Rushwa kwa walinzi wa mlimani city shopping mall

Mimi.

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
2,120
Reaction score
3,059
Wakuu,

Nimeona si vibaya nikiwataadhalisha mkawa makini pale mnapoingia katika gate la mlimani city ili msije mkapata usumbufu kama ulinionipata mimi

Ni hivi ukiingia pale hasa ili geti kubwa la Sam nujoma rd mida ya mchana pale getini haukuti walinzi wanakua wamejificha pale kwa chini kwenye kibanda chao na geti la kuingilia wanaliacha wazi,nia na madhumuni ya kujificha kwao ili uingie bila ya card na utakapotoka bila ya ile card wakutoze faini ya shilingi elfu kumi pamoja na photocopy ya driving license na card ya gari kama hautaki huo usumbufu wa kwenda kutoa copy unatoa Rushwa ya shilingi 5000 kwa mlinzi basi unaluusiwa kuondoka,mnapoingia pale muwe makini kamwe husikubali kupita mpaka mlinzi atoke mafichoni kwenye kile kiofisi chao na upewe card ya kuingilia,
 

Hiyo ishanikuta, nikawavimbia, sikuwapa senti tano na nikakataa kusogeza gari pembeni, wakaachia geti.

Nilifikiri ni mimi tu, kumbe ndio ka mchezo kao. Uongozi wa hao walinzi na wa Mlimani lazima utazame hili suala, ni kero.
 
ndio zaoo hata sikushangaa nna kadi 2 kwa gari yangu za mlimani city ...nshawah ibiwa pale power windows sikupata msaaada wowote
 
aiseeee babaangu mlimani city ndio wapi??? Ili 2kija uko dar 2sije kupata izo tabu,,, eti ni mlimani city ndio pale magari yanayotoka mkoani yanaingia
 
nilishapa hiyo kadhia pia muwe makini sana
 
kweli - mbuzi ula kwa ulefu wa kamba yake, hili taifa limejaaa ufisadi tuuu na rushwa, hata kama hutaki kutoa utatengenezewa mazingira.

mfano nimefatilia stika ya usalama barabarani, naambiwa zimeisha, lengo kesho wanikamate niache kitu kidogo. poleni waTz
 
wapuuzi sana hao.....ndo mana nimehamia quality centre
 
Ni kweli kabisa ni wizi mkubwa kwanza izo card zinazuia vipi wizi?
 
"Huwa nawaonea huruma sana gari ya mtu ikiibiwa na ikatoka pale pale getini" nafikiri inabidi wawe wakali sana kwenye issue za wasio na card wakati wa kutoka,sasa utajuaje kama gari ni ya kwako?na pia parking zote pale at your own risk!
 
Kuna uongozi pale lakini. Ukikuta hawapo kibandani park gari hapo hapo kibandani mtafute meneja wao

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mi nikikuta wamejificha napaki getini hapohapo naziba njia.
 
nlikutana na hilo kufika wakanambia pita nkapita kutoka wananiuliza kadi nliwavimbia mbaya wakanambia hatukukupa tukijua we ni staff wa voda kweli mchezo huo uko kuweni makini
 
Hizi Cards hazisaidii,
Naweza nkaingia asubuhi nkaacha gari ndani, nusu saa tu inanitosha ku-reproduce kadi kama zile kwenye stationery za Mwenge!!

Jamaa yangu mmoja alipoteza kadi pale, ikabid anipigie nije na laptop + flashdisk ili tupate kadi ya kufanyia magumshi.

Kifupi ni kwamba zinafojika kwa urahis, so usalama wake ni mdogo zaidi ya kwamba zinaleta jam tu getini, isitoshe hazina namba rejista.
 
Njaa tu zinawasumbua,wakikuzuia nxt time na wanajifanya hawaelewi maelezo sogeza gari mpaka pale gate linaponyanyukia,then tulia hapo uone foleni yake huko nyuma,mbona watakuachia fasta
 

ilishanitokea hiyo last week.. nikwapa 1500/- Nikasepa ,wapuuzi sana wanafanya makusudi kabisa
 

nyinyi ndio mnarudisha maendeleo nyuma .... huna tofauti na yle kibaka aliyetaka kuiba vyuma vya reli ile siku mwakyembe amezindua train....

huo uliofanya ni uhalifu...

ustaarabu unaanza kwako then kwa mwengine....

usirudie tena...
 
Ila kuna watu wengine wanawadharau sana wale jamaa, kuna siku mdada na Noah yake kaonyeshewa kadi hata kufungua vioo hakufungua akapita, basi wakataarifiana, tehe 2 day next ndo alikuja to gari pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…