Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile, amesema Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi billioni 1.2 kwa ajli ya ujenzi wa Mahakama Mpya za Mwanzo, katika Wilaya ya Sumbawanga, Nkasi na Kalambo ambazo kukamilika kwake kutawawezesha wananchi kupata huduma za kimahakama kwa urahisi.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mkuu huyo wa Wilaya ya Sumbawanga kupitia maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Sheria, ambayo kwa kanda ya Sumbawanga yamefanyika katika Manispaa ya Sumbawanga, amewataka Watumishi wa Mahakama kuwekeza zaidi katika kuwasaidia wananchi, ikiwemo kuwapatia elimu ya msaada wa kisheria.
Kwa upande wake mwakilishi wa TLS James Lubus, amesema anaipongeza serikali kwa kuwapatia gari, ambayo itawezesha kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi wakati wa utoaji huduma za kisheria vijijini.