LGE2024 Rungwe: Hivi ndivyo Wagombea wa CHADEMA walivyochukua fomu za kugombea Uenyekiti wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ukiondoa Rungwe wapi kwingine. Ama ndo wameanza. Siku hizi cdm ya baridiiiii in jk voice
 
Nafurahia sana na kupenda juhudi zako za kutuletea taarifa, mkuu, Erythro. Natamani sana nchi nzima ingekuwa na mwonekano wa aina hii; hapo hata CCM ingewastua, kwa sababu wange anza kupiga mahesabu upya.

Pesa ya kuwazungukia wote hawa kuwanunua ingepatikana wapi; hata wajomba wangesita!

Nchi nzima iwe na mwamko kama huo, policcm wataanzia wapi kuwatisha watu.

Sasa, kwa bahati mbaya, mwonekano huu ni sehemu za kuokoteza, hapa moja na pale nyingine. Na kama ujuwavyo, na kutokana na uzoefu wa polisi kuzima maandamano, sasa wataanza kujipanga kuzima hata haya.

Kwa upande wa pili: Kwa nini hali hii isiwe kama ni kupasha joto misuri, ikiwa kama somo maalum la 2025; kwa maana muda wa kuyafanya haya kwa mpangilio na kwa matokeo chanya bado upo wa kutosha.

Natumaini umenielewa, vinginevyo nifahamishe nieleze kwa ufasaha zaidi ninayo yawaza.
 
Mungu baba Ibariki CHADEMA
 
Ni kosa kubwa kuwaachia hawa nguruwe wa kijani shamba la mihogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…