Rupia na Hela za Zamani:
Nimekuwa na habby ya kukusanya na kuhifadhi vitu vya zamani kwa mda mrefu sasa. Na hivi karibuni nikaanza kukusanya Rupia, Hela za matobo, Sarafu na noti za zamani za Tanzania, Sarafu za toleo maalum, etc za East Africa and Africa kiujumla, nchi za kiarabu, india and nchi nyingine nyingi.
Kufikia sasa nina hela nyingi sana, karibu ndoo ya lita kumi kujaa.
Thamani:
Pia mimi sioni hizi zikiuzwa mamilioni mengi, ila nimekutana na watu wengi wanaziuza mpaka rupia moja milioni tano hadi kumi na kuendelea. Watu hawa ninapowaambia pia mimi ninazo kama wanazouza, huwa wanataka wanishirikishe ili kutapeli watu - kitu ambacho huwa nakataa. (Inasemeka zinatumika katika uganga, kujikinga na kusindikwa / kuzikwa .. ndio maana 'wateja' wanaoamini mambo haya huwa wako tayari kutoa hela nyingi ili kufanikisha 'mission' zao.
Kwa kweli sasa tukizungumzia thaman halisia, kuna wateja wengi ambao hununua hizi hela kama kumbukumbu, historia au kuongezea kwenye collection zao za hobby hii (haswa wazungu, wahindi, waarabu na pia waswahili hapa na pale).
Kwa hiyo kweli ukiwa nazo sio mbaya, hela ipo.... kulingana na hela uliyo nayo, unaweza kuuza dola 2, 5, 15, 22 hadi mia na mia hamsini.
Kwa mfano na hela za kwanza za tanzania au hela za matobo, hata ukiuza kila moja dola tano na una sarafu elfu moja (kama mimi), sio hela mbaya. Na unavyozidi kukaa nazo ndivyo zinavyopanda bei.
Usitapeliwe, pengine kama mganga wako amekutuma na unaamini mambo hayo.
sample hela nilizonazo hi sarafu nyingi na noti za zamani, na special issue coins kama ya uhuru na pia ya Sh elfu 50,000 ya Karume. (ningekua najua jinsi ya kuweka picha hapa ningewaonesha - nielekezeni niweke picha)
Asante