ksny
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 1,704
- 1,694
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekiri kupoke rufaa za wagombea nafasi ya ubunge na udiwani zipatazo 557. Tume iliahidi kuanza kuzifanyia kazi kuanzia tarehe moja mwezi wa tisa na kutoa majibu japo hatujasikia jibu kwa mkata rufaa hata mmoja.
Kwakuwa kampeni zimeanza kushika kasi tungependa kupata majibu ili wagombea waweze kujipanga Kama wameshinda rufaa zao. Ikiwezwkana tume itoe matokeo ya Kila rufaa iliyotolewa uamuzi bila kusubiri zoote 557 zikamilike.
Kuchelewesha rufaa kutahesabika Kama mbinu za kupima hali ya ushindani ili kujua rufaa ipi ikubaliwe na ipii ikataliwe. Hapa NEC itakuwa sehemu ya siasa. Chondechonde vyama visijisahau virudi kutazama namna ya kushinikiza mapitio ya hizo rufaa.
Sidhani Kama rufaa zote zinahitaji muda mrefu kujadiliwa ukizingatia sababu zilizotolewa na wasimamizi kuwaengua wagombea.
NEC isije kujifungia ofisini ikipanga Nani awe mbunge na nani asiwe. Nafasi 557 nyingi sana . Ukiengua hata nusu tu itakuwa umehujumu uchaguzi kwa kiwango kikubwa.
Sisi wananchi tungependa majina yarudi na kuturudishia haki yetu ya kuchagua badala ya NEC kutuchagulia kwa kivuli Cha ameandika herufi kubwa badala ya ndogo , hakuweka picha nk
Nadhani ni wakati muafaka matokeo hayo kuambatana na majina. Tutajuaje ni kweli au figisu tu!