Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
RULE NO 8; MAISHA NA DIPLOMASIA.
Anaandika, Robert Heriel
Mwanafalsafa.
Lengo; andiko hili nimeliandika Kwa ajili ya kujenga kizazi Bora, kuanzia ngazi ya familia, ukoo, na taifa Bora. Andiko hili laweza kusomwa na yeyote na kutumiwa na yeyote.
Yeyote atakayesoma au kusikiliza au kusimuliwa apate ujumbe na maana Kama ifuatavyo;
i. Maisha ni kuishi
ii. Kuishi ni kuhusiana na watu na mazingira.
iii. Ili mtu aishi akiwa na mahusiano mazuri na watu na mazingira itampasa awe na Diplomasia.
iv. Mahusiano mazuri ndio huleta mafanikio katika Jambo lolote, kifamilia, kiukoo, kitaifa na kiulimwengu.
V. Hata hivyo Vita inaweza kuwa sehemu ya Diplomasia endapo kutakuwa hakuna namna nyingine.
Niite Taikon wa Fasihi, Mwanadiplomasia.
Ushindi ulioratibiwa kuvuruga mahusiano ya watu wawili ndio ushindi mkubwa kuliko ushindi katika uwanja wa vita. Adui mahiri mwenye werevu wa Hali ya juu apambanapo hatua za Kwanza atakachokifanya ni kuzorotesha mahusiano ya mahasimu wake. Hakika endapo adui yake akifanikiwa kuingia katika kambi yako na kuvuruga mahusiano yako na watu wako atakuwa amekushinda Kwa hakika.
DIPLOMASIA NI NINI?
Diplomasia inafafanuliwa kinadharia kama sanaa ya mawasiliano kati ya pande tofauti pande hizo inaweza kuwa wawakilishi wa nchi moja na Nchi nyingine, au utawala mmoja na utawala mwingine, au mtu mmoja na mtu mwingine. Kwa lengo la kuleta mahusiano yenye tija na manufaa baina ya pande hizo mbili.
Huwezi tenganisha Diplomasia na Maisha.
Aina za Diplomasia
i. Diplomasia ya Kifamilia
ii. Diplomasia ya Kiuchumi
iii. Diplomasia ya Kisiasa
iv. Diplomasia ya Kiroho
i. DIPLOMASIA YA KIFAMILIA
Mwanaume anapooa anaenda kuunda serikali ya familia yake. Kama Mtawala wa serikali hiyo lazima awe na mambo Yafuatayo;
Rais/Mfalme/ Kiongozi/ Mtawala ni Baba, Malkia, Waziri Mkuu ni Mama.
Watoto ni Raia WA kawaida wanaotakiwa kutii mamlaka na amri zote zitakazokuwa zimeundwa katika utawala huo. Mama ndiye Mkuu wa shughuli zote za Serikali ya familia. Hivyo Oda zote za Baba anatakiwa kuhakikisha zinatekelezwa. Ni uhaini ambao kamwe hautakiwa kuvumiliwa Kwa Mama kujitungia mambo yake yatakayoenda kinyume na maelekezo ya BABA. Kiutawala Mama akifanya hivyo anaweza hata kutumbuliwa.
Maadui Siku zote katika maisha huangalia Sera na sheria zako, mipango na malengo yako, kisha huingilia humo kuvuruga mahusiano ya wahusika katika Familia yako.
Kama Mtawala itakupasa utie mkazo Kati mambo Yafuatayo unapoanzisha Familia/utawala wako;
i. Upendo bila upendeleo, umoja na ushirikiano baina ya watu wote katika serikali yako. Nguzo kuu ya serikali ya familia ni Upendo.
ii. Haki na wajibu
Kila mtu umpe haki yake, na kila mtu ndani ya serikali yako awajibike Kwa majukumu yanayomhusu. Hata hivyo kusaidiana katika wajibu ni muhimu ili kuleta umoja na kuepuka ubinafsi na Majivuno au kiburi.
iii. Usimamizi na Protocol izingatiwe
Kama Baba lazima uhakikishe kuwa maono yako Mkeo ayatie akilini, yaani aone kama unavyoona wewe.
Usimamizi ya kila sheria, Sera, mipango, mikakati ni muhimu sana.
