Rukwa: Tume ya madini kuimarisha usimamizi wa sheria kuinufaisha jamii dhidi rasilimali zake, ujenzi wa shule wachangiwa mifuko 50 ya Saruji

Rukwa: Tume ya madini kuimarisha usimamizi wa sheria kuinufaisha jamii dhidi rasilimali zake, ujenzi wa shule wachangiwa mifuko 50 ya Saruji

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Tume ya madini mkoani Rukwa imeenza utekelezaji wa kanuni na utaratibu za umiliki wa leseni ya madini na namna ya uwajibikaji kwa jamii ilikuhakikisha jamii inayozungukwa na shughuli za uchimbaji wa madini inayonufaika na shughuli hizo.

Akitoa ufafanuzi wa namna sheria hiyo inavyo tekelezwa afisa mkazi wa madini mkoani rukwa Mhandi Joseph Kumburu,wakati ameeleza kuwa mmiliki wa Leseni ya madini atawajibika kuandaa mpango madhubuti wa wajibu wake kwa jamii kwa kushirikiana na Halmashauri ya kijij au mtaa uliopo katika eneo lenye shughuli za madini katika Halmashauri husika.

Wakizungumza wakazi wa kijiji cha malolwa kilichopo katika kata ya Mpwapwa iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya sumbawanga ambako kumeanzishwa shule ya sekondari kupitia nguvu zao wameeleza msukumo wao ulio wafanya kuanzisha ujenzi huo sanjari na kuishukuru serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwanamna inavyo waboreshea huduma muhimu kwa jamii.

kwa upande wake diwani wa kata ya mpwapwa Abel Msumbachika ameeleza changamoto zinazoo wakabili watoto hao pamoja na hatu walizo zifanya kama halmashauri kuhakikisha wanawaunga mkono wana kijiji hao katika ujenzi huo.

Aidha mkuu wa wilaya ya sumbawanga nyakia Ally Chirukile amewasihi wakazi wa sumbawanga kuendelea kusomesha watoto wao katika mazingira bora na kuwapa kipaombele watoto wa kike kwani ndio wenyechangamoto kubwa ya kukatisha masomo yao.

 
Back
Top Bottom