Rushwa imeifikisha pabaya TAMISEMI. Je, hawa viongozi wanaoiongoza wanapaswa kuwepo hapo?

lazima wasiipende JAMIIFORUMS kwa mwendo huu, nondo kwa nondo....wanabakia uchii mda wote
 
Kila nikitaka kumtetea Nyamhanga, ninakutana na mchambuzi alieandaa vizuri hoja zake kuhusu hayo madudu. Basi Braza nimeshindwa kukutetea, lakini nashangaa kuona bado mnabofya kwenye kile kidude cha kidole hapo ofisini kwenu kusaini kila asubuhi pamoja na madudu haya bila kuwajibika
 
Ukweli wa hizi ajira MUNGU anajua
Niwatie moyo tu wale ambao mmekosa ajira tangia mwaka 2015 hadi sasa, MUNGU aliyekupigania zaidi ya miaka sita bila ajira Bado yupo hai na atakuweko milele na milele atakupigania wewe na kizazi chako

Ukweli wa ajira hizi ni sawa na shamba la mtama lililo funikwa na magugu mengi ukiwa mbali utafurahi sana kuwa shamba langu limestawi sana nina mtama mwingi
Kumbe sio.

Kivipi
Ukweli ni kwamba kuna idadi kubwa ya ajira hewa na unacho kiona utata wa hizo namba ni moja wapo ya ajira hewa, na kuna mengine yameeditiwa ambayo ni ajira hewa.

Ili tuone kuwa ni walimu wameajiliwa pengine ajira za kweli huwenda zisivuke hata alf4
Embu fikiria siku yakwanza katibu mkuu TAMISEMI anatangaza post za ajira bado aliendelea kuaadaa uma wa watanzania kuwa ni waajiriwa wapya ni 13 elfu na pia ni kwanini hawakuweka serial number? Na pia madai yao ya kujirudia rudia kwa majina na kuchanganya index namba kuwa ni matatizo ya IT na mfumo wao huo ni uongo kabisa hata mwanafunzi wa introduction to computer hawezi shindwa
Hivyo hayo yote yalikuwa planned na ukweli wanaujua

Ndio maana yule katibu wa utumishi kipindi anatoa ufafanuzi alisema wameajiri elf 8 tu na kutakuwa na awamu ya pili ambayo itachukua elfu 5 kwa sababu ya malipo yao kuwa kuepusha malimbikizo lakini ikimbukwe kama kweli wao ndio walitoa kibali cha kuajiri elfu 13 sio elf 8 na hilo nalo linajibika tu kiuraisi kuwa hizi ajira serikali bado ilikuwa haijajipanga ila wali kurupushwa tu na tamko la mkuu wa nchi kipindi cha kampeni

Na ndio maana zilicheleweshwa hata kutangazwa kwa post na pia mpaka leo na madudu yote hayo Raisi amenyamaza kimya nawakati hii wizara ipo chini ya ofisi yake

Hivyo tukubari tu kuwa serikali haina hela kama alivyo sema katibu wa utumishi ndio maana wanaajiri kwa awamu lakini tambua zinapo tolewa ndani yake kuna magugu mengi sana

Madhara yake ni yapi? Tunapambana na elimu bure lakini ufanisi wa elimu (ubora) haupo kutokana na upungufu wa walimu kuendana na ongezeko la wanafunzi.

Tukubari tu kuwa kwa sasa hatuna walimu wakutosha kuendana na ongezeko la wanafunzi, hatuna madarasa yanayo kizi ongezeko la wanafunzi.

Tuchakachue mambo mengine yote lakini tusiguse swala la ELIMU, ELIMU ndio uhai wa taifa
Leo hii tunafanganywa na matokeo lakini ukweli elimu yetu kila kukicha inadorola

Pia kitu kingine ni hii TAMISEMI nimwanini tamisemi ndie iwe wizara ya kufanya vetting ya watumishi nawakati sera za elimu zinatolewa na wizara ya elimu?
Ni kwanini msimamizi mkuu wa elimu na mtoa sera ambaye ni wizara ya elimu ndio ifanye vettingi ya kuajiri
Kwani hawa ndio Curriculum designer and developer na ndio wanao simamia NECTA na necta na mwalimu hawa ndio Curriculum implementer and curriculum accessor
Sasa katika hili ni vema wangerudisha wizara husika ndio ifanye hiyo kazi.

MUNGU NI MWEMA
 
Braza umejieleza Sana lakini tambua hii ni Tanzania hakuna kitakacho ongelewa apo ata kama lingetoka jina LA mwanafunzi aliemaliza darasa LA saba isingekua shida nchi ya kijinga Sana hii
 
Magufuli ana Kazi sana,Hivi JPM hutuoni tulioko chini huku? Mbona tunafaa sana tukusaidie hizo nafasi?
 
Watu mpo concrete! Shikamoo JF
 
Mkuu OTTER ,haya uliyoyaandika ni kweli!???
Itakuwa vyema kila kitu kiwekwe hadharani ili tujue wapi tatizo la msingi limeanzia. Wengine tupo mbali na huko nyumbani,hivyo tungeona uthibitisho wa haya uliyoyaandika,tungeweza saidia nini cha kufanya.
Aliyoyasema OTTER ni kweli, ndiyo yalikuwa maelekezo ya wakurugenzi kwa wakuu wa shule na waratibu elimu kata. Hii ilitolewa mwezi wa 8 mwishoni wiki chache kabla ya kutangazwa ajira mpya
 
Hao makatibu wakuu wa wizara zote tatu zilizo shugulika na huo mchakato mzima walifikiri suala hili lilivotangazwa wakati wa kampeni basi kila mpiga debe wa CCM alikuwa na sifa ya kuajiriwa!
Natoa wito pia kwa Mh. rais kutowarudisha mawaziri wote wa wizara hizo kwenye nyadhifa zao na kama bado anawahitaji basi awapeleke wizara zingine huko wameshachemka maana walikuwepo ofsini hadi rais alipoapishwa hivyo hakuna kisingizio kwamba hawakuhusika!
 
Yaani hapo ni shughuli nzito,tamisemi hawashomoi
 
Sema kwa sauti mkuu,yaani wanatuona hatujui chochote
 
Stahiki yao ni kupasuliwa majipu bila ganzi make hamna namna
 
Namwaga miamala yote walioifanya hawambwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…