Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Copper blocks hizo zimetengenezwa kutoka kwenye nyaya ambazo zimeibiwa TANESCO na TRC ilikuficha uhalisia wake.
Chanzo cha kukamatwa kwao ni baada ya kukamatwa kwa gari moja aina ya Fuso iliyokuwa imebeba shehena ya blocks na nyaya za copper walizotoa kiwandani kwao kwa ajili ya kwenda kuzificha baada ya kuona operesheni kali ya Polisi inayoendelea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kubaini, kuzuia na kuwakamata wale wachache ambao hawataki kufuata njia halali za kujipatia kipato na badala yake wanahujumu miundombinu ya Serikali.
Aidha operesheni hii itaendelea hadi mtu wa mwisho aliyehusika katika hujuma hizi atakapo kamatwa.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kipolisi Rufiji