Rule No 5: Usiombe ushauri kwa aliyeshindwa

Rule No 5: Usiombe ushauri kwa aliyeshindwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
RULE NO. 5; USIOMBE USHAURI KWA ALIYESHINDWA.

Ni Yule, Robert Heriel

Watu wengi wanaoniuliza kuwa Kwa nini nimepunguza kuandika Mtandaoni nimeona niwajibu Kwa pamoja hapa; Namalizia kuandika kitabu ambacho kitakuwa cha manufaa Kwa kizazi hiki mpaka kizazi kijacho.

Haya nirejee kwenye ujumbe wa leo.

Nao walioshindwa na wengi, wako mbele, wako nyuma, wako kushoto na pia wako kulia, wametuzunguka pande na pande. Hivyo usishangae ukisikia wakikuambia huwezi, huo ndio wimbo wao Kwa sababu wao ni wasioweza, akili zao ni zisizoweza, macho Yao ni yasiyoweza hivyo huona kila mtu hawezi Kama walivyo wao.

Sio ajabu kukatishwa tamaa katika jamii inayokuzunguka, hii ni sababu kuwa wengi wameshindwa, walishapoteza Pambano.

Basi, nisiseme mengi;

Hakuna Jambo geni Duniani, yote yapo, vipo tuvitumie, tusipovitumia watavitumia wengine.
Hakuna yaliyojificha, mambo yote yapo wazi, isipokuwa watu huamua kuyawekea mambo Madaraja, unaweza kuyafanya Kwa kificho au Kwa uwazi lakini mambo yote yapo wazi.

Wenye akili huyafanya mambo yaliyowazi kuwa yasirini ili wajipatie faida, tena hutengeneza hofu ili wenye hofu na watu dhaifu wasiyafikie. Basi hivyo ndivyo ilivyo katika dunia hii. Palipo na mwenye akili hakuna Siri, Ila palipo na wajinga Siri zipo zilizofichwa na wenye akili.

Usiombe Ushauri Kwa ALIYESHINDWA. Usiombe maoni Kwa mtu ambaye hajawahi kujaribu kufanya kile ukitakacho.

Usitafute maarifa Kwa walioshindwa, waliopigwa, waliokosa USHINDI, mpigwa hawezi kukushauri mambo ya USHINDI isipokuwa atakushauri alivyoshindwa na kujifanya yeye hakustahili kushindwa wakati keshashindwa.

Kwenye vita, Mshindi ndiye anaandika Historia, mathalani taifa moja linapotoka kupigana na taifa jingine, taifa litakaloshinda ndilo huandika historia.

Hata kwenye maisha ambayo ni vita, Mshindi ndiye hupaswa kunena, kuandika rekodi, kuandika historia na sio ALIYESHINDWA.

Ipo hatari kubwa ukiomba ushauri Kwa ALIYESHINDWA,
Washindwa Wana maneno ya kujifariji na kujitia Wana haki au kuonewa.

Mshindwa katika vita ya Utajiri na umasikini, akapata umasikini
Hujikuta akiwa na kauli mbaya zisizovumilika, mathalani;
"Tajiri hawana Raha" "Pesa ni Shetani" "matajiri hawatauona ufalme WA Mungu".
" Huwezi kuwa na pesa nyingi bila kuwa mchawi" na kauli nyingi kama hizo.

Mtu wa hivyo usithubutu kumuomba ushauri wala maoni yake kuhusu Utajiri, usimuhusishe katika mishe zako, atakupa Fikra na Roho ya kushindwa.

Usiombe Ushauri Kwa mtu ALIYESHINDWA kwenye ndoa yake.
Unakuta mwanamke/mwanaume ameachika/ameachwa. Huyo asikushauri Jambo lolote katika ndoa.
Siku zote washindwa ndio hujifunza Kwa walioshindwa, Ila washindi hujifunza Kwa washindi.

Mtu anapoachika/anapoachwa zipo sababu nyingi mno, lakini sababu kubwa kuliko zote sio siku ya kuachana kwao Bali ni siku ya kukutana kwao.
Kuachana ndani ya ndoa kuna yoa tafsiri kuu moja, ambayo ni kuwa Mhusika Hakuwa makini katika kuchagua katika nyakati za Mwanzoni.

Siku zote Mshindi anashinda Mwanzoni na wala sio mwishoni.
Ukiona Jambo lolote umeshindwa mwishoni basi jua kuwa ulishindwa tokea ulipoanza.

Vita inahitaji tathmini kabla hujaingia katika mapambano. Vita yoyote lazima matokeo yajulikane tokea haijaanza.
Ukiona unafanya Jambo lolote pasipo kujua matokeo yake ujue tayari katika Jambo Hilo umeshashindwa, na ikitokea umeshinda basi jua huo ushindi sio halisi na hautadumu.

