Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii point imetulia sana.Mimi sitaki kubishana na wewe.
Kwa aliyeshindwa labda ukachukue historia tuu lakini sio ushauri.
Hivyo ndivyo ilivyo.
Kukataa ni kujifariji tuu.
Ndio maana mataifa yote Duniani au watu wote wenye akili na waliofanikiwa huenda kujifunza kwenye mataifa au watu waliofanikiwa/walioshinda.
Iko hivyo
Kwa hiyo hata uzoefu wake uliopelekea kwenye kushindwa usiusikilize, ili nawe uishie huko huko. Penye kushindwa, kuna kujifunza pia.RULE NO. 5; USIOMBE USHAURI KWA ALIYESHINDWA.
Ni Yule, Robert Heriel
Watu wengi wanaoniuliza kuwa Kwa nini nimepunguza kuandika Mtandaoni nimeona niwajibu Kwa pamoja hapa; Namalizia kuandika kitabu ambacho kitakuwa cha manufaa Kwa kizazi hiki mpaka kizazi kijacho.
Haya nirejee kwenye ujumbe wa leo.
Nao walioshindwa na wengi, wako mbele, wako nyuma, wako kushoto na pia wako kulia, wametuzunguka pande na pande. Hivyo usishangae ukisikia wakikuambia huwezi, huo ndio wimbo wao Kwa sababu wao ni wasioweza, akili zao ni zisizoweza, macho Yao ni yasiyoweza hivyo huona kila mtu hawezi Kama walivyo wao.
Sio ajabu kukatishwa tamaa katika jamii inayokuzunguka, hii ni sababu kuwa wengi wameshindwa, walishapoteza Pambano.
Basi, nisiseme mengi;
Hakuna Jambo geni Duniani, yote yapo, vipo tuvitumie, tusipovitumia watavitumia wengine.
Hakuna yaliyojificha, mambo yote yapo wazi, isipokuwa watu huamua kuyawekea mambo Madaraja, unaweza kuyafanya Kwa kificho au Kwa uwazi lakini mambo yote yapo wazi.
Wenye akili huyafanya mambo yaliyowazi kuwa yasirini ili wajipatie faida, tena hutengeneza hofu ili wenye hofu na watu dhaifu wasiyafikie. Basi hivyo ndivyo ilivyo katika dunia hii. Palipo na mwenye akili hakuna Siri, Ila palipo na wajinga Siri zipo zilizofichwa na wenye akili.
Usiombe Ushauri Kwa ALIYESHINDWA. Usiombe maoni Kwa mtu ambaye hajawahi kujaribu kufanya kile ukitakacho.
Usitafute maarifa Kwa walioshindwa, waliopigwa, waliokosa USHINDI, mpigwa hawezi kukushauri mambo ya USHINDI isipokuwa atakushauri alivyoshindwa na kujifanya yeye hakustahili kushindwa wakati keshashindwa.
Kwenye vita, Mshindi ndiye anaandika Historia, mathalani taifa moja linapotoka kupigana na taifa jingine, taifa litakaloshinda ndilo huandika historia.
Hata kwenye maisha ambayo ni vita, Mshindi ndiye hupaswa kunena, kuandika rekodi, kuandika historia na sio ALIYESHINDWA.
Ipo hatari kubwa ukiomba ushauri Kwa ALIYESHINDWA,
Washindwa Wana maneno ya kujifariji na kujitia Wana haki au kuonewa.
Mshindwa katika vita ya Utajiri na umasikini, akapata umasikini
Hujikuta akiwa na kauli mbaya zisizovumilika, mathalani;
"Tajiri hawana Raha" "Pesa ni Shetani" "matajiri hawatauona ufalme WA Mungu".
" Huwezi kuwa na pesa nyingi bila kuwa mchawi" na kauli nyingi kama hizo.
Mtu wa hivyo usithubutu kumuomba ushauri wala maoni yake kuhusu Utajiri, usimuhusishe katika mishe zako, atakupa Fikra na Roho ya kushindwa.
