"Rudi huko huko" au "Kalale huko unakotoka"... wanatarajia nini?

tafazali Kipipi,nyumba nijenge mimi kulala nilale kwa jirani? Arrrrrrrrooooo tena usirudie kusema maneno hayo!

Nyumba ni yako umeacha wafanyakazi wako humo ndani? Au umekodi mtu wa kukulindia chumba? Nani anapenda kujiwa usiku wa manane kila siku, mfanyakazi wa kufua suruali, kutandika kitanda na kufungua mlango?? Unamlipa sh. ngapi? Kama we jeuri badilisha kitasa uwe na funguo yako......upoo!!
 
Pole sana kama yalikukuta mzee, we nakuamini najua ulibanwa na
kazi ukachelewa kurudi. Bora tu usinzie hapohapo mlangoni kuliko
kwenda hukohuko.
 
akiniambia nilale hukohuko... ntafurahi
 
Inakuwaje unachelewa kila siku? Imagine mwanamke anaweza fanya kama wewe ukakubali? Wanawake siyo wajinga afikie kukwambia lala huko. Ni tabia ambayo umekuwa ukifanya kwa muda mrefu.
 

kwani hata kuna haja ya ugomvi basi?!we unakataa kufungua mi nageuza kimya kimya kurudi 'nilikokuwa'!siku nyingine nikichelewa kurudi nakupigia simu nikiwa 'huko huko' ili kama 'unajisikia' kufungua siku hiyo ndo nianze safari ya kurudi home.hii haijalishi kama nyumba ni 'yako','yangu' au 'yetu'!
 

Hebu nisaidiwe katika hili.. ni njia ipi sahihi zaidi: ni pale ambapo mke/mume anahakikisha mwenza wake ana funguo ili anaporudi kutoka katika starehe zake /mihangaiko yake (hapa nataka ku exclude ishu muhimu kama vile kazini) ajifungulie mlango mwenyewe au ni vyema akae macho wazi kuhakikisha mwenzie anaporudi anamfungulia mlango?
 

Mkuu wewe hujawahi kutana na vichwa vilivyopinda, kama kweli unapenda mahusiano yako au unathamini familia/ndoa yako, hakuna haja ya mashindano kuna wakati inabidi lazima mmoja ajijishushe.. wakati mwingine hata yule asiye na kosa. Otherwise mtaishia kwenye mashindano ambayo impact yake inaweza kuwa mbaya zaidi. Mfano: unageuza kimya kimya, siku ingine haurudi kabisa.. Walahi utakuta wife keshamegwa au akachukua maamuzi mengine zaidi kukukomoa au kulipiza ..lol
 
Pole sana kama yalikukuta mzee, we nakuamini najua ulibanwa na
kazi ukachelewa kurudi. Bora tu usinzie hapohapo mlangoni kuliko
kwenda hukohuko.

Hah a hahaaa.. umenichekesha sana kwa kweli.
 

Safi sana kijana manake hapo utakuwa umenidhihirishia kuwa ulisogeza mtu wa kukufanyia kazi na haukuoa mke!! Kwa sababu kama ungekuwa umeoa basi ungeithamini ndoa na kuuona umuhimu kupunguza/kuondoa tatizo kuliko kuliongeza mara 10 tena kwa makusudi!! Na hayo unayoyasema ndugu, utayafanya kama huna shida ya ndoa!
 
Hizo zinatokea na hasa kwa watoto wakiambiwa rudi wanafurahi hadi asubuhi, wanaenda kumalizia raha zao. Nimeshudia mara nyingi tu wazazi wa namna hiyo au kwa watoto au wenyewe kwa wenyewe. Watoto wanachelewa makusudi wakijua wataambiwa warudi, na kweli wanarudishwa. Asubuhi wanajitetea na kuomba msamaha kuwa walikosa na walilala kwa "aunt".
 
Na hivi sasa hivi kuna simu,nikichelewa nampigia simu,akinifokea na kuniambia lala hukohuko ndo kwanza hata siharibu hata nauli
 

shida ninakuwa nayo na nakuwa nakupenda kiukweli kabsa kipipi,ila mara nyingine nyie visirani vyenu tukiviendekeza maisha yatasimama kabisa aisee!sasa kama huyo jamaa alieamua kuruka ukuta baadae akavunjika na kupelekea kifo ni upuuzi wa mke tu!fungua mlango tuzungumze mama,wewe kunifungulia mlango sio kwamba ndo mfanyakazi wangu bana,ndo hata maji ya kuoga hamweki siku hizi eti 'kuna shower'!,sasa kwenye shower mdalasini unawekaje!?hebu kuweni wanawake bwana na mtumie nguvu kubwa ya 'uanamke'(bado kidogo nikosee hapa,wallah.ningekula ban refu!)wenu kulinda na kutulea sisi wanafamilia jamani!!
 
hahahaaaah! katika wanaume huyo ndio mwenyewe!!!
 

hahahaaa! We ungeropoka tu naivi Paw yuko around.......lol! Unajua vitu vingine vinauma alafu vinaudhi vile vile!! Ni wazi kwamba ndoa inahitaji heshima iwepo na mara nyingi a man ndo anaenjoy heshima zaidi. Lakini pamoja na hayo bado unapaswa kunisikiliza na mimi sio eti kwa sababu we ni kichwa cha familia basi ndo unajiamulia na kujipendelea wewe tu bila kuwa na kiasi!! Ofcoz sikukatazi na ni vizuri pia ufanye yanokufurahisha, lakini every day kwenye mipombe, every day kunirudia saa nane za usiku, why?? Alafu unalalamika, nimhandle nani wakati mume anaondoka asubuhi kurudi usiku mnene, sasa hayo sio maisha ya mtu na housegal wake? Mwanaume hujirekebishi mpaka sasa nachoka natamani ni bora ulale huko huko, lakini we unaona ni kisirani na unaona utaniendekeza, do u think unachokifanya ni kizuri hata nikushangilie? Hell NO!!!!! Na hapo ndipo mtu anafikia hatua ya kufunga mlango ili kuwe na other alternative manake mazungumzo yamefail, if u decide kurudi ulipokuwa fine na hiyo utakuwa hunikomoi bali unanipa chance ya kuamua. Huyo aloruka ukuta hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda? Hata ndugu? Hilo sio kosa la mke bali ye mwenyewe aliona aibu ndo akaamua kuruka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…