Kiimani, Jambo lolote ukilifanya bila Imani ni dhambi, na tafsiri ya dhambi ni kushindwa.

Sitaki kusema maneno mengi, nisije kuwaudhi baadhi yenu mliowavivu au msiopenda mambo mengi.

Unataka ushauri wa biashara nenda Kwa mfanyabiashara aliyefanikiwa, huyo atakushauri
Unataka ushauri wa kilimo, nenda Kwa mkulima aliyefanikiwa, upate ushauri wa kilimo.

Unataka ushauri wa ndoa, nenda Kwa waliondoani waliodumu Kwa miaka nenda Rudi unaowaona wanafurahia ndoa Yao. Omba ushauri.

Sio uombe ushauri Kwa majitu yaliyoshindwa, niamini hutopata ushauri wa maana isipokuwa kushindwa ndiko unakutafuta.

Mambo makuu matatu uyapatayo kwenye ushauri wa watu;
1. Uzoefu
2. Mtazamo/Fikra
3. Roho/Imani.

Ukiomba ushauri Kwa walioshindwa jua unaenda kupewa uzoefu wa kushindwa, Fikra za kushindwa, na Roho/Imani ya kushindwa.

Walioshindwa wengi huamini kuwa kushindwa kwao ni mapenzi ya Mungu(hiyo ni imani),
Wakati walioshinda huamini kuwa jitihada zao ndizo zilizowafanya washinde.

Fikra za walioshindwa hujikita katika kulaumu wengi na kulaumu Mazingira.
Fikra za walioshinda hujikita katika kujidhatiti na kujiandaa muda wote.

Uzoefu wa walioshindwa ni kushindwa,
Uzoefu wa walioshinda ni kushinda.

Usiombe Ushauri Kwa walioshindwa, huna utakalopata zaidi ya kushindwa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
I am the Wisest Man Alive, for I know One thing and that is I know Nothing....

Mwenye busara hakatai wala hazibi masikio kwenye ushauri wa yoyote yule, bali kuufanyia kazi ushauri ule anashirikisha akili zake (za kuambiwa anachanganya na zake).

Mtu inawezekana alishindwa ndio ila kuomba ushauri kwake unaweza ukajua kwanini alishindwa na wewe usipite mule mule... (in short kama una muda sikiliza (sio kufuata) chochote unachoambiwa huwezi kujua hata mauaridi yanapitikana katikati ya miba
 
I am the Wisest Man Alive.., for I know One thing and that is I know Nothing....

Mwenye busara hakatai wala hazibi masikio kwenye ushauri wa yoyote yule...
Wengi walioshindwa hawajui Kwa nini walishindwa.

Kushindwa kunaanzia Mwanzoni sio mwishoni, mwishoni huwa ni matokeo tuu.

Kama hakujua atashindwa tafsiri yake ni kuwa hata atakachokushauri hana uhakika nacho Kwa sababu Hana uzoefu wa kushinda, Hana Fikra za ushindi, Hana Imani ya USHINDI.

Mtu akishakosa hayo matatu huwezi omba ushauri kwake.

Labda uende kufuata historia ya Kwa nini alishindwa na sio ushauri
 
I am the Wisest Man Alive.., for I know One thing and that is I know Nothing....

Mwenye busara hakatai wala hazibi masikio kwenye ushauri wa yoyote yule..., bali kuufanyia kazi ushauri ule anashirikisha akili zake (za kuambiwa anachanganya na zake)...

Mtu inawezekana alishindwa ndio ila kuomba ushauri kwake unaweza ukajua kwanini alishindwa na wewe usipite mule mule... (in short kama una muda sikiliza (sio kufuata) chochote unachoambiwa huwezi kujua hata mauaridi yanapitikana katikati ya miba

Na ndio maana unaona katika jamii zetu kuwa ukizaliwa familia za kimasikini utaendelea kuwa Masikini,
Na ukizaliwa kwenye familia tajiri utaendelea kuwa tajiri.

Maji hufuata Mkondo, na mtoto wa nyoka ni nyoka.

Ingawaje Exceptional inatokeaga lakini Kwa Asilimia ndogo Sana isiyofika 10%.

Unaweza pia itathmini familia au ukoo wenu utaweza gundua Jambo hili.

Kama ni ukoo au familia masikini basi utashangaa 90% ni masikini alafu 10%(ambao ni exceptional) huwa na Hali tofauti na yenu
 
Wengi walioshindwa hawajui Kwa nini walishindwa.

Kushindwa kunaanzia Mwanzoni sio mwishoni, mwishoni huwa ni matokeo tuu.

