Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

Moja kwa moja utawaza kuhusu rupia(rupee ya mjerumani) na pesa nyingine za kale na yale yanayosemwa kuzihusu hasa kwenye habari nzima za kichawi
Watu wamezinguka na kuzinguliwa hasa watu wametapeliwa na wengine kufa wakitafuta hivi vitu vinavyotajwa kuwa na thamani kubwa

Ukweli huu hapa na si pesa tu bali na vitu vingine vya kale
1. Aina ya malighafi iliyotumika
Wakati huo vilitengenezwa vitu imara sana kutokana na upatikanaji wa malighafi ya kutosha ...vitu kama vyombo vya bati na chuma urembo kama bangili mikufu pete nk leo hii ukivipata na kuviyeyusha kila kimoja unaweza kutengeneza kumi kupitia hicho kimoja

2. Uhifadhi
Wajerumani kwa hapa kwetu walikuta malighafi vito na madini ya kutosha sana! Kutokana na uhifadhi hafifu wakati huo vingi ya hivi vitu viliwekwa tu majumbani mwao wakiviandaa kuvidafirisha kwao
Vita ya pili ya 1939-45 iliwachanganya mno na walipoelekea kushindwa waliamua kuficha mali yote kwenye mashimo makubwa mashambani misituni kwenye mahandaki na milimani kusikofikika kwa urahisi kisha wakawaua watu karibia wote walioshiriki na wanaojua yale maficho wakasepa
Huku kote mali hizo zilihifadhiwa kwenye vyumba imara vilivyojengwa kwa zege gumu hasa ili iwe ngumu kuchimbua ama kuvunja na kama ni mapangoni yalikuwa mapango ya mbali hasa milimani na misituni

3. Dhana ya majoka na viumbe wa ajabu
Huko kwenye hayo maficho kuna baadhi ya watu walisalimika hivyo wakasimulia vizazi vilivyofuata
Kizazi cha kusaka utajiri wa haraka kikaona fursa na kuamua kuchangamkia dili. ..Wajerumani hawakuweka ulinzi wowote wa majoka! Hao ni viumbe tu walijitwalia makazi huko ambako ndio maisha yao yaliko
Watu walioenda bila tahadhari waliumwa na hayo madubwana na kupoteza maisha! Waliosalimika walitimua mbio na kuunda stories za kufikirika

4. Dhana ya uchawi na majini
Kwa wale waliosaka kwenye mahandaki na mashimo marefu yenye vyumba vilivyojengwa kwa zege , baada ya kufanikiwa kuvunja hayo mazege na kutaka kuingia ndani nao walikutana na mauzauza ya kila aina
Unajua ni kwa nini? Sehemu yoyote yenye mfumo wa nyumba ama chumba isiyokaliwa na binadamu roho zinazotangatanga na mapepo hufanya makazi yao kumbuka ile mada ya kutakasa makazi! Hivyo ukiingia huko lazima ukutane na vitu vya ajabu...Mjerumani hahusiki kabisa!

5. Uamuzi wa kufanya kafara ama tambiko kabla ya kuchimba ama kuingia pangoni
Wengi walitafuta waganga wa kienyeji kwenye hili na hawakufanikiwa. ..waliofanikiwa walifanikiwa kwa ujanja tuu....ukienda kwenye pango misituni ukachinja mnyama ukapiga manyanga automatically mkiondoka ile nyama italiwa na kuna wakati manyanga huleta kelele na kufukuza mnyama yoyote aliyeko pangoni...ndio maana baada ya kafara hamuingii siku hiyo hiyo bali kesho yake nk
Wale wa kwenye mashimo NA mahandaki ni ibada tu ya kuziomba roho ziondoke ama kuzifukuza kwa kutumia mitishamba na harufu wasizozipenda....mkikutana na roho korofi mtachezea kichapo mpaka muache kila kitu na kutimua mbio kali sana

