KERO Rushwa barabara ya Singida - Nzega imekithiri. Magari yanajaza kupita uwezo

KERO Rushwa barabara ya Singida - Nzega imekithiri. Magari yanajaza kupita uwezo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Oct 3, 2022
Posts
5
Reaction score
3
Hatari! Hatari! Hatari!

Ndugu zangu Watanzania mtuombee tufike salama Mwanza muda huu tunaelekea Nzega

Gari nililopanda nikitokea Dar limejaza abiria balaa wengine wamesimama, wengine wamepanda kwenye daladala hili kukwepa traffic wa hapo mbele kisha watarudi kwenye BUS kuendelea kujazwa.

Traffic wa barabarani wameona hali hii ila wameruhusu gari iendelee baada ya kutoa hela ya kiwi.

Ndugu zangu hawa abiria waliosimama wote hawajafunga mkanda, gari liko spidi balaa.

Mwenye huruma na hizi roho tafadhali tunaomba MSAADA

gari ni ZUBE TRANS namb T 966 DEE
Mwanza- Dar
 
Kuna gari nimewahi kupanda wakataka kunishusha nipande mchomeko tukutane mbele nikawachomolea.
 
Kwanza hicho kipande cha nzega singida ndo kinaongiza kwa tochi za kimandazi kabisa.
 
Back
Top Bottom