Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Mheshimiwa Aesh Hilaly, ameonesha moyo wa upendo na kujali ustawi wa akina mama wajawazito kwa kuchangia mabeseni 1,000 kwa ajili ya wanawake wanaotarajia kujifungua katika hospitali mbalimbali ndani ya Wilaya ya Sumbawanga.
Hatua hii imekuja baada ya akina mama wa Mkoa wa Rukwa, katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, kuibua changamoto ya upungufu wa mabeseni kwa wajawazito hospitalini na kuomba msaada wa mabeseni 100. Mbunge Aesh Hilaly, baada ya kuguswa na changamoto hiyo, aliamua kuongeza idadi ya mabeseni hayo na kutoa mabeseni 1,000 badala ya 100 kama walivyoomba akina mama hao.
Mabeseni hayo yamesambazwa katika zaidi ya hospitali tano zilizopo Wilaya ya Sumbawanga, ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma kwa wajawazito na kuhakikisha wanajifungua katika mazingira safi na salama.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa Bi Silafu Jumbe Siku Machi 21 2025 amesema kuwa mchango huo ni sehemu ya jitihada za akina mama na Mbunge za kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa kina mama wajawazito, hususan wale wenye uhitaji mkubwa.
Wananchi wa Sumbawanga, hususan akina mama wajawazito, wameelezea shukrani zao kwa mbunge huyo kwa msaada huo, wakisema kuwa utaongeza faraja kwa kina mama wengi watakaopata huduma hospitalini.