6. Ukweli hasa ni UPI?
Baada ya vita ya pili kukoma na baadae Uhuru wajerumani walishindwa kurudi kwa ubabe hivyo wakatumia njia za kijanja kurudi
Unajua waliondoka na ramani zote kule mali zilikofichwa hivyo walirudi kuzichukua kwa njia ya kununua yale maeneo na kuyaendeleza kwa kujenga shule vyuo hospital nk ama miradi ya barabara ufugaji na kilimo
Kwa njia hii walichukua vyao kiulaini mno

7. Thamani na umaarufu wake ni UPI!?
Vitu vya kale kwa wenzetu vina thamani kubwa sana....wenzetu wana utaratibu wa kuweka vituo vya antiques na kuchaji watalii pesa ndefu kuviangalia . kila kimoja kinakuwa kimeandikiwa historia yake. Kwa hiyo wakija huku kuvitafuta wengi huenda kuviuza kwenye hayo maduka kwa bei kali mno

8. Nguvu ya utajiri
Biashara imevamiwa , vitu vya kale haviwezi kukupa utajiri wa miujiza ..havina huo uwezo bali kuna baadhi kutokana na malighafi iliyotumika kuvitengeneza vina mvuto kwenye ulimwengu wa giza kama mabangili ya shaba

9. Usumbufu
Kuna watu wanawachezea wenzao shere na kuwasumbua bila sababu.. Miaka hiyo pesa ilitengenezwa kwa mpango maalum(nadhani hata sasa) na zilitengenezwa kwa miaka... Kuna miaka pesa hazikutengenezwa. Sasa mtu anakupa dili na kukuahidi kukupa pesa ndefu ukimletea rupee ya mwaka fulaniView attachment 526110

10. Hitimisho
Kuna baadhi ya sehemu kulikofichwa hizo mali wafichaji walinuizia ama kufanya mambo ya giza ili atakayejaribu kuchukua ama apate madhara au asizione kabisa...lakini kwa sehemu kubwa ni habari zilizotiwa chumvi nyingi

JUMAPILI NJEMA
Jr[emoji779] [emoji781]
Safi sana atilisti namesahau sias kidogo [emoji113][emoji110][emoji122]
 
Asante hii kitu imenifumbua macho kwenye baadhi ya vitu maana nilikua nafikiria pia kuhusu haya mambo.

Kuna Jamaa alichimba na kujaribu kuweka hata vibarua ila akavunjika mkono ndio ikawa hivyo tena akaachana na hiyo habari.
 
Mkuu umenitoa tongotongo merci .nilikuwa nasikia hazina ya mjeruman ila sikuijua kama hivi.

Asante hii kitu imenifumbua macho kwenye baadhi ya vitu maana nilikua nafikiria pia kuhusu haya mambo.

Kuna Jamaa alichimba na kujaribu kuweka hata vibarua ila akavunjika mkono ndio ikawa hivyo tena akaachana na hiyo habari.
Kuna mengi sana kwenye ishu za rupia ya kweli na ya uongo pia ya kuzusha na story za kusadikika pia
Binafsi nimeshafika mpaka kwenye mapango ambayo kwa kuangalia tu bila hata ishu za kishirikina kuna hatari nyingi za wadudu na mimea yenye sumu kama nge tandu nk nk
 
Asante hii kitu imenifumbua macho kwenye baadhi ya vitu maana nilikua nafikiria pia kuhusu haya mambo.

Kuna Jamaa alichimba na kujaribu kuweka hata vibarua ila akavunjika mkono ndio ikawa hivyo tena akaachana na hiyo habari.

