Rufiji, Pwani: Mahabusu aliyekuwa na kesi ya mauaji afariki kwa kupigwa na radi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Mahabusu ambaye alikuwa na kesi ya mauaji, Musa Haji Mchana, alipigwa na radi na kupoteza uhai Oktoba 13 kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ukanda wa Pwani.

Aidha wafungwa wanne wamejeruhiwa na radi hiyo na hivi sasa wako hospitali wakiendelea na matibabu. Wafungwa hao ni Richard Simau, Issa Haji, Hashim Rashid na Ismail Mtupa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema gereza lililopata kadhia hiyo ni gereza la Wilaya linaloitwa Mng’aro lililoko Kibiti.

Kamanda amesema hakuna wafungwa wala mahabusu waliotoroka baada ya kupigwa na radi hiyo na ulinzi umeimarishwa zaidi.
 
Kwakuwa sikuhizi hakuna adhabu ya kunyongwa, basi mahabusu kachagua fungu lake analog stahili.
 
Hukumu imetolewa baada ya kusikilizwa na mwenyezi Mungu, hakuna rushwa hapa.
 
Kwakuwa sikuhizi hakuna adhabu ya kunyongwa, basi mahabusu kachagua fungu lake analog stahili.
Hizi ni kati ya taarifa adimu sana kutolewa, kunawakati naweza kujitoa ufahamu nikapingana na taarifa hii- isije ikawa alipata ajali tofauti ya ndani kwa ndani, ni fikra tuuuuuu
 
Back
Top Bottom