Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Rui Pinto ni jina ambalo huenda mashabiki wengi wa Manchester City hawalijui na wasilipende kuliskia, lakini nyaraka za siri alizovujisha zilisaidia kufichua mambo ya ndani ya klabu hiyo na zikahusishwa na uchunguzi mkubwa wa masuala ya fedha katika soka la England.
Pinto, raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 37, alianzisha tovuti yake ya Football Leaks mwaka 2015 akisema alitaka kufichua "upande wa pili wa soka usiojulikana".
Kupitia Football Leaks, alianza kuchapisha nyaraka za siri kutoka ndani ya vilabu, zikiwemo barua pepe na taarifa kuhusu mikataba ya udhamini, malipo na miamala mingine ya kifedha.
Miaka kadhaa baadaye, mamilioni ya nyaraka hizo ziliingia mikononi mwa waandishi wa habari wa uchunguzi barani Ulaya na kufichua taarifa kuhusu baadhi ya majina makubwa katika soka.
Miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa ni taarifa zilizohusisha Manchester City na masuala ya fedha, ambayo baadaye yakawa sehemu ya mazingira ya uchunguzi mkubwa wa Ligi Kuu ya England
Lakini Pinto mwenyewe amekuwa mtu wa utata: kwa baadhi ya watu ni mtoa taarifa aliyefichua mambo ambayo umma ulipaswa kuyajua, huku wengine wakimwona kama mdukuzi aliyepata taarifa hizo kwa njia haramu.
Alivyoanza na alivyotaka haki ionekane
Safari ya Pinto ilianza katika mji wa Vila Nova de Gaia, upande wa pili wa Mto Douro kutoka Ureno. Baba yake alifanya kazi katika kiwanda cha viatu kabla ya kujihusisha na biashara ya vitu vya kale, huku mama yake akifariki, Pinto akiwa na umri wa miaka 11.
Mwalimu wake wa zamani, Mario Falcao, anamkumbuka kama kijana aliyekuwa mchangamfu, mwenye uwezo wa kutumia kompyuta na aliyekuwa na udadisi mkubwa. Wakati mwingine alikuwa akikosa masomo, lakini uwezo wake wa teknolojia ulionekana mapema.
Credit: BBC Swahili