Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

56cb742d9275a16ee717d8e407d4b38f.jpg

Mashine yangu ya ukweli! Nachimbua tu! Maisha yanakwenda!
Mkuu umejitahidi kuamisha kama yako nioneshe kwenye ring sensa yake,Ndo ujue má master tunazijua kama haujaamisha sehemu
 
kuna mtu alisha chimba eneo lote na alibakiza kidogo aka kata tamaa
mzungu alipo kuja almanusura akate tamaa ila nilichogundua huwa wana kuja na raman na huwa wana zikuta mali zote zipo in short ngum sna kuzipata
 
Kuna ukweli kwa hili huku kwetu ushora kuna kanisa walijenga kwa mawe halafu kwenye madhabahu wakaficha mali mwaka juzi walikuja wakasema wanarekebisha wakavunja wakachukua mali zao wakasepa
Hao waliohusika kujenga hiyo madhabahu hawakujua kuna mzigo apo? Au walikibitiwa mapema baada ya kumaliza kazi
 
Jamani hiii nikweli waliacha mali Tanzania..kuna maeneo mengi ukitembea milimani utakuta vyuma flani vya mviringo vimejazwa udongo wa cement kali.juu kuna maandishi yanaonesha vipimo flani vya umbali kutoka usawa wa alama hiyo ilipo.ninae changia maada hii ninauhakika. Ila cjawahi kuona wamefika na kuchukua mali ila hali hii ipo kabisa.. Nivigum kuamini kwasababu tumechelewa kupata elim lkn habari hii ni yakweli kabisa
Uongo tu kaka,hakunaga mambo kama hizo..sahau mkuu,ni kama habari za Freemason
 
Hizo habari zipo na kweli kuna maeneo nimepata kuyaona yanatia mashaka sana, kuna shule moja nilisoma ile shule imejengwa na wakoloni na tangu waondoke kuna handaki moja limejengwa kwa zege imara na juu limefunikwa ( pia kuna mlima mmoja huko kwetu hadi leo unawekewa ulinzi na kuna mzungu mmoja alikuwa anafanya utafiti sana eneo hilo ni mwanajeshi mstaafu wa nchi moja huko ulaya) hizi habari kuna sehemu naweza kuziamini kwa kile ninachokiona.....kama hujawahi kushuhudia huwezi kupata hoja ya Nguvu kwenye huu uzi
 
Kuna mwana ambaye aliwahi kuhusika Ktk utafutaji wa hzo mambo bila Mafanikio, Zilikua chini ya Ardhi na walitumia mpk mashine ya kunyonyea maji ila, Walikua na Mganga wao na ilifika Hatua wakakutana na michoro ktk mwamba ambao ulikua unatoa uelekeo..
yle Mganga akawaambia ili kwenDa chini zaiDi inabidi Damu imwagike kwakua hlo Eneo Kuna Damu za watu zilimwagika
Kwa kifupi Issue ilikua na mambo ya Ajabu sana na hawakufanikiwa licha ya Gharama zote walizoingia
 
Huu msemo ni kweli kabisa. Hizo fedha za kijerumani zipo sehemu mbali mbali Chini ya ardhi au milima. Miaka ya 90 wazungu walifika kijijini kwetu na kununua eneo kubwa kwa ajili ya ufugaji, wakaajiri wafanyakazi kama 50. Katika shamba Lao hawakufikisha hata ng'ombe 100. Walikaa kama miaka saba hivi, sasa inasemekana walikuwa wanatafuta mali ambazo zilifukiwa na babu zao, na walifanikiwa kupata sanduku mbali za shaba, ila haikujulika mlikuwa na nini. , walipofanikiwa tu walikabidhi shamba Lao kwa serikali wakaondoka zao, mifugo, magari ng'ombe na mbuzi hawakuwa na shida nao tena. Watu wengine hubahatika kuoteshwa wapi zilipo pesa hizo ila masharti yake magumu, uwe na roho ya jiwe, unaweka mwanao hapo unaichimba, kila ukiikaribia mwanao anazidi kudhoofika,.
 
Kati ya makanisa ya katoliki makubwa zaidi afrika mashariki na kati la tatu lipo wilaya ya mbulu manyara, lile kanisa lina milingoti 12 na underground ya kutosha tu. Jamaa walijidai kujenga kwa msaada kumbe walikuwa wanachukua chao na cha kishangaza zaidi pembeni kuna uwanja mdogo wa ndege na zilikuwa zinatua usiku kwa usiku. Kuna ukweli ndani ya hili suala.
 
Hili suala kutokana na shahidi mbalimbali zilizotolewa na wachangiaji inaweza ikawa ni kweli
 
Hizo habari zipo na kweli kuna maeneo nimepata kuyaona yanatia mashaka sana, kuna shule moja nilisoma ile shule imejengwa na wakoloni na tangu waondoke kuna handaki moja limejengwa kwa zege imara na juu limefunikwa ( pia kuna mlima mmoja huko kwetu hadi leo unawekewa ulinzi na kuna mzungu mmoja alikuwa anafanya utafiti sana eneo hilo ni mwanajeshi mstaafu wa nchi moja huko ulaya) hizi habari kuna sehemu naweza kuziamini kwa kile ninachokiona.....kama hujawahi kushuhudia huwezi kupata hoja ya Nguvu kwenye huu uzi
Ulinzi kivipi mkuu,analinda nani,jeshi gani?!,ni wapi huko mkuu
 
Mlimani hauruhusiwi kufika kabisa na askari polisi muda wote wapo doria kwenye huo mlima ila shuleni hakuna mtu anaelinda.
Kwahiyo mkuu hapo pana ulinzi na polisi wanapangiwa zamu tangu enzi za mkoloni?!
Bro are you serious?!!
Ni wapi huko,mlima unaitwaje?!
 
Kwahiyo mkuu hapo pana ulinzi na polisi wanapangiwa zamu tangu enzi za mkoloni?!
Bro are you serious?!!
Ni wapi huko,mlima unaitwaje?!
Ni kweli mlima una ulinzi na ni ngumu kufika huko....nilielezwa kuwa una mahandaki mle mlimani.....yule mzungu kwa maelezo Amekuja kufata hivyo vitu walivyoacha hao wenzake ila hajatembea hapo tu inasemekana singida pia kafika na maeneo mbalimbali hapa Nchini....na akifika sehemu huanzisha mradi wowote mkubwa wakati anaendelea na uchunguzi wake.....na baadae huiacha hata hiyo miradi pale anapokuwa ametimiza kile alichotaka kufahamu.

Haya mambo nahisi ni ya kweli kuna vitu wazungu waliacha.
 
Back
Top Bottom