Kama hakujua atashindwa tafsiri yake ni kuwa hata atakachokushauri hana uhakika nacho Kwa sababu Hana uzoefu wa kushinda, Hana Fikra za ushindi, Hana Imani ya USHINDI.

Mtu akishakosa hayo matatu huwezi omba ushauri kwake.

Labda uende kufuata historia ya Kwa nini alishindwa na sio ushauri
Ukianza kuchagua wapi pa kuchukua ushauri unaji-limit, maisha sio black and white, there a lot of grey areas..., mtu inawezakuwa alishindwa sababu hana desire au motivation lakini ana good plans..., knowing and doing are two different animals....

Hivi unajua kwanini wasomi / experts wengi wanaweza wasi-excel kwenye industry fulani kuliko non-experts ? Jibu ni kwamba hawasikilizi na wanaona hakuna wa kuwaambia kitu, in the end they miss out on something...

Pili katika kufanya mambo kuna layers nyingi sana, itakuwa ni uchizi uache kuomba ushauri kwa mtu aliyeendesha hoteli akashindwa sababu ya bad money management ukaacha kumsikiliza kumbe alikuwa amebobea kwenye upishi na ni the best Cook in Town.... Kumbuka haulazimishwi kufuata ushauri ila haupotezi kitu kuzikiliza unachoambiwa alafu unachuja...

Kumbuka pia mafanikio yanahitaji kutokukata tamaa, desire na dedication hata kama sio mtaalamu, ila unaweza ukawa mtaalamu hauna hizo skills nilizoweka hapo mwanzo ila mtu mwenye hizo skills akakutumia ili yeye ndio ashinde ingawa bila wewe na yeye anaanguka...
 
Na ndio maana unaona katika jamii zetu kuwa ukizaliwa familia za kimasikini utaendelea kuwa Masikini,
Na ukizaliwa kwenye familia tajiri utaendelea kuwa tajiri.

Maji hufuata Mkondo, na mtoto wa nyoka ni nyoka.
Not necessarily hio inatokea sana kutona na lack of opportunities especially ulimwengu wa sasa wa its not what you know but whom you know...

Kuna watu masikini wengi self made wanakuwa matajiri wa kutupwa baadae, hata hao walioanzisha big empires historically walitokea familia za kimasikini WHY you may ask....., Sababu ya ile desire ya kuondokana na poverty cycle wanajituma na kutokukata tamaa, wana Desire ya kufanya kitu against the odds (You can Never Beat Such People)
Ingawaje Exceptional inatokeaga lakini Kwa Asilimia ndogo Sana isiyofika 10%.

Unaweza pia itathmini familia au ukoo wenu utaweza gundua Jambo hili.

Kama ni ukoo au familia masikini basi utashangaa 90% ni masikini alafu 10%(ambao ni exceptional) huwa na Hali tofauti na yenu
Ndio maana nikasema in the Capitalist World kama utakuwa handed some Capital una advantage tayari kuliko anayeanza square one (life is not black or white) kuna mengi sana hapo katikati, na ukiondoa cultures ambazo watoto wanafundishwa business za wazazi wao toka utotoni especially indians; second generations nyingi huwa zinafuja mali za wazazi wao..., tofauti na mtu ambaye ni self made from scratch, such a specie would rather die than loose his business....
 
Ukianza kuchagua wapi pa kuchukua ushauri unaji-limit, maisha sio black and white, there a lot of grey areas..., mtu inawezakuwa alishindwa sababu hana desire au motivation lakini ana good plans..., knowing and doing are two different animals....

Hivi unajua kwanini wasomi / experts wengi wanaweza wasi-excel kwenye industry fulani kuliko non-experts ? Jibu ni kwamba hawasikilizi na wanaona hakuna wa kuwaambia kitu, in the end they miss out on something...

Pili katika kufanya mambo kuna layers nyingi sana, itakuwa ni uchizi uache kuomba ushauri kwa mtu aliyeendesha hoteli akashindwa sababu ya bad money management ukaacha kumsikiliza kumbe alikuwa amebobea kwenye upishi na ni the best Cook in Town.... Kumbuka haulazimishwi kufuata ushauri ila haupotezi kitu kuzikiliza unachoambiwa alafu unachuja...

Kumbuka pia mafanikio yanahitaji kutokukata tamaa, desire na dedication hata kama sio mtaalamu, ila unaweza ukawa mtaalamu hauna hizo skills nilizoweka hapo mwanzo ila mtu mwenye hizo skills akakutumia ili yeye ndio ashinde ingawa bila wewe na yeye anaanguka...

Mimi sitaki kubishana na wewe.

Kwa aliyeshindwa labda ukachukue historia tuu lakini sio ushauri.

