Rungwe: Mchungaji aomba msamaha kwa kukataza waumini wake kutumia ARV'S na kusababisha wengine kufariki

Rungwe: Mchungaji aomba msamaha kwa kukataza waumini wake kutumia ARV'S na kusababisha wengine kufariki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya, Emmanuel Mlundilwa amesema kukosa uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARV’s), kulisababisha kuwakataza waumini wake kutumia dawa hizo na wakazidi kudhoofu na kupoteza maisha.

Amewaomba radhi ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao kutokana na kutofuata ushauri wa wataalamu wa afya kutokana na msimamo wake wa kuamini wataponywa kwa maombi kutoka kwake.

Mchungaji Mlundilwa alisema hayo alipokuwa akitoa ushuhuda kwenye mkutano wa kuhitimisha mradi wa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na kukomesha ukatili kwa vijana na watoto wa Pepfer FBO Initiative uliokuwa ukiendeshwa wilayani Rungwe na shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania.

Alisema kupitia vifungu kadhaa vilivyopo kwenye Biblia alikuwa akiwakataza waumini waliokuwa na maambukizi ya VVU wasitumie ARV’s na kuwataka wategemee maombi aliyokuwa akiwafanyia mpaka alipokutana na waratibu wa mradi wa Pepfer FBO Initiative aliosema walichukua muda mwingi kumbadilisha.

Alisema hadi anafikiwa na mradi huo alikuwa na waumini 15 waliokuwa wakiishi na maambukizi ya VVU na alikuwa amewaachisha kutumia dawa na wanne kati yao walikuwa taabani huku watatu wakiwa tayari wamefariki dunia.

Alisema kinachomuuziza zaidi ni kuona hata alipofuatwa na ndugu wa wamumini waliopoteza maisha na kumlilia kuwa amechangia vifo vya ndugu hao kwa kuwakataza dawa, aliwaaminisha kuwa ndugu zao walikufa kishujaa na wako mbinguni kutokana na kufa wakiwa na imani

Chanzo: Gazeti la Habari Leo
 
ARV ni kama sigara kwenye damu

Huwezi kumuambia mtu ametumia ARV kwa miaka mitano aache tu ghafla, lazima atateteleka kiafya

Anatakiwa aache pole pole mpaka mwili uzoee siyo ghafla tu acha

Mbaya zaidi hakuna aliyewahi kuzipinga hizo ARV na akabaki salama popote duniani
 
Ndo maana huwa sikubaliani na kitu kinaitwa "MAOMBI" katika kutatua matatizo.
Haya makanisa yanayojiita ya kiroho mengi yanapotosha sana.
Ila waumini nao wanatakiwa kutumia akili sio wanaendeshwa na mchungaji
 
ARV ni kama sigara kwenye damu

Huwezi kumuambia mtu ametumia ARV kwa miaka mitano aache tu ghafla, lazima atateteleka kiafya

Anatakiwa aache pole pole mpaka mwili uzoee siyo ghafla tu acha

Mbaya zaidi hakuna aliyewahi kuzipinga hizo ARV na akabaki salama popote duniani
anzisha uzi wa hili somo ,udadavue
 
Back
Top Bottom