Kama Baba, itakupasa usiwe legelege katika kumsimamia Mkeo na kuhakikisha ana-adapt tabia yako katika miaka mitatu ya Mwanzoni.
iv. Uhuru na Mawasiliano
Sheria na Sera za familia yako izingatie haki ya Uhuru Kwa kila mtu katika familia yako Kwa kuzingatia Umri, jinsia na maumbile ya wahusika ndani ya serikali yako.
Yapo mambo ni huru Kwa watu wote lakini yapo mengine sio huru Kwa watu wote.
Mfano, Uhuru wa kujieleza ni Haki ya kila mtu ndani ya familia yako.
Lakini Uhuru wa kujiamulia baadhi ya vitu sio haki ya kila mtu katika familia yako.
Baba ndiye muamuzi WA mwisho, kisha afuate Mama(kama Baba hayupo Mama ndiye muamuzi WA mwisho).
Baba kama Mtawala utatoa Uhuru Kwa wanafamilia, Uhuru wa kuku-challenge lakini challenges hizo hazitahusisha Mamlaka na utawala wako au maamuzi yako hasa Yale yenye tija na kulinda Amani ya familia.
Uhuru wa mavazi ni muhimu lakini usivuke mipaka, hata hivyo kama Baba sio kila wakati utumie ubabe katika kufundisha watoto wako. Kama mtoto atataka kuvaa mavazi yanayopingana na Sheria na Sera za familia yako,
Utamchukua mtoto huyo na kumruhusu Avae hayo mavazi kisha mtoke wote, kisha Yale yatakayojitokeza huko mtaani utamfafanulia.
Mfano, Binti yangu unaona watu wanavyokutazama, unajua ni Kwa nini? Atakujibu, kisha utamuambia kuwa mavazi hayo sio mazuri kwani yanadhuru watu wengine kwa kuwasababishia kuwaka tamaa. Hivyo ni kosa kisheria za pale nyumbani na kosa Kwa Mungu. Na Kwa vile ni kosa basi madhara yake huweza kuwa kubakwa, au kupata mimba, na hata magonjwa hatari ya ngono.
Utampa na mifano ya watu waliowakuta, kisha siku nyingi utampitisha binti yako kwenye maofisi makubwa aone wanawake wanaojielewa, wenye hadhi, na waamuzi wa nchi jinsi wanavyo Act, Utamueleza matokeo mazuri ya kujiheshimu ni kuwa kama hao Wanawake anaowaona.
Kisha mwambie ndio maana umeunda zile sheria na haupo tayari kumuona panya yeyote akizivunja.
Baada ya hapo eleza msimamo wako na ukali kuwa hutaki mchezo katika serikali yako. Muambie kuwa hautomvumilia yeyote katika serikali yako atakayeenda kinyume na sheria na Sera za familia yako.
Vinginevyo wasubiri wakue watakapojitegemea ndio wakafanye wanavyojisikia.
v. Uaminifu na kujizuia
Lazima ujenge uaminifu katika familia yako. Uaminifu ni sehemu muhimu ya Haki. Kile unachokisema ufanye, kujizuia na kuendeshwa kimwili, kihisia na kiakili kutakakosababisha usaliti. Uaminifu sio katika kutenda mazuri tuu Bali hata kutenda mambo yanayoumiza. Mfano, kama umeahidi kuwa atakayevunja sheria Fulani utamchapa bakora za kutosha basi watoto wajue kuwa Baba ni muaminifu atatimiza Kwa hakika kile alichokisema. Mtoto akikosea na Kama uliahidi Kwa mdomo wako basi lazima umtandike tuu.
Makosa ya kusamehewa mara nyingi ni Yale ambayo hukuyatolea maelezo wala hukusema kuwa utatoa adhabu. Ila kosa lolote ambalo ulisema kuwa atakayekiuka atakiona chamoto basi hakikisha kuwa maneno yako ni dhahiri.
Kufanya hivyo ni kujenga uaminifu Kwa wanaokuzunguka, yaani Mkeo na watoto wanakuamini zaidi. Kuliko useme alafu usamehe, huo Msamaha wataufurahia lakini utabomoa nguzo muhimu ya Familia ambayo ni uaminifu.
Katika utawala na mamlaka yoyote kubwa na yenye nguvu, uaminifu ni moja ya nguzo muhimu.
