Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

Mauzauza kabisa, natamani ungeendela zaidi kama uko na nafasi ya kuongea!
Naweza ongea kiasi ila sio deep sana kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu, miaka minne au mitano nyuma ndio sekeseke la hizi mali lilipoanzia kwa upande wangu sitasema sana ilikuaje ila nilitakiwa kufika eneo husika katika mkoa ambao sio nilipo nilimuagiza mke wangu alienda akaingia sehemu husika ni pango nje kidogo ya mji huo kuna mavazi alitakiwa kuvaa na siku maalumu kwa ajili ya kuona vitu vile siku ilipofika alienda akaona vilivyopo kisha akakabidhiwa funguo ya pale arudi nayo (cheni ina maajabu kidogo sababu wiki ya kwanza kile kinachoning'inia kilikua kinabadilika umbo lake) akapewa baadhi ya maagizo aje kunipatia alirudi akanieleza vyote vilivyotukia na maagizo ya pale ambayo yote kwa ujumla niliyakamilisha mwaka jana hivi vitu ni real hata mimi sikua na uhakika hadi niliposhuhudia maana hata ramani yake imeandikwa kijeruman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa kushare, ila nimenusa harufu ya msaada wa mganga hapo! Nilitamani nisikie kutoka kwa aliyeviona bila kupitia kabisa kwa mganga kutafuta msaada wa kuvipata hivi vitu.Maana waganga nao wanamazingaombwe yao wanaweza kukuwekea hivyo vitu unadhani vipo kumbe ni bikini macho vya waganga.Thanks man.

Sijawahi pitia kwa mganga na huwezi pata pitia mganga sababu ya ulinzi wa hizi sehemu,mganga hawezi thubutu hizi sehemu kwa msaada hii sehemu ni chimbuko la mke wangu mama yake alizaliwa maeneo hayo kuna kahusiano fulani ambacho bado sijapata uhakika sana ila aliponiambia ndani ya hiko kijiji ndipo chimbuko la mama yake mzazi,msaada niliupata pitia marafiki kwangu au walimu watu wengi hupenda kuwaita hivyo, siwezi weka mtiririko wote kama nilivyosema ila sijawahi pata msaada wa mganga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry mkuu, nilipata hizo hisia sababu ya hivyo vigezo vya mavazi na mida ya kuingia nikaweka hapo dhana ni kwa masharti. Thank you again🙏
Sijawahi pitia kwa mganga na huwezi pata pitia mganga sababu ya ulinzi wa hizi sehemu,mganga hawezi thubutu hizi sehemu kwa msaada hii sehemu ni chimbuko la mke wangu mama yake alizaliwa maeneo hayo kuna kahusiano fulani ambacho bado sijapata uhakika sana ila aliponiambia ndani ya hiko kijiji ndipo chimbuko la mama yake mzazi,msaada niliupata pitia marafiki kwangu au walimu watu wengi hupenda kuwaita hivyo, siwezi weka mtiririko wote kama nilivyosema ila sijawahi pata msaada wa mganga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili suala la Rupia Luna kipind ilifikia hatua mm nikaamini kwan ndugu yangu alisema kuwa baba yake na babu yetu alikuwa na hzo rupia na aliziweka mahali Fulani sasa ikaleta shda sana akachimba chumbani hakuna akarud tena kwa mganga a akaambiwa et avunje NYUMBA mi nikasema hapana kama unauhakika jenga NYUMBA nyingne kama hyo halaf hyo ya zamani vunja halaf tuvunje kwenye mgao WEWE utachukua asilimia 60% sasa naona had Leo kimya
 
MwanaJF,

Je, umeshawahi kusikia visa na mikasa ya watu wanaotafuta rupia maarufu kama pesa au hazina ya Mjerumani?

Binafsi nimekuwa nikisikia kuna watu huwa wanakwenda mahala ambapo wamepewa viashiria kuwa kuna rupia na huchimba kama wachimbavyo wachimbaji wa migodini.

Hii shughuli ni maarufu sana mkoani Mbeya na Njombe, Iringa, nimewahi ona tukio la nyumba kubomoka baada ya watu waliokuwa wakichimba chini kwa chini kutokezea kwenye nyumba ya mzee mmoja huko Mbeya.

Maswali yangu ni:

1. Je, kuna ukweli wowote wa hili jambo?
2. Je, rupia ni nini...ni pesa hasa au aina fulani ya kitu cha thamani?
3. Je, rupia hutumiwaje baada ya kupatikana? kwani kuna tetesi kuwa ina thamani kubwa sana.
4. Kuna mtu ashawahi kuiona hiyo rupia?

Nawasilisha
A very good overview Mshanah Jr,hongera.
 