Usiombe Ushauri Kwa mtu ALIYESHINDWA kwenye ndoa yake.
Unakuta mwanamke/mwanaume ameachika/ameachwa. Huyo asikushauri Jambo lolote katika ndoa.
Siku zote washindwa ndio hujifunza Kwa walioshindwa, Ila washindi hujifunza Kwa washindi.
Mtu anapoachika/anapoachwa zipo sababu nyingi mno, lakini sababu kubwa kuliko zote sio siku ya kuachana kwao Bali ni siku ya kukutana kwao.
Kuachana ndani ya ndoa kuna yoa tafsiri kuu moja, ambayo ni kuwa Mhusika Hakuwa makini katika kuchagua katika nyakati za Mwanzoni.
Siku zote Mshindi anashinda Mwanzoni na wala sio mwishoni.
Ukiona Jambo lolote umeshindwa mwishoni basi jua kuwa ulishindwa tokea ulipoanza.
Vita inahitaji tathmini kabla hujaingia katika mapambano. Vita yoyote lazima matokeo yajulikane tokea haijaanza.
Ukiona unafanya Jambo lolote pasipo kujua matokeo yake ujue tayari katika Jambo Hilo umeshashindwa, na ikitokea umeshinda basi jua huo ushindi sio halisi na hautadumu.
Kiimani, Jambo lolote ukilifanya bila Imani ni dhambi, na tafsiri ya dhambi ni kushindwa.
Sitaki kusema maneno mengi, nisije kuwaudhi baadhi yenu mliowavivu au msiopenda mambo mengi.
Unataka ushauri wa biashara nenda Kwa mfanyabiashara aliyefanikiwa, huyo atakushauri
Unataka ushauri wa kilimo, nenda Kwa mkulima aliyefanikiwa, upate ushauri wa kilimo.
Unataka ushauri wa ndoa, nenda Kwa waliondoani waliodumu Kwa miaka nenda Rudi unaowaona wanafurahia ndoa Yao. Omba ushauri.
Sio uombe ushauri Kwa majitu yaliyoshindwa, niamini hutopata ushauri wa maana isipokuwa kushindwa ndiko unakutafuta.
Mambo makuu matatu uyapatayo kwenye ushauri wa watu;
1. Uzoefu
2. Mtazamo/Fikra
3. Roho/Imani.
Ukiomba ushauri Kwa walioshindwa jua unaenda kupewa uzoefu wa kushindwa, Fikra za kushindwa, na Roho/Imani ya kushindwa.
Walioshindwa wengi huamini kuwa kushindwa kwao ni mapenzi ya Mungu(hiyo ni imani),
Wakati walioshinda huamini kuwa jitihada zao ndizo zilizowafanya washinde.
Fikra za walioshindwa hujikita katika kulaumu wengi na kulaumu Mazingira.
Fikra za walioshinda hujikita katika kujidhatiti na kujiandaa muda wote.
Uzoefu wa walioshindwa ni kushindwa,
Uzoefu wa walioshinda ni kushinda.
Usiombe Ushauri Kwa walioshindwa, huna utakalopata zaidi ya kushindwa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
Kwa hiyo hata uzoefu wake uliopelekea kwenye kushindwa usiusikilize, ili nawe uishie huko huko. Penye kushindwa, kuna kujifunza pia.
Ni kweli, mfano mdogo nimeomba ushauri kwa jamaa kadhaa nataka kufanya biashara fulani eneo ambalo wapo wauzaji wengi wa bidhaa hiyo cha ajabu wananikatisha tamaa eti hapo kila mtu anawateja wake tayari mimi nitawatoa wapi
Leo umeandika utumbo wa mende. Mimi aliyeshindwa ushauri wake ndo ulinifanya natanua kwapa mjini hapa.
Sawa mkuu. Hii uliboronga kaka, msema kweri ni mpenzi wa Mungu.Sawa.
Sibishanagi