PreGE2025 Rungwe asisitiza Sera ya Ubwabwa akikaribisha wanachama wapya Chaumma

PreGE2025 Rungwe asisitiza Sera ya Ubwabwa akikaribisha wanachama wapya Chaumma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
b82f3d14-4f4d-4b39-97e8-ec74adbf5e05.jpg

DAR. Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amesisitiza Sera ya chama hicho ya Lishe maarufu Ubwabwa akisema Taifa lisilo na lishe haliwezi kujiletea maendeleo.

Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua mkutano maalum ya kukaribisha wanachama wapya wakiwamo wa kundi la G55 waliojitoa Chadema leoMei 21, 2025 katika ukumbi wa Ubungo Plaza,Jijini Dar es salaam.

Soma pia: Chaumma yakaribisha G55

“Taifa ambalo halina lishe hakika halitaweza kuendelea na ndio maana sisi Chaumma tunaamini kuwa ili kujenga taifa madhubuti na lenye watu imara ni lazima tuhakikishe kuwa wanapata lishe madhubuti tangu wakiwa watoto, huwezi kujenga taifa imara kama watu wake wanakuwa na shida ya utapiamlo, ndio maana halisi ya kauli mbiu yetu ya UBWABWA kwa wote. Karibuni tukajenge taifa lililoshiba na lenye afya njema,” amesema huku akishangiliwa.

Ameongeza kuwa, watu walioshiba wataweza kupiga kura kwa utashi wao kwani hawatasubiri kupewa rushwa ya chakula ili wauze utu wao.

Amesema chama hicho kimepitia mapito mengi tangu kiliposajiliwa mwaka 2012, huku akirejea lengo la kupatikana kwa uhuru wa nchi, ambapo waasisi wa taifa letu walikuwa na walikuwa na ndoto kuhusu jamii ambayo waliitaka kuijenga.

“Walikusudia kujenga jamii ambayo pamoja na tofauti lakini jamii yenye usawa katika mahitaji ya msingi na ya lazima. Walikusudia kujenga jamii ambayo watu watashindana katika ziada lakini lakini wote wanakuwa sawa katika kupata mahitaji ya msingi, heshima na utu wao.

“Chaumma tunaamini kuwa taifa letu linatakiwa kuwa kwenye misingi ya soko la kijamii lenye nidhamu kwani ndio msingi wa majibu ya changamoto zinazolikabili taifa letu kwa sasa na siku zijazo.

“Tunaamini kuwa soko la kijamii ni daraja la kurejesha taifa letu katika kujenga jamii ambayo inaheshimu sheria,kujenga ustawi wa kiuchumi kutokana ma utajiri wa rasilimali ambao Mwenyezi Mungu ametujaalia,” amesema.
eab5b3ca-c584-4eb1-9461-ed3a1c0ec805.jpg

Akizungumza baada ya Rungwe kumaliza, Makamu Mwenyekiti wa Chaumma (Bara), Devotha Minja amesema Minja amesema lengo la chama hicho ni kushika madaraka na ndio maana ya chama cha siasa tofauti na kikundi cha wanaharakati.

“Twendeni tukashiriki uchaguzi, tupiganie mabadiliko ambayo tutnaamini tutayapata katika uwanja huo na kamwe hatuwezi kuchukua ushindi tukiwa nje ya ulindi na hatuwezi kuchukua kombe kama tumeondoa timu uwanjani, twendeni katika uwanja kwa ajili ya mapambano,” amesema.
 

Attachments

  • b82f3d14-4f4d-4b39-97e8-ec74adbf5e05.jpg
    b82f3d14-4f4d-4b39-97e8-ec74adbf5e05.jpg
    297 KB · Views: 45
Back
Top Bottom