rugberna97
Senior Member
- Sep 22, 2016
- 147
- 126
Mwanzilishi wa THT na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa clouds FM, Ruge Mutahaba amesema kuwa licha ya Ruby kujiondoa kutoka kwenye usimamizi wake hawezi kushuka kimuziki sababu ana kipaji cha hali ya juu.
Akiongea na mtangazaji wa mashujaa FM ya Lindi Baby Dinny Ruge amesema, "Mimi naamini Ruby ana kipaji sana. Binafsi ana kipaji cha ukweli kabisa wala sio uongo"alisema Ruge. "Kama atashuka labda itakuwa ni mambo yake tu mwenyewe lakini sidhani kama kuna namna kipaji chake kitashuka" aliongea na kumshauri kuwa apate watunzi wengine wazuri wa kumsaidia. Amedai kuwa nyimbo zake tatu na yule, sijutii na forever ziliandikwa na Amini na Barnaba.
Kwa upande mwingine Ruge amesema haoni kama kuna tatizo Ruby kuondoka THT kwa kuwa tofauti na wengine wanavyodhani THT si label bali ni kama chuo ambacho wasanii mbalimbali hunolewa,"Yeye ameona yuko tayari kivyake kwenda kwenye sehemu anayoweza kupata maslahi zaidi, ndio hivyo tu kwa hiyo sioni kama kuna shida"amesisitiza Ruge.
Pia amedai kuwa muda wowote muimbaji huyo atahitaji ushauri kutoka kwake milango ipo wazi kwani ataendelea kumchukulia kama mdogo wake.
Chanzo: BONGO5