Izizimba
Senior Member
- Jan 23, 2017
- 143
- 382
Rushwa imekuwa kama ugonjwa katika taasisi nyingi za serikali, ambapo kila kitu kinaonekana kuendeshwa kwa mlungula. Bila bahasha, huwezi kupata huduma kwa wakati, na bila "connections," mambo yako yatakwama hadi uchoke, utazungushwa mpaka uchakae. Hakuna anaejali umetoka wapi unapigwa tu tarehe.
Sitasahau siku niliyoenda kufuatilia kibali cha ujenzi nikajibiwa hakijatoka bila kuulizwa hata JIna langu😀😀
- Ukitaka Hati ya kiwanja RUSHWA
- Kibali cha ujenzi RUSHWA - Unahitaji hati au kibali cha kujenga? Jiandae kwa safari ndefu ya kuhonga maafisa wa serikali ili mafaili yako yasonge.Sitasahau siku niliyoenda kufuatilia kibali cha ujenzi nikajibiwa hakijatoka bila kuulizwa hata JIna langu😀😀
- Ukitaka Hati ya kiwanja RUSHWA
- Cheti cha kuzaliwa RUSHWA
- Barabarani RUSHWA - Barabarani ukipatikana na kosa, usihofu – Mradi uwe na kiasi cha kumpa afande, kesi inaweza kupotea kama moshi lakini hata kama huna kosa watu wanataka chao 😀
- Ajira RUSHWA - Ukitaka kazi serikalini, uwe na bahasha au "connection." Vijana wenye akili na vyeti wanabaki mitaani huku watoto wa vigogo wakiingia kazini bila hata interview.
Hospitali RUSHWA - Hospitalini, bila chochote mfukoni, unaweza kufa ukiwa unangoja huduma. Dawa zinazopaswa kuwa bure zinauzwa chini ya meza, na vifaa vya matibabu vinakwenda kwenye maduka ya binafsi.
Kuna muda unatengenezewa kabisa mazingira ili utoe hata kama hutaki. Usipotoa huduma utachelewa kupata au utapewa huduma mbovu.
Kimsingi nchini bila rushwa utasota sana. Serikali inajua ila haina cha kufanya maana mianya ya rushwa ni mingi sana na ni ngumu kuiziba sio leo wala kesho. Mifumo imeoza.
My take
1. Serikali ijikite zaidi katika kuboresha huduma za umma na itengeneze mifumo ya kudhibiti rushwa hii itapunguza mwingiliano wa binadamu katika huduma.
2. Kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma ili kupunguza tamaa ya mlungula.
3.Kuwajibisha viongozi na kuwafikisha mahakamani wanaojihusisha na rushwa.
4. Usalama wa taifa na TAKUKURU wajikite zaidi katika kutafuta njia madhubuti ya kumaliza rushwa, Wadeal na kiini cha tatizo.