Hapa Mbimba kuna uwezekano mkubwa kwanza lile bwawa lina miujiza ya kumeza wengi pia mradi wa utafiti wa mbegu za kahawa unaolizunguka bwawa hilo unafadhiliwa na EU inadaiwa njia ya kuingilia kwenye ipo katikati ya bwawa hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbozi naskia hata pae Mbozi mission pia ,hii dunia hii
[emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja kwa moja utawaza kuhusu rupia(rupee ya mjerumani) na pesa nyingine za kale na yale yanayosemwa kuzihusu hasa kwenye habari nzima za kichawi
Watu wamezinguka na kuzinguliwa hasa watu wametapeliwa na wengine kufa wakitafuta hivi vitu vinavyotajwa kuwa na thamani kubwa

Ukweli huu hapa na si pesa tu bali na vitu vingine vya kale
1. Aina ya malighafi iliyotumika
Wakati huo vilitengenezwa vitu imara sana kutokana na upatikanaji wa malighafi ya kutosha ...vitu kama vyombo vya bati na chuma urembo kama bangili mikufu pete nk leo hii ukivipata na kuviyeyusha kila kimoja unaweza kutengeneza kumi kupitia hicho kimoja

2. Uhifadhi
Wajerumani kwa hapa kwetu walikuta malighafi vito na madini ya kutosha sana! Kutokana na uhifadhi hafifu wakati huo vingi ya hivi vitu viliwekwa tu majumbani mwao wakiviandaa kuvidafirisha kwao
Vita ya pili ya 1939-45 iliwachanganya mno na walipoelekea kushindwa waliamua kuficha mali yote kwenye mashimo makubwa mashambani misituni kwenye mahandaki na milimani kusikofikika kwa urahisi kisha wakawaua watu karibia wote walioshiriki na wanaojua yale maficho wakasepa
Huku kote mali hizo zilihifadhiwa kwenye vyumba imara vilivyojengwa kwa zege gumu hasa ili iwe ngumu kuchimbua ama kuvunja na kama ni mapangoni yalikuwa mapango ya mbali hasa milimani na misituni

3. Dhana ya majoka na viumbe wa ajabu
Huko kwenye hayo maficho kuna baadhi ya watu walisalimika hivyo wakasimulia vizazi vilivyofuata
Kizazi cha kusaka utajiri wa haraka kikaona fursa na kuamua kuchangamkia dili. ..Wajerumani hawakuweka ulinzi wowote wa majoka! Hao ni viumbe tu walijitwalia makazi huko ambako ndio maisha yao yaliko
Watu walioenda bila tahadhari waliumwa na hayo madubwana na kupoteza maisha! Waliosalimika walitimua mbio na kuunda stories za kufikirika

4. Dhana ya uchawi na majini
Kwa wale waliosaka kwenye mahandaki na mashimo marefu yenye vyumba vilivyojengwa kwa zege , baada ya kufanikiwa kuvunja hayo mazege na kutaka kuingia ndani nao walikutana na mauzauza ya kila aina
Unajua ni kwa nini? Sehemu yoyote yenye mfumo wa nyumba ama chumba isiyokaliwa na binadamu roho zinazotangatanga na mapepo hufanya makazi yao kumbuka ile mada ya kutakasa makazi! Hivyo ukiingia huko lazima ukutane na vitu vya ajabu...Mjerumani hahusiki kabisa!

5. Uamuzi wa kufanya kafara ama tambiko kabla ya kuchimba ama kuingia pangoni
Wengi walitafuta waganga wa kienyeji kwenye hili na hawakufanikiwa. ..waliofanikiwa walifanikiwa kwa ujanja tuu....ukienda kwenye pango misituni ukachinja mnyama ukapiga manyanga automatically mkiondoka ile nyama italiwa na kuna wakati manyanga huleta kelele na kufukuza mnyama yoyote aliyeko pangoni...ndio maana baada ya kafara hamuingii siku hiyo hiyo bali kesho yake nk
Wale wa kwenye mashimo NA mahandaki ni ibada tu ya kuziomba roho ziondoke ama kuzifukuza kwa kutumia mitishamba na harufu wasizozipenda....mkikutana na roho korofi mtachezea kichapo mpaka muache kila kitu na kutimua mbio kali sana

6. Ukweli hasa ni UPI?
Baada ya vita ya pili kukoma na baadae Uhuru wajerumani walishindwa kurudi kwa ubabe hivyo wakatumia njia za kijanja kurudi
Unajua waliondoka na ramani zote kule mali zilikofichwa hivyo walirudi kuzichukua kwa njia ya kununua yale maeneo na kuyaendeleza kwa kujenga shule vyuo hospital nk ama miradi ya barabara ufugaji na kilimo
Kwa njia hii walichukua vyao kiulaini mno

7. Thamani na umaarufu wake ni UPI!?
Vitu vya kale kwa wenzetu vina thamani kubwa sana....wenzetu wana utaratibu wa kuweka vituo vya antiques na kuchaji watalii pesa ndefu kuviangalia . kila kimoja kinakuwa kimeandikiwa historia yake. Kwa hiyo wakija huku kuvitafuta wengi huenda kuviuza kwenye hayo maduka kwa bei kali mno

