Rufaa ya mchezaji Langa Lesse Bercy wa Congo Brazzaville

the muter

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2012
Posts
1,347
Reaction score
1,828
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, mwaka huu lilimkatia rufaa mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse Bercy, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).

TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia gharama za vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.

Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.

Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko "vitani",eneo hilo halikutajwa.

TFF inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .

Kadhalika Aidha TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.
 
Kumbe watanzania tumeamka kama tunafatilia kujua Aki yetu tumechoka kuonewa lazima vijana wetu waende Madagascar kusakata kabumbu tff komaeni tu
 
Tumaweza tukapata fursa ya kwenda alafu huko tukawa tunapewa dozi za uhakika tukaanza tena tungejua.
 
Kwani Congo Brazzaville kuna vita gani? Waongo hawa wameshajua wanaumbuka live
 
Very Funny Indeed!!!! wakati wa mechi amekuwa akipatikana lakini wakati wa kwenda kipimwa vipimo na jopo la madaktri kuhusu umri wake imeshinidikana.
Kwenye hili ningekuwa ni CAF ningeiadhibu shirika la mpira la nchi hiyo na kumfungia mchezaji huyo na mengine yangeendela ili kuleta nidhamu kwenye mpira.
 
Tunataka tupitie mlango wa nyuma? TFF nashauri waachane tu na hii habari, tutaenda kutia aibu huko.
 
November 19, 2016

Kama ilivyoripotiwa awali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

TFF ilikata rufaa ya mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF). Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo Langa Lesse Bercy, CAF iliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo Cairo Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake.

Langa anatakiwa kupimwa kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance). kipimo ambacho TFF iliagizwa na CAF igharamie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia gharama za vipimo.

Kutoka kulia ni Langa Bercy wa Congo anayedaiwa kudanganya umri

Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo Misri, ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.

Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko vitani eneo hilo halikutajwa, TFF bado inafuatilia na kuhakikisha haki inatendeka.

Imetolewa na TFF
 
November 19, 2016

wa kwanza kulia langa lesse bercy anaedaiwa kuwa kijeba

Imetolewa: TFF
 
Haki gani mkuu!!!
Ya kung'ang'ania kushinda?

Uchumi umebana, hali mbaya jamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…