Wapi alipojaribu kuchimba...naweza pata coordinate
 
Kuna maeneo mengi watu waliamka asubuhi na kukuta mashimo tu yaliyofukuliwa usiku...ukweli ni upi!? Walipata?walikosa? Haijulikani
Eneo moja pale Mbwewe tulikuta mizoga miwili ya kondoo hirizi tunguli kaniki na zana za kuchimbia
Sijui nini kiliwatokea hao watu lakini inaelekea walitimua mbio. .
Mashimo kama haya yapo sehemu nyingi[emoji116] [emoji116] [emoji116]
1450816321167.jpg
 
Moja kwa moja utawaza kuhusu rupia(rupee ya mjerumani) na pesa nyingine za kale na yale yanayosemwa kuzihusu hasa kwenye habari nzima za kichawi
Watu wamezinguka na kuzinguliwa hasa watu wametapeliwa na wengine kufa wakitafuta hivi vitu vinavyotajwa kuwa na thamani kubwa

Ukweli huu hapa na si pesa tu bali na vitu vingine vya kale
1. Aina ya malighafi iliyotumika
Wakati huo vilitengenezwa vitu imara sana kutokana na upatikanaji wa malighafi ya kutosha ...vitu kama vyombo vya bati na chuma urembo kama bangili mikufu pete nk leo hii ukivipata na kuviyeyusha kila kimoja unaweza kutengeneza kumi kupitia hicho kimoja

2. Uhifadhi
Wajerumani kwa hapa kwetu walikuta malighafi vito na madini ya kutosha sana! Kutokana na uhifadhi hafifu wakati huo vingi ya hivi vitu viliwekwa tu majumbani mwao wakiviandaa kuvidafirisha kwao
Vita ya pili ya 1939-45 iliwachanganya mno na walipoelekea kushindwa waliamua kuficha mali yote kwenye mashimo makubwa mashambani misituni kwenye mahandaki na milimani kusikofikika kwa urahisi kisha wakawaua watu karibia wote walioshiriki na wanaojua yale maficho wakasepa
Huku kote mali hizo zilihifadhiwa kwenye vyumba imara vilivyojengwa kwa zege gumu hasa ili iwe ngumu kuchimbua ama kuvunja na kama ni mapangoni yalikuwa mapango ya mbali hasa milimani na misituni

3. Dhana ya majoka na viumbe wa ajabu
Huko kwenye hayo maficho kuna baadhi ya watu walisalimika hivyo wakasimulia vizazi vilivyofuata
Kizazi cha kusaka utajiri wa haraka kikaona fursa na kuamua kuchangamkia dili. ..Wajerumani hawakuweka ulinzi wowote wa majoka! Hao ni viumbe tu walijitwalia makazi huko ambako ndio maisha yao yaliko
Watu walioenda bila tahadhari waliumwa na hayo madubwana na kupoteza maisha! Waliosalimika walitimua mbio na kuunda stories za kufikirika

4. Dhana ya uchawi na majini
Kwa wale waliosaka kwenye mahandaki na mashimo marefu yenye vyumba vilivyojengwa kwa zege , baada ya kufanikiwa kuvunja hayo mazege na kutaka kuingia ndani nao walikutana na mauzauza ya kila aina
Unajua ni kwa nini? Sehemu yoyote yenye mfumo wa nyumba ama chumba isiyokaliwa na binadamu roho zinazotangatanga na mapepo hufanya makazi yao kumbuka ile mada ya kutakasa makazi! Hivyo ukiingia huko lazima ukutane na vitu vya ajabu...Mjerumani hahusiki kabisa!

5. Uamuzi wa kufanya kafara ama tambiko kabla ya kuchimba ama kuingia pangoni
Wengi walitafuta waganga wa kienyeji kwenye hili na hawakufanikiwa. ..waliofanikiwa walifanikiwa kwa ujanja tuu....ukienda kwenye pango misituni ukachinja mnyama ukapiga manyanga automatically mkiondoka ile nyama italiwa na kuna wakati manyanga huleta kelele na kufukuza mnyama yoyote aliyeko pangoni...ndio maana baada ya kafara hamuingii siku hiyo hiyo bali kesho yake nk
Wale wa kwenye mashimo NA mahandaki ni ibada tu ya kuziomba roho ziondoke ama kuzifukuza kwa kutumia mitishamba na harufu wasizozipenda....mkikutana na roho korofi mtachezea kichapo mpaka muache kila kitu na kutimua mbio kali sana

