Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
WAJUMBE wa baraza la ushauri la mkoa wa Rukwa (RCC) wamepitisha rasmu ya pendekezo la kuugawa mkoa huo katika mikoa miwili na kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Mpanda kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.
Katibu Tawala wa mkoa huo, Innocent Mwenda aliwaeleza wajumbe hao kuwa kazi hiyo ya ugawaji wa mkoa wa Rukwa itazingatia vigezo muhimu vikiwemo vya ukubwa wa eneo, idadi ya watu pamoja na shughuli za kiuchumi.
Pendekezo hilo limekuja wakati tayari kuna pendekezo la kuigawa wilaya ya Mpanda na kuanzisha wilaya mpya ya Katavi na kuigawa wilaya ya Sumbawanga na kuanzishwa kwa wilaya ya Kalambo iliyopitishwa na kikao cha RCC mwaka 2006.
Source:Mwananchi.
Wanajamvi naomba msaada huu mtindo wa kuanzisha mkoa kwa kisingizio cha kusogeza huduma karibu na wananchi mbona umekaa kifisadi !.Hivi kweli Tanzania inahitaji kuongeza idadi ya mikoa ili kufikisha huduma karibu na wananchi.
Kwa upande wao, wajumbe wa mkutano huo walitahadharisha kuwa, mgawanyo wa mkoa huo uwashirikishe wananchi na uzingatie zaidi maslahi ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na siyo ya kisiasa.
Hata hivyo makao makuu ya mkoa huo mpya wa Mpanda yanatarajia kuwa mjini Mpanda huku ukiwa na ukubwa wa eneo la kilometa za mraba zaidi ya 47,000 na watu zaidi ya 500,000.
Utaratibu wa kuomba kuanzisha mikoa au wilaya huanzia kwenye wilaya inayohusika na kupitia kwenye mkoa unaohusika na kisha e mapendekezo kuwasilishwa serikalini.
Mkoa wa Rukwa haukuwepo wakati wa Uhuru, eneo hilo la mkoa wa Rukwa lote lilikuwa chini ya mkoa wa Mbeya na Tabora.
Wakati huo wilaya ya Mpanda ilikuwa chini ya mkoa wa Tabora na wilaya ya Sumbawanga na Nkasi zilikuwa chini ya mkoa wa Mbeya.
Hali hii ilisababisha wananchi wa maeneo ya Mpanda, Nkasi na Sumbawanga kuwa mbali sana na serikali yao ya mkoa na Taifa.
Hivyo ili serikali iweze kuwa karibu na wananchi, Januari 29, 1974 Mkoa wa Rukwa ulianzishwa ukiwa na Wilaya 2 Mpanda na Sumbawanga. Mnamo mwaka 1975 wilaya ya Nkasi iliundwa na kufanya Mkoa kuwa na wilaya tatu, na Halmahauri ya Mji.