Hivyo ndivyo ilivyo.

Kukataa ni kujifariji tuu.

Ndio maana mataifa yote Duniani au watu wote wenye akili na waliofanikiwa huenda kujifunza kwenye mataifa au watu waliofanikiwa/walioshinda.

Iko hivyo
 
You are wrong brother

Failure is part and parcel of success

Those who avoid failure also avoid success

Jifunze kwa wote uliza kwa wote

Tunategemeana

Mbaya zaidi hata mafanikio yenyewe siyo hayo watu mmekuwa mkihubiri

Kwenu wengi wenu mafanikio ni kuwa na pesa nyingi kitu ambacho si kweli na ni upumbavu mtupu
 
Mimi sitaki kubishana na wewe.

Kwa aliyeshindwa labda ukachukue historia tuu lakini sio ushauri.

Hivyo ndivyo ilivyo.

Kukataa ni kujifariji tuu.

Ndio maana mataifa yote Duniani au watu wote wenye akili na waliofanikiwa huenda kujifunza kwenye mataifa au watu waliofanikiwa/walioshinda.

Iko hivyo

Ngoja nikupe Case Study kidogo tu..., Huko Marekani Watumwa walikuwa wakionekana kama watu wasio na akili wala hawajui hili wala lile na hawawezi kufanikiwa sababu ya IQ yao ndogo

ALAS

Slaves’ inventions exploited by owners​

During the 17th and 18th centuries, America was experiencing rapid economic growth. Black inventors were major contributors during this era – even though most did not obtain any of the benefits associated with their inventions since they could not receive patent protection.

Slave owners often took credit for their slaves’ inventions. In one well-documented case, a black inventor named Ned invented an effective, innovative cotton scraper. His slave master, Oscar Stewart, attempted to patent the invention. Because Stewart was not the actual inventor, and because the actual inventor was born into slavery, the application was rejected.

Again life is not black or white; Kuna sababu nyingi za kutokufanikiwa leo Facebook Ipo Juu, ingawa MySpace ilitangulia na ilikuwa na idea hio...., leo Google inasikika kila kona ila kabla tulikuwa na Yahoo...., kwahio utaniambia nikikutana na previous Yahoo CEO niachane nae sababu juzi nilikutana na CEO wa Google ?
 
Mpaka uone mtu ameshinda ujuwe alishakutana na kushindwa mara nyingi sana ila hakukata tamaa
 
Na wakati mwingine kushindwa ndiyo ushindi wenyewe

Kuna mengi kwenye kushindwa kuliko unavyoona matokeo ya mwisho

Usikariri hivi > ^NEVER GIVE UP^

Kariri hivi > ^DO NOT GIVE UP^

NEVER SAY NEVER
 
Labda ungesema tusiombe ushauri kwa waliokata tamaa na siyo walioshindwa

Hakuna mwanadamu ambaye hajawahi kushindwa kitu fulani maisha yake yote
 
Labda ungesema tusiombe ushauri kwa waliokata tamaa na siyo walioshindwa

Hakuna mwanadamu ambaye hajawahi kushindwa kitu fulani maisha yake yote
Pia ushauri wa nifanye au nisifanye ni wewe mwenyewe ndio uamue kutokana na matakwa yako...., Ila kama kuna A, B, C , D na E huenda anayekupa ushauri alishindwa zote ila E aliweza na hata kama amekata tamaa sio kwamba atakuwa amesahau kuhusu hio E.

Labda jamaa angesema usipende kukaa na watu ambao ni Naysayers au Negative watakukatisha tamaa, ila pia ukiwaelewa unaweza kuwachimba ukapata madini (Kutokukata Tamaa ndio Siri kubwa ya Mafanikio)
 
Kuna kitu tulianza fanya, watu wote tuliowauliza walisema haiwezekani, tukajipa moyo na kusema kama ni hela wacha ipotee.... Leo hii wale wale waliotutamkia hatutaweza wanatuomba kazi na chakula kupitia kile kile walichosema hatuwezi.

Usikwamishwe na walioshindwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu kama ni ushauri unaweza kuwa wa hovyo pia kwa sababu waswahili wanasema mtu hujifunza kutokana na makosa..kwa hiyp mtu akiwa mzuri inawezekana hapo nyuma ni matokeo ya kujifunza kutokana na makosa.Kama mtu ameshindwa ana jambo la kujifunza la kukuambia

Watu hawaombi ushauri Kwa walioshindwa labda watu wa hovyo.

Labda aliyeshindwa ndio ajipendekeze kuja kukushauri lakini sio wewe uende kuomba ushauri wa Jambo ambalo mtu kalishindwa, utakuwa kioja nakuambia
 
Back
Top Bottom