TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Kifo cha huyu jamaa! Kiliniacha hoi sana! Naweza sema kwamba alikua na hili tatizo la figo muda kidogo,lakini nakumbuka kitu kimoja!

Kuna siku Magufuli akiwa Rais,alisema Makonda na Ruge ni vijana wake,wapatane wakae chini wayamalize,pale kwenye jukwaa Magufuli aliwaita wote Makonda na Ruge,na akasema wanaposhuka kutoka kwenye jukwaa washikane mikono!

Wote tuliona kwa macho yetu,Ruge alikataa kushikana mkono na Makonda,baada ya hapo tukaja sikia tu Ruge anaumwa yupo South Africa anatibiwa!

Hadi siku ya Mauti,Magufuli ndiyo alitoa taarifa ya kifo cha Ruge!

Kutokushikana mkono na Makonda,wakati Rais katoa amri,tena mbele ya watu wengi,lilikua ni chukizo kubwa sana kwa mnene!
 
Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amefariki dunia usiku huu Februari, 26 akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na Watanzania kuomboleza kifo hicho huku akituma salamu za pole kwa wafiwa wote wakiwemo Ndugu, Jamaa na Marafiki wote


UMOJA WA MATAIFA(UN) WAMLILIA RUGE MUTAHABA

We join the rest of the country in mourning the loss of Ruge Mutahaba.

We were very happy to have worked with him to spread the message of the #GlobalGoals all over #Tanzania.

R.I.P Ruge @ALVARO_UNTZ



Ruge Mutahaba Biography


Ruge alizaliwa Brooklyn New York Marekani mwaka 1970, Primary School amesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha akahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo alipomaliza darasa la saba.

Kisha akasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo akarudi Marekani ambako alienda kusoma San Jose University California ambako alichukua BA in Marketing na BA in Finance, kozi zote alisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo akarudi tena Tanzania.

Kuanzishwa kwa Clouds FM.

Wakati yupo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, yeye Ruge akawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo waka-build good friendship. Sasa, aloporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yake, Joseph Kusaga akamshawishi sana abaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo alipojikuta yupo Clouds Entertainment.

Vyanzo vinadai kuwa Mutahaba hakuwahi kufunga ndoa rasmi lakini alikuwa na mahusiano na Zamaradi Mketema na walipata watoto wawili wanaoitwa Juju na Shubi na wengine watu. Jumla kaacha watoto watano.

Kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo Mutahaba alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo, kwa maana hiyo alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu hadi mauti yalipomfika tarehe 26 Februari 2019.

Pia Soma viambatanisho vifuatavyo


UPDATES
27/2/2019: RUGE MUTAHABA UNATARAJIWA KUWASILI NCHINI IJUMAA YA MACHI 1,2019

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa ya Machi 1,2019 na utazikwa Bukoba, mkoani Kagera wiki ijayo.

Akizungumza leo Jumatano Februari 27, 2019 nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam, msemaji wa familia Annik Kashasha amesema taratibu za kuuleta mwili zimeanza kufanyika kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akitibiwa.

“Mwili wa marehemu utarejeshwa hapa nchini siku ya Ijumaa (Machi 1) na siku ya Jumapili (Machi 3) utasafirishwa kwenda Bukoba kwaajili ya mazishi.

Kashasha amesema shughuli za kumuaga Ruge ambaye ni mwanzilishi wa semina za fursa zitafanyika siku ya Jumamosi.


1/3/2013: MWILI WA MAREHEMU WAWASILI DAR ES SALAAM KUTOKA AFRIKA KUSINI

Siku ya Leo Mwili wa Rugemalira Mutahaba umewasili Tanzania kutoka Afrika Kusini ambako umauti ulimkuta wakati akipatiwa matibabu. Mwili wake umezungushwa baadhi ya mitaa ya Dar es Salaam ili kutoa fursa kwa wananchi kuaga mwili huo.

Mwili huo ulikuwa na msafara ambao ulianzia Airport - Tazara - Buguruni - Bomani - Magomeni - Tandale - Sinza - Bamaga - ITV - Clouds - Lugalo

Zaidi fuatilia video iliyoambatanishwa chini




2/3/2019: MATUKIO KUTOKA KARIMJEE, DAR - KUAGA MWILI WA RUGE MUTAHABA

View attachment 1037673
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba
Leo mwili wa Ruge Mutahaba unaagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli amewaongoza wakazi kuaga mwili.

Pia wanasiasa na watu wengine mashuhuri wamehudhuria.

Baada ya kuaga mwili, utasafirishwa kwenda Bukoba Vijiji kwa ajili ya kutoa fursa ya wanabukoba kuaga na hatimaye mazishi ambayo yatafanyika siku ya Jumatatu ya tarehe 4 Machi, 2019.

Familia ya Ruge Mutahaba imesema wanatambua Ruge aliwahi kuwakosea watu kwa kuwa yeye ni binadamu hajakamalika. Mtoto mkubwa wa Ruge amesema "Familia inaomba msamaha kwa niaba yake." Lakini pia wapo waliomkosea Ruge na pengine wapo wanaoendelea kumkosea. Familia imesema "TUMEWASAMEHE WOTE....TUENDELEE MBELE"

View attachment 1035994
Mtoto mkubwa wa Ruge Mutahaba, Mwachi Mutahaba akisoma wasifu wa baba yake

View attachment 1036008
Caption; Watoto wanne(hao wadogo) wa Ruge Mutahaba, ameacha jumla ya watoto watano


View attachment 1035984
Viongozi mbalimbali waliohudhuria Viwanja vya Karimjee
View attachment 1035985
Rais Magufuli akiwafariji wafiwa
View attachment 1035987
Rais Magufuli akitoa heshima za mwisho
View attachment 1035986
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dr. Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa Salamu za mwisho

3/3/2019: MWILI WA RUGE MUTAHABA WAWASILI BUKOBA NA KUPOKELEWA NA MAMIA YA WANABUKOBA

Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba umewasili Bukoba kwa ndege ya Serikali iliyotolewa na Rais Magufuli. Mwili umepokelewa na mamia ya wakazi wa Bukoba wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ambaye pia aliongoza msafara mpaka kijinini Kiziru Kabale ambako makazi ya milele ya Marehemu yameandaliwa



View attachment 1037708View attachment 1037709
View attachment 1039240
Mwili wa Ruge ukiwa umewasili kijijini kwao

View attachment 1037738
Taswira ya nyumbani kwa Mutahaba


4/3/2019: MWILI WA RUGE WAAGWA VIWANJA VYA GYMKHANA BUKOBA NA KUZIKWA KIJIJINI KIZIRU,KABALE

View attachment 1039241View attachment 1039243View attachment 1039242

RUGE ATAKUMBUKWA NA WANABUKOBA KWA KULETA AZIMIO LA VIJANA LA BUKOBA
View attachment 1039246


Miaka inaenda it's almost 6 years.
 
Back
Top Bottom