Katika Familia, maadui mara nyingi hupitia katika lango la wanawake zaidi kuliko Sisi wanaume. Ingawaje wapo wanaume ambao pia huweza kutumika kuiangusha familia. Hasa wanaume wenye hulka ya kike.
Adui anapoanzisha vita na wewe kuangusha utawala wako anatarajiwa apige Maeneo Yafuatayo;
i. Amtumie Mkeo ikiwa haukumuandaa vizuri kuwa Mtawala atakayekurithi
Mkeo ni mrithi namba moja wako. Hivyo lazima katika hatua za awali unatakiwa um-shape vile anavyotakiwa kuwa kama wewe. Hatakuwa wewe Kwa 100% lakini angalau 80% awe Kama awe. Ndoa ni umoja, ufanano, ambao huundwa na mume na mke.
Na ili hayo yafanyike upendo ndio msingi Mkuu. Huwezi kumuongoza Mkeo kama hakupendi(ingawaje kiasili hawako hivyo Ila wanaakisi upendo kutoka kwetu) upendo wa mwanamke sio halisi ni Kama Mwanga wa mbalamwezi unavyosharabu nuru kutoka kwenye Jua. Hivyo ni kusema Mwanaume ndiye jua(chanzo kikuu cha upendo) alafu mwanamke ni mbalamwezi ambacho huchukua upendo kutoka Kwa mumewe.
Taikon Hili nilishawahi kulizungumzia, Upendo WA Mkeo huweza Kuisha Kwa namna unavyomfanyia, hili ni somo jingine.
Mkeo atatumiwa zaidi na Wale ambao aidha unawaamini Sana au wale ambao unawadharau Sana, hao ndio watakuangusha.
ii. Wakosoaji wa sheria na Sera zako
Ni kawaida Watu wenye mafanikio kuonekana Kama wanamisimamo na sheria kali katika familia zao.
Maadui ni kawaida kusema kuwa familia yako inateseka, sijui haina Uhuru, au unamuonea Mkeo ili kuchochea uasi Kwa mkeo au Kwa watoto wako. Familia zote kubwa Duniani zinasheria Kali, miiko, maadili na mifumo Yao.
Huwezi kufika tuu katika familia hizo bila mchakato Fulani au taarifa. Hata kwenda tuu Marekani au nchi zilizoendelea kuna vizuizi vingi mno tofauti na Nchi za ulimwengu WA tatu. Wazazi au wakwe wanaweza kutaka kuingiza Sheria zao katika serikali yako usikubali.
Iii. Utandawazi na Teknolojia
Diplomasia katika maisha ni Jambo la msingi Sana wenye kuleta tija katika maisha ya familia au koo zenye nguvu. Zingatia Diplomasia inahusu Sanaa ya Mawasiliano baina ya makundi mawili.
Unaposema mawasiliano unazungumzia taarifa zinazosafirishwa kupitia chombo maalumu kiitwacho Lugha.
Hizo taarifa huwezi kuzipata pasipo kuwa na vyanzo vya taarifa, kuzikusanya na kuzichakata kisha ndipo mawasiliano yafanyike. Katika ngazi ya familia, ni muhimu kujua na kupata taarifa za watu wa familia yako Kwa kadiri itakavyowezekana. Wanasema informations is power.
Kwa leo tutaishia hapa.
Jipatie kitabu changu kiitwacho;
FUNGUO SABA, Milango kumi na mbili.
Kwa Tsh 20,000/= Hardcopy.
Mawasiliano: 0693322300
Mfumo uko hivi,
Utatoa Oda yako, kisha kitabu ndio kitachapishwa.
Kila Oda 50 vitabu vitachapishwa.
Ni Yule Mtibeli
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

- kusudio na Agenda, Kwa nini anaunda hiyo familia, Kwa nini kaoa.
- maono, anataka serikali atakayoiongoza ifike wapi, iweje, Kwa kiwango kipi. Atakaowaongoza na watakaomsaidia kuongoza(mkewe) anataka waweje.
- mipango na malengo kisha mikakati ya kutimiza hayo.
- Sheria na Sera zitakazolinda na kufanikisha mahusiano ya watu wake, mipango,mipango na mikakati, Mali na nguvu kazi za serikali, mapato na matumizi, maadili na mitindo yote ya maisha ya watu wake ndani ya hiyo familia anayoenda kuianzisha.