Ruge mutahaba ajibu mashambulizi dhidi ya tuhuma za lady jaydee

Joseph Kusaga naye anajitetea lini? maana watuhumiwa ni watatu.

Joey hana haja ya kuijtetea. Ajitetee nini sasa wakati hakuna tuhuma mahsusi dhidi yake zaidi ya 'kuwabania' wasanii. Ukiuliza wasanii gani, wapi, na lini 'walibaniwa' hupati jibu.

Ila mimi nashangaa sana na bado nitaendelea kushangaa hivi Ruge ndio nani nchi hii? mbona tunakwenda kulicheza Ngwasuma bila ushawishi wa Clouds? au tunavyokwenda Twanga ni kwa ushawishi wa Clouds?

Swali zuri sana hilo. Ila kwa jinsi watu wanavyolialia utadhani Ruge ni bonge moja la kingmaker na unaweza hata kudhani Tanzania nzima hakuna vituo vingine vya redio zaidi ya Clouds.

Bwana mdogo naona sasa umeanza kuwa na akili. Super big up.
 

Mashabiki wa Ruge mbona mnakimbilia kutukana badala ya kushirikisha ubongo? Kaeni chini tafakarini, Jay Dee sio wa kwanza kumchana Ruge, wengi wanachukizwa lakini hawasemi. Hata hao waliopo THT ukiwauliza kimya kimya watakuambia, usisapoti usichokijua labda kama unanufaika.
 


Haya Gadner ana 40 na Jide ana 34
 
Hah hah hah hah haaaaaaaaaaah walete walete walete walete...
Tola umenifurahisha sana.
Sasa ukitaka ugomvi na Jide ni hapo kwenye suala la Umri.

Haya tusubiri jibu sasa

kuna jamaa yangu yeye alisoma na JIDE class moja, huyu jamaa ndo alikuwa mdogo kwa umri kipindi hicho, kwasasa huyu jamaa ana umri wa miaka 35 so ukikadiria jide atakuwa na umri wa kati ya 35-40!
 
Vita ya maneno humalizwa kwa vitendo,wakutane wasemezane
 
Hata kama kuna tatizo,alichofanya Jide sio njia nzuri ya kulitatua..
 
Ruge kajieleza Vizuri sana, Ile ni Radio binafsi haipangiwi cha kufanya,Mbona Majic hawajalaumiwa kwa Kumpotezea Diamond, Jide kastuka watu washampokea kijiti ndo anaweweseka, Kwa sebastian Ndege atakalishwa sana!
 

Sahizi umeonesha una busara.
 

Ishu sio Idadi ya wanaomchana ishu ni Facts, do they have a Concrete Points? Kwenye Soko huria huna ruhusa ya kusema unadhulumiwa na mshiriki wako wa Biashara kama hakuna maslahi unachapa mwendo, kama nyimbo zako hazipigwi ni maamuzi binafsi ya wenye Radio, mbona jide aliwapiga biti Clouds wasipige nyimbo zake lakini Ruge hajalalamika, mbona radio na tv nyingi tu huwa hazitoi taarifa za watu wasioelewana nao na hakuna Tatizo, Mengi hatangazi habar za Manji wala Riostam na mambo ni shwari tu?jide analalamika kupewa laki nane kwenye Fiesta yeye alitaka kupewa ngapi? Alikuwa na Mkataba au alipanda stejin kiushkaj tu.
 
EA radio ilimbania Ray C. Kwa mujibu wa Ruge,alimchukua Ray C hadi kwa mzee Mengi,akaelekezwa matatizo yake,tatizo likaisha!
 
Kuna wakati vitu vingine vinashangaza kidogo, sasa kama hawa Wasanii wanashindwa ku survive nyumbani wakienda Japan kama Fresh Jumbe au Sweden kama Dekule Vumbi watayamudu maisha?

Kuna wakati Ray C alikuwa anafanyia kazi zake Kenya sasa kule napo kuna Ruge na Clouds? hivi Msondo ngoma kweli wanabebwa na Clouds?

Ukiangalia kwa undani sana utakuta kuna waliopata pesa nyingi kuliko hata walivyostahili zikawalevya sasa salio linashuka wanaona ilikuwa ni haki yao.

Hawa hawajuhi mpaka leo tunawapa nauli ya Daladala Wanamuziki wa Sikinde na Msondo kwenda kwenye Show maana wamepigika.

Kuna issue ya Fiesta JD kilipwa laki nane, sijui kama walikubaliana au lah, lakini mimi mwaka juzi tu niliwachukuwa Twanga bendi nzima na wacheza show siku ya Jumatano kwa laki saba tu.

Last but list, mimi si bendera fuata upepo huwa na base kwenye fact tu.
 
maelezo ya Ruge leo yalikuwa mazuri laiti ingekuwa hii ni kesi mahakamani kashinda kabisa
 

Matola Sasa nakutambua rasmi...... Nadhani sasa utakuwa unanielewa pia huwa Sikurupuki! Endelea kusimama kwenye fact.
 
Last edited by a moderator:

Wewe nahisi Uwezo wako wa uelewa ni mdogo sana! Unaijua kauli ya "MNYONGE MNYONGENI LKN HAKI YAKE MPENI"? Kulalamikiwa kwa Ruge haina maana kila utakachokisikia umuone mbaya tuu! Kuwa muelewa Ishu ya Ugomvi ni Bendi ya Sky light kujitangaza clouds na kuchukua Wanamuziki wake yule Bibi anashindwa kujipanga Upya anawateka watu wenye uwezo mdogo wa uelewa km wewe kusema Ananyonywa na nyimbo hazipigwi Anashindwa kuelewa Kulikuwa na Bendi hapa mjini Inaitwa AKUDO leo hii haipo na wakati Inatamba hatukuwasikia TWANGA wakisema Wananyonywa wala wanabaniwa.
 
maelezo ya Ruge leo yalikuwa mazuri laiti ingekuwa hii ni kesi mahakamani kashinda kabisa
Ni kwa nini asishinde kama wasanii wenyewe malalamiko yao ni jumla jumla tu wala hakuna hainisho au contract kwamba Ruge ali breach contract ya million 5 akalipa laki 8?

Kuna kipage ushuzi kipo Facebook eti kifo cha Clouds sasa mimi nimewauliza mnaweza kuiuwa Clouds kwa kucoment matusi dhidi ya Ruge hapa facebook? watu wanatokwa na povu lakini hakuna hata mmoja anayetoa scientific strategy ya kuiwa clouds, is too childish.

Kuna kapumbavu kengine kanajiita sukari ya Warembo tunasubiri baada ya miaka miwili naye aanze kutokwa na povu, nampenda Mr Nice hajalaumu mtu kwa kufulia analia na nafsi yake tu.
 
Ninachokiona mimi toka kwa Ruge ni kwamba kwanini aende kuongelea Shutuma zake kwenye Radio yake ya Clouds tena kwenye kipindi cha Power Breakfast na sio kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo?
1.Anaogopa maswali ya waandishi wa habari?
2.Anajua jamii itafahamu uhalisia wa malalamiko dhidi yake?
3.Anaogopa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…