PreGE2025 Rukwa: Mradi Mkubwa wa maji wakamilika Mafinga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wananchi katika Kijiji cha Kasekela kata ya Mfinga bonde la ziwa Rukwa Wilaya ya Sumbawanga, wameondokana na adha ya kuugua homa za matumbo baada ya Serikali kukamilisha mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi 422,498,413 .37 utakaohudumia wakazi wapatao 3500.

Kaimu meneja wa RUWASA wilayani humo Mefwu Wiliamu amebainisha kuwa mradi huo umefikia asilimia 75 ya utekelezaji na utahudumia zaidi ya wakazi 3500 na kwamba mradi huo utahudumia vijiji vya Msila na Kasekela na unatatajia kukamilika ifikapo May 2025.

Amesema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Jamaa Contraction Campani Limited kwa gharama ya shilingi 422,498,413.37 ambapo ununuzi wa malighafi za mabomba umefikia asilimia 90 na kwamba mradi huo utahusisha ujenzi wa tangi la maji lita laki moja lenye mnara wa mita 12 ulazaji wa bomba mita 1045 na ujenzi wa vituo vya maji 10 vyenye koki mbili.

Mapema akizindua mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile amepiga marufuku wananchi kuendesha shughuli za kibinadamu kando ya vyanzo vya maji na kusisitiza jamii kujenga utamaduni wa kutunza miundombinu ya maji ili kuifanya kudumu kwa muda mrefu.

Baadhi ya wananchi katika kijiji hicho wameipongeza Serikali kwa kuwajengea mradi huo na kwamba utawawezesha kuondokana na adha ya kuugua ugonjwa wa homa za matumbo ambazo zilikuwa zikijitokeza kutokana na kutumia maji yasio safi na salama.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Wameondokana na adha.
Serikali imekamilisha mradi.
Mradi umefikia asilimia 75.
Wananchi katika Kijiji cha Kasekela kata ya Mfinga bonde la ziwa Rukwa Wilaya ya Sumbawanga, wameondokana na adha ya kuugua homa za matumbo baada ya Serikali kukamilisha mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi 422,498,413 .37 utakaohudumia wakazi wapatao 35

Back
Top Bottom