TANZIA Rukia Juma(Mama yake Isha Mashauzi) amefariki dunia

TANZIA Rukia Juma(Mama yake Isha Mashauzi) amefariki dunia

R.I.P rukia....dah na ile ngoma ya mama nipe radhi ni hatari..hasa pale anapoanza ...aaah mwananguuuuu,,,hii ndio duniaaaa...asee
 
Poleni sana Isha msiba mzito sana huo, Mungu akutie nguvu katika kipindi hichi kigumu unachopitia. May God rest her soul in eternal peace
 
Alikuwa na sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni, alale pema
 
Aliyewahi kuwa muimbaji wa bendi ya ToT Rukia Juma ambae pia ni mama mzazi wa Isha Ramadhan (Isha Mashauzi) afariki Dunia , Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema.

=====

Mmiliki na mwanamuziki wa kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani maarufu ‘Isha Mashauzi’ amepata pigo baada ya kumpoteza mama yake mzazi, Rukia Juma aliyefariki dunia leo Mei 29, mwaka 2019.

Bi Rukia Jumaa ambaye pia alikuwa mwimbaji wa taarabu katika bendi ya Mashauzi Classsic na TOT Taarab, amefariki jioni hii njiani akiwa anapelekwa Hospitali ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa Abdul Said aliyejitambulisha kuwa ndugu wa karibu na familia hiyo, amsema Bi Rukia alikuwa anaumwa lakini alizidiwa na kufariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hopitali ya Taifa Muhimbili.

Said amesema kwa sasa Msiba upo nyumbani kwa Isha Mashauzi Kinondoni Hananasifu hadi itakapofika saa tatu msiba utapelekwa Mbezi kwa Msuguri alipokiwa akiishi Bi Rukia

Hili ni pigo kwa mwanamuziki Isha ambaye miaka minne iliyopita alimpoteza baba yake mzazi, Ramadhani Makongo.

Chanzo: Mwananchi
Pole kwa Wafiwa na R.I.P Mama Rukia Juma
 
Back
Top Bottom