Ruge na Clouds wanyoosha mikono kwa Rubby

msemakwelitz

Member
Joined
Sep 23, 2016
Posts
15
Reaction score
38
Clouds ikiongozwa na mkurugenzi wao RUGE walisusa kupiga nyimbo za mwanamziki Rubby kama walivyofanya kwa LADY JD kutokana na Rubby kuwagomea kufanya show ya FIESTA kutokana na malipo madogo yanayowanyonya wasanii badala ya kufanya makubaliano wakaamua kumkomoa kwa kutokupiga nyimbo zake lakini leo clouds radio na jana CLOUDS TV wamepiga nyimbo yake na kuionesha ktk TV aliyoimba na yemi alade wa Nigeria ktk Coke studio kutokana na kubanwa na mkataba wao na COCACOLA ...

Viva Rubby na na JAY DEE kwa kujielewa na kuwa na msimamo [emoji1434][emoji1434] wataelewa tu. Wasanii wengine mna kila sababu ya kujielewa na kuwa na msimamo badala ya kupelekwa pelekwa na CLOUDS FM.
 
Clouds nyimbo za rubby wanapiga kama kawaida.siku ya msiba wa sita walipiga nyimbo ya goodnight zaidi ya Mara 5 huyo JD alikataza mwenyewe wasipige nyimbo zake
Mkuu we huwajui clouds yani wale wakigombana na msanii wanasitisha kupiga nyimbo zake Kama huamini ngoja uone Kama watapiga nyimbo za TID tena ndo maaana ruby aliwaita mungu mtu
 
Bila wasaniii kuungana na kuukataa unyonyaji kwa pamoja hawezi kuwafanya lolote Clouds.
Clouds waishajua Njaa za hawa wasaniii na watawafanya wanavyotaka na huyo sijui rubby hana mda mrefu ataenda kupiga magoti.

pili wasaniii wenyewe ndio wapi hapa Bongo? kwa nyimbo zipi za maana walizonazo? acheni Cloods wapige pesa wao walichungulia fursa mapema.

Sugu na usugu wake alikaaza mwenshowe akaja kuachia mwenyewe tena akiwa mbunge. unadhani hicho sijui ki rubby kina nini?
 
Mkuu we huwajui clouds yani wale wakigombana na msanii wanasitisha kupiga nyimbo zake Kama huamini ngoja uone Kama watapiga nyimbo za TID tena ndo maaana ruby aliwaita mungu mtu
Huyu TID ambaye jana alikuwa uwanjani katika mechi ya clouds na wasanii
 
ila ukiangalia clouds wanajitahidi sana kupiga nyimbo za wasanii wa ndani kiukweli!
Ila ukiangalia chanel nyingine unakuta sio kivile sana kama promo inayofanyika clouds!
Bado haijajitokeza chanel ambayo italeta upinzani wa kupromote wasanii wa nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…