Mchochezi
JF-Expert Member
- Feb 29, 2012
- 10,962
- 7,830
Anaitwa Rui Felipe da Cunha Faria au maarufu kwa jina la Rui Faria ambapo alizaliwa 14 June 1975 huko nchini Ureno. Kwa taaluma ni Kocha lakini pia ni mtaalam wa elimu ya viungo na mazoezi.
Kocha huyu amejipatia umaarufu kwa kufanya kazi na Kocha mwenye vituko vingi Jose Mourinho. Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2001 na toka hapo wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja na kuwa maswahiba wakubwa hata nje ya kazi yao.
Rui Faria ndiye kocha msaidizi wa Jose Mourinho katika kila klabu Mourinho anayoenda kufundisha yaani kwa kifupi unaweza ukamuita Jemedari wa Jose Mourinho. Wamekuwa wote katika vilabu vya Uniao Leiria, Porto (2002-2004), Chelsea (2004-2007), Inter Milan (2008-2010), Real Madrid ( 2010-2013), Chelsea (2013-2015), Man Utd (2016-).
Katika klabu zote hizo Rui Faria amekuwa kama msaidizi wa Mourinho na mtu anayaeaminika sana na Mourinho. Wawili hawa wameshibana kiasi cha kwamba Rui Faria aligoma kuwa kocha anayejitegemea licha ya kuwa na vyeti vyote vya ukocha na badala yake yeye amejikita katika benchi la ufundi la Mourinho huku akiwa kocha msaidizi katika kila timu anayoenda Mourinho. Ukimuona Jose Mourinho basi jua nyuma yake yupo Rui Faria. Na ukimuona Rui Faria basi jua nyuma yake yupo Jose Mourinho, wawili hawa wanafanana sana tabia na hulka zao.
Rui Faria na Mourinho wakiwa Chelsea mwaka 2004
Rui Faria na Mou wakiwa Inter Milan mwaka 2009
Rui Faria na Mou wakiwa Real Madrid
Rui Faria na Mou wakiwa Chelsea kwa mara ya pili 2015
Rui Faria na Mou wakiwa Man Utd
Kama ilivyo kwa Mourinho, Rui Faria nae ni mkorofi na ameshatolewa nje ya benchi na waamuzi zaidi ya mara tano katika career yake ya ukocha akiwa na Mou.
Rui Faria na Jose Mourinho maisha yao nje ya kazi.
MWISHO