8. Nguvu ya utajiri
Biashara imevamiwa , vitu vya kale haviwezi kukupa utajiri wa miujiza ..havina huo uwezo bali kuna baadhi kutokana na malighafi iliyotumika kuvitengeneza vina mvuto kwenye ulimwengu wa giza kama mabangili ya shaba

9. Usumbufu
Kuna watu wanawachezea wenzao shere na kuwasumbua bila sababu.. Miaka hiyo pesa ilitengenezwa kwa mpango maalum(nadhani hata sasa) na zilitengenezwa kwa miaka... Kuna miaka pesa hazikutengenezwa. Sasa mtu anakupa dili na kukuahidi kukupa pesa ndefu ukimletea rupee ya mwaka fulaniView attachment 526110

10. Hitimisho
Kuna baadhi ya sehemu kulikofichwa hizo mali wafichaji walinuizia ama kufanya mambo ya giza ili atakayejaribu kuchukua ama apate madhara au asizione kabisa...lakini kwa sehemu kubwa ni habari zilizotiwa chumvi nyingi

JUMAPILI NJEMA
Jr[emoji779] [emoji781]
Vintage Mshana Jr

Huwa nakukubali sana mkuu, ulivyopangilia hizi hoja ni kama thesis ya PhD.

You're a great thinker indeed
 
Mbozi September 27, 2008

WAFA WAKICHIMBUA VITO VYA WAJERUMANI

WATU watatu wamefariki wakifukua hazina inayodhaniwa kufukiwa na wamishionari Wajerumani katika kijiji cha Mbozi wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Tukio hilo lililotokea juzi mchana katika eneo la kanisa la Moravian usharika wa Mbozi Mission lilisababishwa na watu hao kukosa hewa katika shimo hilo ambalo linaaminiwa kufukiwa dhahabu na rupia.

Afisa Mtendaji kata ya Igamba Ambakisye Waya amewataja marehemu kuwa ni Green Sichone (50), mapacha Erick na Sadock Mnkondya (30) wote wakazi wa kijijini hapo.

Waya alisema kuwa mapema mwaka huu wachimbaji hao walipata taarifa kutoka kwa mtu asiyefahamika zikielezea kuwepo kwa hazina kubwa ya dhahabu, sarafu na vito mbalimbali vya thamani vilivyohifadhiwa na wamishenari wa Kijerumani waliofika kufungua misheni hiyo mwaka 1902.

“Agosti mwaka huu watu hao walituma maombi kwa baraza la wazee wa kanisa chini ya Mchungaji Lordrick Sichone ya kutaka kuchimbua eneo hilo na kutafiti iwapo haizna hiyo ipo, baraza liliwaruhusu kufanya kazi hiyo” Aliongeza mtendaji huyo.

Alisema kuwa watu hao walichimba mashimo mawili kati ya mwezi Agosti na Septemba ambapo katika shimo la pili lililokuwa na upana wa mita 2 na kina mita 17 walipata vikwazo kwa kuibuka maji na upungufu wa hewa ambapo iliwalazimu kutumia mashine ya kuvuta maji na kupeleka hewa.

Naye Mchungaji Sichone alisema kuwa baada ya kuona watu hao hawatokei kwa muda mrefu aliamua kwenda kuchungulia ambapo aliona shimo likiwa limejaa moshi na harufu ya petroli na maiti wakielea juu ya maji.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zerothe Stephen alithibitisha tukio hilo na akamtaja Mchungaji Sichone kuwa ndiye aliyegundua tukio hilo.

Chanzo: maishanivita dot blogspot dot com
 
Sijui walilipua nini huko chini

Hizi mambo zipo sababu kwa upande wangu nimebahatika kuzijua kwa msaada fulani ila sio mfatiliaji sana huwa siwekei maanani sana, kuna kikundi cha watu walikua wanatafuta sana hizi mali nilikutana nao lakini kwa muongozo niliona wana tatizo kidogo lakini sikuamua kujali sana nakumbuka mwaka jana nilijaribu kuwapelekea kitu kati ya vitu wanavyohitaji asee sisahau ile siku ilikua kila nikibeba kitu sifiki mbali kinarudi nyumba niliyofikia zaidi ya mara nne nilipata maelezo kidogo ya kuwahoji matokeo yake wakawa hawaeleweki mwisho kitu chenyewe kikarudi mahala pa kwanza kilipotoka...kwa tukio lile hata wife alijua kuwa havikua vitu vya kawaida..sijaeleza kwa mfuatano mzuri kwasababu binafsi ila hizi vitu vipo ila kubahatika kuvijua ni bahati tu

Sent using Jamii Forums mobile app
embu ni pm au nyoosha history nzima
 
Back
Top Bottom