Rukwa: RPC asema kuna kesi 88 za watu kutelekeza familia kwa mwaka 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Theospita Mallya ameeleza kuwa katika kipindi cha Mwaka 2022 kulikuwa na makosa 88 yaliyoripotiwa kupitia Dawati la Jinsia ya watu kutelekeza familia na watoto

Takwimu za mwaka 2021 zinaonesha mashtaka yalikuwa 87, hivyo kuna ongezeko na sababu kubwa ikitajwa kuwa ni ulevi kupindukia umechangia maamuzi hayo

Amesema “Pia tunaposema kuna mmomonyoko wa maadili ni kama vile suala la kuzaa lilivyo kwasasa, wengi wanaokuja kushtaki kutelekezwa wanasema hawajalipiwa mahari wala hawajaolewa, wanazaa wakiwa hawajuani vizuri matokeo yake wanakimbiwa.”

Chanzo: EATV
 
Inafikirisha sana
 
Kazi ipo.Wanawake mjitahidi kutafuta kazi za kuwapa kipato.Kulialia mnatelekezwa nao ni ulemavu wa akili.Haujatolewa mahari,haujaolewa ila mmepata mtoto,jitahidi umtunze.Ni wenu wote.
 
Mbona fureshiii tu, malezi ni jukumu la kike….. ajifunze kwa ndege na wanyama.
 
Hata kama wangeolewa kwa harusi kubwa na kulipiwa mahari na kutunukiwa cheti cha ndoa wanaachwa tu kwa kuwa hakuna maadili ya ndoa. Mkipendana mkaanza mahusiano ya kimapenzi na hatimaye kuzaa hiyo ndoa tosha, mambo mengine ni mbwembwe tu zilizozoeleka. Mahusiano ya kimapenzi yaangazie nini kitatokea wakati wa uhusiano huo linapokuja suala la mtoto kutokea. Huyo mtoto atunzwe kikamilifu na wazazi wote
 
Hao wanaotelekeza familia zao siku wake zao wakichukuliwa na watu wengine wa kuwapa mahitaji wasilalamike. Wapo wanaume hawana wake, sasa wakikutana na mwanamke aliyeachwa analia njaa akisaidiwa yeye mpaka watoto wake watamlaumu nani? Ukiacha wengine wanachukua
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Theospita Mallya ameeleza kuwa katika kipindi cha Mwaka 2022 kulikuwa na makosa 88 yaliyoripotiwa kupitia Dawati la Jinsia ya watu kutelekeza familia na watoto

Takwimu za mwaka 2021 zinaonesha mashtaka yalikuwa 87, hivyo kuna ongezeko na sababu kubwa ikitajwa kuwa ni ulevi kupindukia umechangia maamuzi hayo

Amesema “Pia tunaposema kuna mmomonyoko wa maadili ni kama vile suala la kuzaa lilivyo kwasasa, wengi wanaokuja kushtaki kutelekezwa wanasema hawajalipiwa mahari wala hawajaolewa, wanazaa wakiwa hawajuani vizuri matokeo yake wanakimbiwa.”

Chanzo: EATV
Mbona RPC ana kigugumizi kutaja hali ngumu ya maisha kama kichocheo pia?
 
Back
Top Bottom