A
Anonymous
Guest
Watumishi wa RUWASA ambao tulikua kitengo cha uchimbaji mpaka leo hatuelewi hatima yetu ni nini, kwani toka tusikie kwamba Idara ya Uchimbaji imeondolewa RUWASA na kupelekwa Ofisi za Bonde, na mashine zote za uchimbaji kukabidhiwa ofisi za Bonde, na ikisemekana kwamba baadhi ya Watumishi itabidi wapunguzwe RUWASA na kuhamia Bonde, yapata zaidi ya miezi tano sasa hatujui kinachoendelea juu yetu sisi Watumishi kwani shughuli zote za kiutendaji zimesimama.
Sambamba na hilo, mabadiliko hayo ambayo mpaka leo hatujui mwisho wake ni upi, yametuathiri kwenye suala la upandishwaji madaraja, kwani kwa taratibu za Kiutumishi ni haki yetu kupanda madaraja kwa mwaka huu mpya wa fedha lakini cha kushangaza mpaka sasa hatujaona mabadiliko yoyote kwenye akaunti zetu za ESS wala hatujajulishwa chochote.
Tunaomba mamlaka husika zitusaidie tuweze kupata haki zetu za msingi ikiwemo kupandishwa madaraja na tuweze kupangiwa kuendelea na majukumu yetu ya kikazi.