benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA), imetoa takwimu za maeneo vinara ya utapeli kwa njia ya simu ikionesha kuwa mkoa wa Rukwa ni kinara kwa wananchi wake kutapeliwa
Katika kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka uliopita 2022, kuanzia mwezi Oktoba 2022 hadi mwisho mwa mwezi Disemba matukio ya utapeli 12,613 yalirekodiwa huku takribani nusu ya matukio hayo yakiwa yametoka katika mkoa wa Rukwa.
Ripoti toka TCRA inaonesha kuwa asilimia 46 ya matukio hayo yametokea mkoani Rukwa ikifuatiwa na Morogoro (25%) kisha Dar es Salaam (13%)
Swali la kujiuliza hapa ni, je? wananchi wa Rukwa WANATAPELIWA KIRAHISI SANA, SIO WAJANJA au kuna siri gani nyuma ya hali hii?