DOKEZO Rushwa imetawala Vituo vya Ukaguzi wa Mazao barabara ya kutoka Segera - Dat via Bagamoyo

DOKEZO Rushwa imetawala Vituo vya Ukaguzi wa Mazao barabara ya kutoka Segera - Dat via Bagamoyo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari ndugu.

Ningependa kufichua uovu wa rushwa unao endelea katika vituo vya ukaguzi wa mazao ya kilimo na mali asili vilivyopo njia ya kutoka Segera kuja Dar kupitia Bagamoyo.

Wale mabwana unafika kituo cha ukaguzi una risiti zote za ushuru bado wanakulazimisha utoe pesa kwa kitisho cha kukufanyia ukaguzi zaidi.

Kwakuwa wanajua umebeba mali za kuoza ama unawahi kufikisha mali sokoni basi wanakuambia ukaguzi huo wa ziada utafanyika kukipambazuka.

Kwakweli ni uonevu uliokithiri, Serikali itume vyombo vyake ikiwemo TAKUKURU kuchunguza ujinga unaoendelea.
 
Hili kwa kweli halikubaliki, huu ni uonevu na dhuluma ya wazi,

Haraka sana serikali iingilie kati
 
Hata mimi nina kero nataka kufichua uovu na uozo na uhujumu uchumi na ufisadi mkubwa unaofanywa na waarabu dhidi ya serikali yetu Tanzania, ila bado nasubiri ruhusa kutoka mamlaka za jukwaa
 
Back
Top Bottom