Ruge: Ruby hawezi shuka kimuziki

Ruge: Ruby hawezi shuka kimuziki

rugberna97

Senior Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
147
Reaction score
126
Mwanzilishi wa THT na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa clouds FM, Ruge Mutahaba amesema kuwa licha ya Ruby kujiondoa kutoka kwenye usimamizi wake hawezi kushuka kimuziki sababu ana kipaji cha hali ya juu.

Akiongea na mtangazaji wa mashujaa FM ya Lindi Baby Dinny Ruge amesema, "Mimi naamini Ruby ana kipaji sana. Binafsi ana kipaji cha ukweli kabisa wala sio uongo"alisema Ruge. "Kama atashuka labda itakuwa ni mambo yake tu mwenyewe lakini sidhani kama kuna namna kipaji chake kitashuka" aliongea na kumshauri kuwa apate watunzi wengine wazuri wa kumsaidia. Amedai kuwa nyimbo zake tatu na yule, sijutii na forever ziliandikwa na Amini na Barnaba.

Kwa upande mwingine Ruge amesema haoni kama kuna tatizo Ruby kuondoka THT kwa kuwa tofauti na wengine wanavyodhani THT si label bali ni kama chuo ambacho wasanii mbalimbali hunolewa,"Yeye ameona yuko tayari kivyake kwenda kwenye sehemu anayoweza kupata maslahi zaidi, ndio hivyo tu kwa hiyo sioni kama kuna shida"amesisitiza Ruge.

Pia amedai kuwa muda wowote muimbaji huyo atahitaji ushauri kutoka kwake milango ipo wazi kwani ataendelea kumchukulia kama mdogo wake.

Chanzo: BONGO5
 
Mbona hawapigi nyimbo zake kama anaamini kwenye kipaji cha huyo binti?
 
Maneno ya Ruge ni Ya kinafiki 100%....Pamoja na figisu anazimfanyia kupitia OSATA atashindwa tu.
 
Rubby katemwa na ruge na hata nyimbo zake ni marufuku kupigwa clouds. Ila mh! Rubby nae anadharau mwanamke yule sijapata ona......... Hata akiwa anafanyiwa interview ana maneno fulani ya kebehi sana ila kwakuwa amezinguana na ruge hakika kipaji chake ndio kinapotea hivyo hatoweza kushindana na akina ruge coz clouds media wana conection kubwa sana na wale jamaa kwa promo nawakubali. Pole sana dada yangu rubby ila nakusihi punguza dharau huko unapokwenda hata kama unakipaji ila ukiendekeza dharau utaangukia pua na utapotea kwenye ramani ya mziki.
 
Mastermind Ruge. Mweledi sana huyu jamaa kwenye bifu. Kasema kinyume.
 
Rubby katemwa na ruge na hata nyimbo zake ni marufuku kupigwa clouds. Ila mh! Rubby nae anadharau mwanamke yule sijapata ona......... Hata akiwa anafanyiwa interview ana maneno fulani ya kebehi sana ila kwakuwa amezinguana na ruge hakika kipaji chake ndio kinapotea hivyo hatoweza kushindana na akina ruge coz clouds media wana conection kubwa sana na wale jamaa kwa promo nawakubali. Pole sana dada yangu rubby ila nakusihi punguza dharau huko unapokwenda hata kama unakipaji ila ukiendekeza dharau utaangukia pua na utapotea kwenye ramani ya mziki.
Umeona eeh? Anajikuta sana huyu Dada, aura mama kasuku mwenye mimba mfyuu
 
kanakipaji, kiburi kinaweza muangusha. hivi kwenye video ya forever alimaanisha nini kuandika New York Texas?
 
Ruby!!! Hamna kitu pale.. Ni upepo tu ulivuma ukapita zake..
 
hiv dogo kumbe naye anatungiwa

Kwa taarifa yako hata Rihanna anagonga multiplatnums kama kuna nyimbo alizoandika mwenyewe (kama zipo) basi hata 5 hazifiki. Sasa we sijui unaishi Dunia gani!!!
 
Back
Top Bottom