RUGE tuamuangalie upande wa pili

RUGE tuamuangalie upande wa pili

Kila binadam anamapungufu yake na udhaifu wake.. wote mnaomdiss hapa mnamapungufu yenu pia yasiyofaa kuigwa na jamii.. Fateni yale mazuri aliyoyafanya hizo bullshit zingine achaneni nazo

kikubwa alichokua akikifanya ni kuwasaidia vijana kuinuka kiuchumi na kuwapa fikra za kimaendeleo na ndo kilichompa umaarufu. wala maisha yake binafsi hayajawahi mpa umaarufu kwanza hajawahi kuweka hadharani maisha yake binafsi wala mahusiano yake au familia yake au watoto wake alikua hataki kabisa kuvizungumzia kwenye media ni sisi ndo tunataka kuyachimba sana

Mambo ya vijana wa clouds kua sijui mashoga hayo ni maisha yao binafsi na ni uamzi wa mtu au mlitaka aanze kucontrol na maisha yao binafsi na tabia zao? Mbona clouds wapo vijana wengi tu waliooa na wadada walioolewa wanafamilia zao, na wanajiheshimu na boss wao hajaoaa?

Swala la yeye kuoa au kutooa halituusu chochote kwanza haya mambo ya mahusiano ni kitendawili huwezi jua alipitia nini mpaka hajaoa
Maana humu mitandaoni watu wanavyosema kwa uhakika ni muhuni ni muhuni Utafikiri walikua wanamsaidia kushika miguu ya hao madem wanaowataja wakati yeye anapiga pumbu.. vitu ambavyomuhusika hajawai kuviweka wazi lakini kuna watu wanajikuta wajuaaaajiiii! Acheni hizo bana hakuna mwenye uhakika kuhusu mambo yake ya mahusiano!

Sent using Jamii Forums mobile app
Jifunze kupokea maoni hata yale usiyoyapenda. Utajifunza mengi.

Don't take things too personal..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu kutokea msiba wake sifa lukuki zimekuwa zikitolewa kuhusu maisha na kazi zake ambazo nyingi ni za kweli. Lakini kama tujuavyo hakuna binadamu aliye mkamilifu hivyo ukitaka kumuelezea mtu halisi lazima na upande wa mapungufu yake uyagusie.

Kwangu mimi Ruge licha sifa zote , hakuwa mfano wa kuigwa kwa maisha ya kijana na nitaeleza sababu zaangu.

Ruge amefariki akiwa na umri wa miaka 49 lakini hakuwa na maisha ya familia, kwa maana ya mke na watoto.

Ameishi maisha ya kihuni yasiyofaa kuigwa kwa vijana wanaotafuta kuishi vizuri. Ruge angekuwa ni mtu aliyefanikiwa kimaisha, msiba wake ungekuwa nyumbani kwake na sio kwa wazazi wake.

Vijana wengi alioibua vipaji vyao japo wengi wamefanikiwa kupata pesa lakini wengi wao wanaishi maisha ya kihuni.

Ndoa zao zimeshindikana na wamekuwa watu wa kuonyesha vitendo vya aibu katika jamii. Hili nalo naweza kulihusisha na Ruge kwani mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake.

Zipo pia tetesi kuwa hata pale Clouds wafanyakazi wengi wanajihusisha na vitendo vya kishoga na kwa msemo wa kiswahili kuwa lisemwalo lipo, huenda likawa na ukweli ndani yake na Ruge akawa ni sehemu ya jamii hiyo.

Nimalize tu kwa kusema Ruge amejitahidi katika sehemu moja ya maisha na kufanikiwa, kiuchumi, ila upande wa pili wa maisha , kimaadili, hakufanikiwa hata kidogo.

Kama binadamu mwenye imani kiasi, namwombea kwa muumba wake aipumzishe roho yake mahali zinakopumzishwa roho zote , Amen

kupanga ni kuchagua , kila mtu ana maisha yake
 
Naunga mkono hoja. Thread hii inabalansi zile sifa za utukufu anazopewa ndugu yetu Ruge. Sio chuki wala!

Ni dhahiri jamaa kuna sehemu aliteleza. Hasa huko kwenye maadili. Watakaopinga watapinga tu kiholela lakini moyoni wanakiri maana ushahidi upo wazi wazi.

However, genius fellows ndivyo walivyo lakini. Wengi wanafeli kwenye mahusiano. Labda ni dhaifu sana eneo hilo au hawana utaalamu nalo hivyo wanababatizwa bila ya kujua.

Tuliobaki tujifunze!

Sent using Jamii Forums mobile app

labda hakutaka kuwa na familia
 
Back
Top Bottom