Rupia: Hazina ya Mjerumani

Mauzauza kabisa, natamani ungeendela zaidi kama uko na nafasi ya kuongea!
Naweza ongea kiasi ila sio deep sana kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu, miaka minne au mitano nyuma ndio sekeseke la hizi mali lilipoanzia kwa upande wangu sitasema sana ilikuaje ila nilitakiwa kufika eneo husika katika mkoa ambao sio nilipo nilimuagiza mke wangu alienda akaingia sehemu husika ni pango nje kidogo ya mji huo kuna mavazi alitakiwa kuvaa na siku maalumu kwa ajili ya kuona vitu vile siku ilipofika alienda akaona vilivyopo kisha akakabidhiwa funguo ya pale arudi nayo (cheni ina maajabu kidogo sababu wiki ya kwanza kile kinachoning'inia kilikua kinabadilika umbo lake) akapewa baadhi ya maagizo aje kunipatia alirudi akanieleza vyote vilivyotukia na maagizo ya pale ambayo yote kwa ujumla niliyakamilisha mwaka jana hivi vitu ni real hata mimi sikua na uhakika hadi niliposhuhudia maana hata ramani yake imeandikwa kijeruman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa kushare, ila nimenusa harufu ya msaada wa mganga hapo! Nilitamani nisikie kutoka kwa aliyeviona bila kupitia kabisa kwa mganga kutafuta msaada wa kuvipata hivi vitu.Maana waganga nao wanamazingaombwe yao wanaweza kukuwekea hivyo vitu unadhani vipo kumbe ni bikini macho vya waganga.Thanks man.
 
Sijawahi pitia kwa mganga na huwezi pata pitia mganga sababu ya ulinzi wa hizi sehemu,mganga hawezi thubutu hizi sehemu kwa msaada hii sehemu ni chimbuko la mke wangu mama yake alizaliwa maeneo hayo kuna kahusiano fulani ambacho bado sijapata uhakika sana ila aliponiambia ndani ya hiko kijiji ndipo chimbuko la mama yake mzazi,msaada niliupata pitia marafiki kwangu au walimu watu wengi hupenda kuwaita hivyo, siwezi weka mtiririko wote kama nilivyosema ila sijawahi pata msaada wa mganga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry mkuu, nilipata hizo hisia sababu ya hivyo vigezo vya mavazi na mida ya kuingia nikaweka hapo dhana ni kwa masharti. Thank you again🙏
 
Hili suala la Rupia Luna kipind ilifikia hatua mm nikaamini kwan ndugu yangu alisema kuwa baba yake na babu yetu alikuwa na hzo rupia na aliziweka mahali Fulani sasa ikaleta shda sana akachimba chumbani hakuna akarud tena kwa mganga a akaambiwa et avunje NYUMBA mi nikasema hapana kama unauhakika jenga NYUMBA nyingne kama hyo halaf hyo ya zamani vunja halaf tuvunje kwenye mgao WEWE utachukua asilimia 60% sasa naona had Leo kimya
 
A very good overview Mshanah Jr,hongera.
 
Mbozi naskia hata pae Mbozi mission pia ,hii dunia hii
[emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vintage Mshana Jr

Huwa nakukubali sana mkuu, ulivyopangilia hizi hoja ni kama thesis ya PhD.

You're a great thinker indeed
 
Mbozi September 27, 2008

WAFA WAKICHIMBUA VITO VYA WAJERUMANI

WATU watatu wamefariki wakifukua hazina inayodhaniwa kufukiwa na wamishionari Wajerumani katika kijiji cha Mbozi wilayani Mbozi mkoani Mbeya.

Tukio hilo lililotokea juzi mchana katika eneo la kanisa la Moravian usharika wa Mbozi Mission lilisababishwa na watu hao kukosa hewa katika shimo hilo ambalo linaaminiwa kufukiwa dhahabu na rupia.

Afisa Mtendaji kata ya Igamba Ambakisye Waya amewataja marehemu kuwa ni Green Sichone (50), mapacha Erick na Sadock Mnkondya (30) wote wakazi wa kijijini hapo.

Waya alisema kuwa mapema mwaka huu wachimbaji hao walipata taarifa kutoka kwa mtu asiyefahamika zikielezea kuwepo kwa hazina kubwa ya dhahabu, sarafu na vito mbalimbali vya thamani vilivyohifadhiwa na wamishenari wa Kijerumani waliofika kufungua misheni hiyo mwaka 1902.

“Agosti mwaka huu watu hao walituma maombi kwa baraza la wazee wa kanisa chini ya Mchungaji Lordrick Sichone ya kutaka kuchimbua eneo hilo na kutafiti iwapo haizna hiyo ipo, baraza liliwaruhusu kufanya kazi hiyo” Aliongeza mtendaji huyo.

Alisema kuwa watu hao walichimba mashimo mawili kati ya mwezi Agosti na Septemba ambapo katika shimo la pili lililokuwa na upana wa mita 2 na kina mita 17 walipata vikwazo kwa kuibuka maji na upungufu wa hewa ambapo iliwalazimu kutumia mashine ya kuvuta maji na kupeleka hewa.

Naye Mchungaji Sichone alisema kuwa baada ya kuona watu hao hawatokei kwa muda mrefu aliamua kwenda kuchungulia ambapo aliona shimo likiwa limejaa moshi na harufu ya petroli na maiti wakielea juu ya maji.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zerothe Stephen alithibitisha tukio hilo na akamtaja Mchungaji Sichone kuwa ndiye aliyegundua tukio hilo.

Chanzo: maishanivita dot blogspot dot com
 
Sijui walilipua nini huko chini
 
embu ni pm au nyoosha history nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…