TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

CCM inawatakia jioni njema.
kunywa maji kwa wingi na epuka pombe kali kuokoa figo ewe mpiga kura, baada ya 2020 una uhuru wa kutopangiwa maana figo ni yako
 
Mbona umeulizwa swali jepesi unarusha cheche?Kwa hiyo na mzee Mutahaba (kama naye baba yake yupo)akazikwe kwa baba yake akifa?

mkuu huwa nakuona mwelewa kumbe nawe mweupe hivi (nimeshindwa iona tofauti yako na selleboss yule diwani huko tanga)

tunazungumiza msiba kuwa kwa baba yake na sio kwake ww unakuja na mambo ya kuzikwa

kwani atakapo zikwa Ruge ni wapi kama si kwa babu yake huko bukoba. wapi umesikia ama kuambies atazikwa kwa baba yake (ulipo msiba hapo dawa)
 
Hii imenishangaza sana kwa kweli wahaya wameanza ujenzi wa kaburi leo mazishi siku tatu zijazo mbona mapema sana au litakuwa la ghorofa? au litakuwa lina underground
Kwani kuna ajabu gani kujenga mapema?

Ughaibuni kuna makaburi yanachimbwa kabla hata atakae zikwa hajulikani. Yanauzwa.

Mafarao walijenga makaburi kwenye pyramid miaka kibao kabla.

Njombe kuna mganga wa tiba za asili kajenga kaburi lake la gharama tena gjorofa na underground kabla hajafa wala kuugua anasema anataka liwe la makumbusho.

Usikariri mazoea au mila ya sehemu flani ukadhani kwa wengine kuna ubaya.
 
Umeenda haraka naamini haujanipata uzuri.Swali ni hivi;Ruge alikuwa ni mtu mzima katika jamii.Japokuwa sijakataa kwa wazazi wake ataendelea kuwa "mtoto".Hoja ni kuwa,kwa nini msiba haukufanyika/kupokewa nyumbani kwa Ruge na badala yake ukiagwa tu uelekee kwa baba yake mzee Mutahaba?Kuna hoja kuwa ni maamzi ya familiakuwa azikwe kwenye makaburi ya familia.Ndiyo maana nilikuuliza swali la kizushi.Ina maana na mzee Mutahaba atarudi kuzikwa kwa babu wa Ruge?Ni swali chokonozi kama ukiliendea kwa umakini.Tafakari.
 
hakuna swali chokonozi hapo sema huna uelewa na kabila la wahaya

mara nyingi wahaya/wachaga huwa na makaburi ya ukoo ko kuna uwezekano mkubwa wa mzee kuzikwa huko.

kama umefanikiwa kuona kaburi la ruge linapo andaliwa kuna makaburi mengine jirani. kifupi ilo eneo huzikwa watu wa ukoo wao.
 
Uko sahihi iwapo tu familia ya Mzee Mutahaba ingekuwa mbali na Dar, au kama huyu mzee asingekuwepo mahali pa karibu kwa sababu yeyote ile. Kwa sasa hivi kwa vile yupo, msiba unakuwa ni wa Mzazi, Prof Mutahaba.Nawapa pole sana wafiwa!
Pole sana kwa kweli..na hao ndiyo wafiwa, wengine wavimba macho tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…