Rungu la TCRA lawashukia Wasafi Tv, Clouds FM, Carry Mastory, Radio one na RFA kwa kurusha maudhui yaliyo kinyume na Sheria

Rungu la TCRA lawashukia Wasafi Tv, Clouds FM, Carry Mastory, Radio one na RFA kwa kurusha maudhui yaliyo kinyume na Sheria

TCRA imetoa onyo kali na kuziweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu Radio Free Africa na Radio One Stereo kwa kukiuka kanuni za utangazaji viliporusha kipindi cha Amka na BBC ambapo Tundu Lissu aliituhumu serikali kuwazuia viongozi wa Chadema kumuaga Hayati Rais Benjamin Mkapa.

Wasafi Media Online TV imetuhumiwa kurusha maudhui yanayochochea vitendo vya ngono kupitia kipindi cha Women Matters. Kosa la ngono kamati imetoa onyo na faini ya milioni 5 itakayolipwa TCRA.

Kamati ya Maudhui ya TCRA imekifungia kipindi cha Jahazi Cha Clouds FM kwa kosa la kurusha maudhui yenye kuchochea kujichua sehemu za siri na ngono. Aidha, Clouds FM imetakiwa kutokujaza muda huo kwa kipindi kingine chenye maudhui sawa na Jahazi

Hivi kuna watu bado wanaangalia na kusikiliza tv na radio za kibongo!?
 
Kazi imeanza. Sasa hivi ni vipindi vya kusifu tu na kuabudu ndivyo vinahitajika. We have a long way to go.
Ulikiona hicho kipindi cha WASAFI Online Dr. Mwaka alizungumza? Ulisikiliza kipindi cha jahazi walipokua wakiwashawishi watu kupige punyeto?

Au ndio zile zama za wapinga kila kitu?
 
Sheria ziko pale kufuatwa na sio vingnevyoo..ndomaana ukitaka kujiua hakikisha unakufa ukipona gvt wanakwambia ww ni mali ya gvt na sio vingnevo...jera unaenda kukaa numa ya nondo mkuu
I thought "kukaa nyuma ya nondo" ndio "kuwekwa "jera" ", kumbe kuna "kukaa "jera" nyuma ya nondo" pia! Ndio najua leo hii.
 
Ulikiona hicho kipindi cha WASAFI Online Dr. Mwaka alizungumza? Ulisikiliza kipindi cha jahazi walipokua wakiwashawishi watu kupige punyeto?

Au ndio zile zama za wapinga kila kitu?
Mwambieni Nyerere uchwara aache mizinguo ya kuminya uhuru wa habari.
 
Haya Clouds endeleeni kupiga lile jingle lenu ambalo Nyerere uchwara anakuwa anaongea ongea . Huwa mnapenda kulipiga asubuhi mara nyingi nimeshalisikia nikiwa kwenye daladala. Huwa najiuliza kwa nini mnalipiga sipati jibu. Haya endeleeni nalo.
 
Wakuu,

Nimeona kupitia nipashetz Instagram account kuwa TCRA wameipiga kufuli hicho kipindi kwa kukiuka maudhui ya utangazaji. Pia hawatakiwi kuwa na kipindi Chenye maudhui hayo kuanzia leo.

Poleni sana kwa Clouds fm kwa pigo hili ingawa hatujui chanzo halisi ni nini.

Ushauri nyakati hizi Jahazi haipo turudisheni burudani za zamani, maneno kidogo muziki mzuri unatawala dizaini ya mid morning jams ile ya dj boogie Master.

Pendekezo: Itapendeza mkimpa space John Dilinga na mtu wa sports kidogo lakini mziki mzuri ukitawala na maneno kidogo.

Kuwa na kipindi kisicho na maudhui ya Jahazi kwa jioni ni mtihani. Kila lakheri kwenu.
Eleza adhabu iliyotolewa n sawa..??
 
Back
Top Bottom