ya kuwasili Stanstead Airport hadi waonane na bii kizee na mbwa wake? Kuna ukweli wowote hapa?

Mkuu, nilinuia kujibu swali la if any of them suffered from life long trauma na nikatoa uzoefu mchungu wa kubadilisha mazingira overnight kutoka joto la tropiki mpaka baridi kali ya Ulaya.

Ni wazi kuwa episode nzima ya utekwaji wa ile ndege una maswali mengine ambayo mpaka leo hayana majibu yanayoridhisha.
 
Paschal kumbe unawajua vizuri ni kweli walikuwa wanapenda gari aina ya Volvo hasa George Mazula
 
Alikuwepo George Mazula. Kama sikukosea George ni mkubwa kwa Deo. George alimaliza form four (1967, Mara SS) na kujiunga na mafunzo ya kuendesha ndege, kule Uganda, Soroti Flying School.
Hapana Deo ni mkubwa na ndiye first born wa mzee Arobogast Mazula Edward Kalendero.
 
Bado nauliza mkongwe,kuna huyu Captain wa Atc matata sana mtu wa kinywaji sana mfupi hivi, mwaka ule baba wa taifa katutoka ye alisema ndio kamtoa London.
Na alipofika pale bar salamu yake ilikua Nendeni mkachukue mzoga wenu nimeshaleta.
Simkumbuki jina huyo nafkiri ni huyo George.
 
Kaburi hilo lina Miili miwili ya wapenzi,ambao waliuawa kwa kuchomwa moto huko Marekani... Kati yao Kijana wa Kiume ni Mtoto wa Marhum Capt. Geoge Mazulla aka KOROBOY
Kaburi la Baba yake lipo pembeni ya hayo mawili ya mtoto wa kiume na mchumba wake.
 
Enzi hizo Waswahili wenye Benzi wanahesabika!. Mimi nawakumbuka Benzi ya Mzee Lupembe, Benzi ya Obed Katikaza, Benzi ya Dr. Mtawali. Benzi ya Dr. fulani Changombe. Tajiri mmoja akiitwa Mgaya yeye ndio alikuwa ana Range!.
P
Lorrd Rajpar alikuwa nalo benzi fulani jeupe, namkumbuka akipenda kukatiza nalo kule ocean road baharini ule mtaa unaopita nyuma ya Ikulu kutokea Aga Khan, mzee unaongelea kabla ya 1984 Dar ile ya kwenda disco pale sea view na usiku sana watu wanarudi wanatembea hakuna bajaji wala bodaboda.
 
Miaka yake ya mwisho akiwa hai alikuwa akishinda pale maeneo ya Pegeout karibu na ilipokuwa bushtrekker. Alikuwa mtu poa sana, akiniona lazima anisalimie.

Walikuwa members wa Gymkhana Club miaka ile, ndio wajanja wa mjini enzi za Nyerere anaondoka anaingia Mwinyi,

Alikuwepo mtu mmoja akifanya kazi habari Maelezo akiitwa Abdallah Ngororo, kila nikifuata bia za wazee Chinese au IFM usiku ninamkuta anapata kinywaji akiwa na hayati Jaji Mapigano, Profesa Shaba na wazee wengine wa mitaa ile.
 
Kaburi hilo lina Miili miwili ya wapenzi,ambao waliuawa kwa kuchomwa moto huko Marekani... Kati yao Kijana wa Kiume ni Mtoto wa Marhum Capt. Geoge Mazulla aka KOROBOY
Usinikumbushe mwanangu Walter mazula....dah

Ova
 
Gymkhana wazee ngoma ngumu pale

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…