6. Ukweli hasa ni UPI?
Baada ya vita ya pili kukoma na baadae Uhuru wajerumani walishindwa kurudi kwa ubabe hivyo wakatumia njia za kijanja kurudi
Unajua waliondoka na ramani zote kule mali zilikofichwa hivyo walirudi kuzichukua kwa njia ya kununua yale maeneo na kuyaendeleza kwa kujenga shule vyuo hospital nk ama miradi ya barabara ufugaji na kilimo
Kwa njia hii walichukua vyao kiulaini mno

7. Thamani na umaarufu wake ni UPI!?
Vitu vya kale kwa wenzetu vina thamani kubwa sana....wenzetu wana utaratibu wa kuweka vituo vya antiques na kuchaji watalii pesa ndefu kuviangalia . kila kimoja kinakuwa kimeandikiwa historia yake. Kwa hiyo wakija huku kuvitafuta wengi huenda kuviuza kwenye hayo maduka kwa bei kali mno

8. Nguvu ya utajiri
Biashara imevamiwa , vitu vya kale haviwezi kukupa utajiri wa miujiza ..havina huo uwezo bali kuna baadhi kutokana na malighafi iliyotumika kuvitengeneza vina mvuto kwenye ulimwengu wa giza kama mabangili ya shaba

9. Usumbufu
Kuna watu wanawachezea wenzao shere na kuwasumbua bila sababu.. Miaka hiyo pesa ilitengenezwa kwa mpango maalum(nadhani hata sasa) na zilitengenezwa kwa miaka... Kuna miaka pesa hazikutengenezwa. Sasa mtu anakupa dili na kukuahidi kukupa pesa ndefu ukimletea rupee ya mwaka fulaniView attachment 526110

10. Hitimisho
Kuna baadhi ya sehemu kulikofichwa hizo mali wafichaji walinuizia ama kufanya mambo ya giza ili atakayejaribu kuchukua ama apate madhara au asizione kabisa...lakini kwa sehemu kubwa ni habari zilizotiwa chumvi nyingi

JUMAPILI NJEMA
Jr[emoji779] [emoji781]

Kuna jamaazangu fulani watu wa Mbeya walifilisika kwa kuuza kilakitu chao eti wanatafu PASS ya Mjerumani/Muingereza na Mecury. Maelezo yao sikuyaelewa ingawa walinielezea. Ila kiasi kidogo cha Mecury inatumika kusafishia kiasi kikubwa cha dhahabu huko migodini na inagharimu pesa nyingi kwa mujibu wa maelezo yao. Hitimisho walitutia hasara kwa kuwapa pesa za kula na matumizi bila mafanikio. Naomba maelezo ya habari hii kama unaufahamu nayo Jr mshana
 
Umesema kweli na kuna wajerumani wawili walikuwa na. Pikipiki kila mmoja ambazo so za kawaida zinaweza kutembea dunia mzima bila kuchakaa.Walifika mji wa malinyi jirani na mahenge
Wakauliza kijiji Fulani kipo mbali ma malinyi.Kijana mmoja walimkodia pikpiki awapeleke.Baada ya kuwafikisha wakamlipa na kumwambia aende zake.Baada ya siku mbili walipita na kutuaga kuwa wamekosa walichokuwa wanatafuta.Lakini Dalili zilionesha kuwa walipata.
 
Nakumbuka miaka fulani kijiji jirani na chetu kuna vijana walikuwa wanatafuta hiyo mali, walichimba shimo refu sana wakifuata alama zilizowekwa lakini mwisho wa siku mwenzao alikufa kimazingara ndani ya hilo shimo baada ya kukutana na nyoka wa ajabu, hali hiyo ilisababisha wenzake kukimbia
Kwa hapo ndio kuna utata, kuna sehemu nyingi sana mpaka alama zipo lakini tatizo ni mazingara ndio hukwamisha watu kuelewa kilicho ndani
 
Back
Top Bottom