Ruhusa ya mikutano ni mtego kwa CHADEMA

Hivi hakuna namna ukawa jukwaani ukasema maneno ya upinzani bila kuzua utata, yaani bila lugha za kichochezi wala matusi?
Mapepo yaliyompagawa mtu huwa hayaondolewi kwa lugha nyororo na ya kulemba. Ni lugha ngumu na amri kuu, na kwa mamlaka ya mbingu. PEPO ULIOLAANIWA TOKA.
 
Hivi hakuna namna ukawa jukwaani ukasema maneno ya upinzani bila kuzua utata, yaani bila lugha za kichochezi wala matusi?
Kauli za kisiasa, hasa za kishindani zilinganishe na wewe unaposhindana na wenzako kupata mchumba.

Mpo vijana wawili ama watatu kwa mfano, mnagombania mchumba mmoja ili kukubaliwa kumuoa.

Je utakapokuwa unajieleza kwa huyo msichana, utawapamba kwa maneno hao mahasimu zako?

Ni kawaida sana 'kupondana' na hakuna matusi yoyote viongozi wa CDM wanatoa, sema matendo yanayofanywa na Serikali kwa raia ndiyo matusi halisi na ni zaidi ya matusi, ni unyama!

Sasa Cdm wanapokuwa wanaexpress matusi yanayofanywa na Serikali pamoja na viongozi wake, ndipo wanapoonekana kama wachochezi!

Sisi wadau mbona hatuyaoni matusi hayo wala uchochezi wowote bali twaona tafsiri yenye kuyapembua matendo maovu ya Serikali?

Kusema: 'baba funga zipu umekaa uchi', je hapo mtoa taarifa atakuwa katukana au katoa taarifa ya kuzuia huyo baba asiendelee kuonesha matusi?

Tuwe tunapima dhamira ya maneno atoayo mtu, hata kama mtu huyo haumpendi.
 
Sasa kama ni hivyo:
Huyo Katambi atatembea nchi nzima kuwasaka watu wa CHADEMA bila polisi? Kama polisi wameruhusu, Katambi akatae,itabidi yeye mwenyewe akatekeleze katazo lake, au siyo?

Pili, kama viongozi wa CCHADEMA watakuwa na hofu hiyo unayoeleza wewe, ya kukamatwa kwenye mikutano; kuna kipi kitazuia hao hao kukamatwa mahali popote. Au watafunga midomo yao wasitamke tena neno lolote kwa kuogopa kukamatwa?

Kama hali inakuwa hii unayoieleza wewe hapa, si hao CHADEMA pekee watakamatwa. Kila atakayeonekana hakubaliani na wanayoyataka hao wakamataji, watakamata tu, bila kujali ni CHADEMA au la.
 
CCM ni Chama Cha Mashetani
 
Hivi hakuna namna ukawa jukwaani ukasema maneno ya upinzani bila kuzua utata, yaani bila lugha za kichochezi wala matusi?
Hiyo ni lugha ya aina gani; kuna kipimo cha lugha hiyo kinachoopambanua ukisema hili ni tusi na hili siyo tusi?
Ni nani huyo anayeshikilia kipimo hiki cha "lufgha ?

maneno yoyote yatakayomuudhi Samia hayo ni matusi hata kama ni maneno ya kweli?
 
Na ndio maana gazeti la NIPASHE la leo Alhamis tarehe 30/7/2026 limeruka na habari " WAZIRI AKINZANA NA POLISI"...wasije tu wakaitwa
 
Zuio bado lipo palepale kwani lilitolewa na waziri mambo ya ndani, halikutolewa na polisi ambaye yuko chini ya waziri kiutendaji.
Hii nchi haieleweki Mkuu.
Nisije nikasema Uongo.
Katiba inasiginwa na Kubakwa.

Waziri hana Mamlaka ya kutangaza hali ya Hatari.
Kuna chombo kinaitwa Balaza la Usalama.

Waziri hana mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa

Waziri hana mamlaka mbele ya IGP
Kumuamlisha atakavyo.
Mambo ni mengi.
 
Zuio bado lipo palepale kwani lilitolewa na waziri mambo ya ndani, halikutolewa na polisi ambaye yuko chini ya waziri kiutendaji.
Hii nchi haieleweki Mkuu.
Nisije nikasema Uongo.
Katiba inasiginwa na Kubakwa.

Waziri hana Mamlaka ya kutangaza hali ya Hatari.
Kuna chombo kinaitwa Balaza la Usalama.

Waziri hana mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa

Waziri hana mamlaka mbele ya IGP
Kumuamlisha atakavyo.
Mambo ni mengi.
 
Tuwaache wapambane wenyewe, sisi ni watazamaji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…