Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Viti vitatu Bara Ndg. Shamira Mshangama amefanya ziara Mkoani Rukwa kwa lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura, zoezi litakaloanza tarehe 12-18 Januari, 2025.
Pamoja na mambo mengine, Shamira amekabidhi kamera kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Rukwa iliyopokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Comrade Albert Kipele pamoja na wajumbe wengine ngazi ya mkoa.
Mshangama amekabidhi kamera hio kwa kuirahishia UVCCM mkoa wa Rukwa kupunguza majukumu ya kukodisha mpiga picha lakini pia kuhakikisha matukio ya Umoja wa vijana yanawekewa kumbukumbu nzuri na yanawafikia vijana wengi zaidi.
Shamira amewasisitiza kuwa "Pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake, Ujenzi wa Chama ni pamoja na kuhakikisha vitendea kazi muhimu vinapatikana katika ofisi za Jumuiya".