Rungwe: Mchungaji aomba msamaha kwa kukataza waumini wake kutumia ARV'S na kusababisha wengine kufariki

Rungwe: Mchungaji aomba msamaha kwa kukataza waumini wake kutumia ARV'S na kusababisha wengine kufariki

Tatizo muda, sina muda kabisa

Mbaya zaidi hizo ni biashara za watu
najua biashara za watu ndio ,hata wewe unajiita miti 7 na sio jina halisi ,tafuta muda usaidie wengi
 
najua biashara za watu ndio ,hata wewe unajiita miti 7 na sio jina halisi ,tafuta muda usaidie wengi
Pekua vizuri hii jf hakuna ambacho hakijaandikwa

Nenda jf intelligence hakuna ambalo halijaandikwa
 
Hawa wachungaji vilaza kweli

Unawakataza watu wasitumie dozi

Wakati wao wenyewe hawana tiba mbadala

Huyo mchungaji kilaza ashikishwe adabu tu

Ova
Halafu wakifa unafurahi na kukenua hadi jino la 32 na kusema sasa wako kwa Mungu! Hui ni uuaji kabisa.
 
Afadhari hata huyu ambaye amepata ufunuo akaamua kuchukua hatua ya kutubu!
Yupo Askofu maarufu hapa Tanzania ambaye kwa miaka mingi alikuwa kinyume na Serikali mpaka aliposhikishwa adabu na Serikali fulani ambayo ilikuwa haiangalii uso wa mtu.
Katika miaka ya mwanzoni ya 2000 alikuwa akiwafundisha waamuni wake kutotumia ARVs badala yake wamtegemee Mungu kwa maombi.
Lakini alienda mbali zaidi baada ya maombi na kufunga ya muda mrefu kanisani kwake aliwatangazia waumini wake kuwa Roho Mtakatifu amemwonyesha dawa ya Ukimwi na kumhakikishia mara 50!
Na akawahakikishia kuwa Watakuja na kufurika Kanisani waarabu na wazungu kutafuta dawa ya Ukimwi.
Hatimaye akatangaza siku rasimi ya kuja kupata dawa hiyo! Siku ya siku aliyotangaza Watu wakafurika lakini hakuna kilichotokea!
Wakati huo waumini waliokuwa Waathirika walikufa kwa wingi sana.
Basi baada ya miaka mingi kadhaa kupita ndipo alipofunguka na kuelekeza waumini kutumia ARVs.
Kwa kweli pamoja na Ukimwi unaua lakini waathirika wengi wa Imani ya Kilokole wamekufa kwa wingi kwa kuaminishwa kuwa Maombi tu yanatosha kuwaponya!
 
Wana wa Adamu bwana,hiv ujinga wa mzee Adamu wa kujificha mbele ya hadhira za muumba tutaacha lini?Wewe kipimo kimeonesha una "hiv",aliye kupa ama unamjua au haumkumbuki(si muhimu)unamlilia Yesu akuponye kwani ndiye aliyekupa?Unaambiwa dawa za kutibu hakuna zipo za kupunguza makali we hutaki!Unataka mbingu si unywe kadawa ka nyasi uwahi huko mbinguni?Tumia dawa bwana acha usumbufu halafu usingizie mchungaji wakati umeumbwa na akili kama yeye wewe kwa ujinga wako hutaki kutumia zako utakufa siku si zako umuache mchungaji wako akijichungia bata za kutosha.Tafuta taarifa za kutosha juu ya jambo unaloliendea ili kupunguza athari na gharama.Haloooo.....kumbe naongea na sim..
 
Hasa wanawake, wakiingia huko atamuheshimu mchungaji kuliko mume wake.
Utasikia, " Leo tuna zamu ya kumsaidia Mama Mchungaji". Mke uoe wewe halafu akafanye kazi ya kumpikia Mchungaji? Ndoa nyingi zinapata msukosuko na mipasuko hasa kwa jinsi kinamana wanavyowaheshimu sana hao jamaa kupita hata waume zao.
 
Utasikia, " Leo tuna zamu ya kumsaidia Mama Mchungaji". Mke uoe wewe halafu akafanye kazi ya kumpikia Mchungaji? Ndoa nyingi zinapata msukosuko na mipasuko hasa kwa jinsi kinamana wanavyowaheshimu sana hao jamaa kupita hata waume zao.
Kabisa mkuu, yaani mtu anayesema anataka kuoa mlokole huwa namshangaa sana
 
ARV ni kama sigara kwenye damu

Huwezi kumuambia mtu ametumia ARV kwa miaka mitano aache tu ghafla, lazima atateteleka kiafya

Anatakiwa aache pole pole mpaka mwili uzoee siyo ghafla tu acha

Mbaya zaidi hakuna aliyewahi kuzipinga hizo ARV na akabaki salama popote duniani
Yaani ARV's unazilinganisha na fegi!
 
serikal imemuacha huru au atatumikia kifungo?
Ulishasikia "maungamo ya hiari" yanasotesha mtu jela?

**** wauaji,majambazimateja nk nk walishawahi jitokeza hadharani na kukiri hadharani katika jamii na kukiri kuachana na hayo matendo, ushasikia wakakamatwa na kushitakiwa?

Kwanza serikali ndivyo inavyotaka raia tubadilike tukiri kwa kujuta makosa yetu kama alivyofanya huyo mheshimiwa mchungaji.
 
Sioni sababu ya kuulaumu ulokole maana kila mtu ameumbwa na akili za kuchanganua.. Ukiona unaakili za kumtegemea mtu basi wewe huna akili kabisa..kuna msemo unasema akili za kuambiwa changanya na zako..by the way kuna bible naona kila kitu kimeelekezwa humo so mi naona ukifata vile bible inaeleza huwezi kuyumbishwa na maneno ya mtu haijalishi ni mch. Askofu, mtume n.k
 
Back
Top Bottom