Pre GE2025 Rushwa na Uchaguzi: Ni kwa kiasi gani Vijana wanashindwa kugombea nafasi za Uongozi kutokana na Rushwa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
1738079796761.jpeg

Rushwa imekuwa kikwazo kikubwa katika mchakato wa uchaguzi, hasa ndani ya vyama vya siasa. Hii si tu inavuruga mchakato wa Kidemokrasia, bali pia inazima ndoto na juhudi za Vijana ambao wangependa kuona mabadiliko chanya katika uongozi wa Vyama na taifa kwa ujumla

Katika Mjadala kuhusu Rushwa na Uchaguzi, tutajadili changamoto wanazopitia Vijana wakemea Rushwa ndani ya Vyama pamoja na masuluhisho yake

Usikose kujiunga nasi leo Januari 28, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums.

Ili kushiriki mjadala huo kupitia XSpaces bofya hapa: Mjadala XSpaces, pia unaweza kushiriki kwa kubonyeza kwenye banner inayoonekana kwenye screen yako ambayo itakupeleka moja kwa moja kwenye XSpaces ya JamiiForums

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

RAHMA MWITA: Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari - ACT Wazalendo

"Sheria ya Rushwa ipo lakini kiuhalisia vitu vinavyotokea kwenye uhalisia ni tofauti, kuna mambo mengi yanaibuliwa kila siku na hakuna kinachofanyika. Hali kama hiyo inafanya watu wengine waanze kukata tamaa ya kutokuwa na Moyo wa ushiriki."

"Suala la kuona Mtu anatoa Rushwa na kisha anafanikiwa ni jambo la kawaida na hiyo inakatisha au inawavunja Moyo Vijana. Kiuhalisia mambo ni magumu, ni kama vile tumeamua kuweka tick kwenye boksi lakini uhalisia ni tofauti."

"Wakati mwingine wanaotoa Rushwa ni Vijana. Mimi ni Kijana na nipo kwenye ngome ya Vijana, kuna wengine unawasikia wanasema "Mimi nimetumia (Tsh) Milioni 50 kupata nafasi hii" Kinachoendelea ni kama tumeamua kuifanya Rushwa kuwa jambo la kawaida."

"Maisha yetu yalivyo tumeifanya Rushwa kuwa sehemu ya Maisha yetu, hiyo ni kwasababu Watu waliopita nyuma yetu walikuwa wanafanya hivyo vitendo na ndio maana hata Vijana wa sasa wanaona bora waendeleze kilekile walichokikuta."

"Tunapoelekea, itafikia hatua Watu wataanza kujichukulia Sheria mkononi kutokana na Mazingira ya Rushwa yanayoendelea na kusababisha upendeleo kwa upande fulani."

"Unapomchagua mgombea kwa kuzingatia Rushwa yake unatakiwa utambue kuwa atakapoingia madarakani atafanya anavyoweza kurejesha kile alichokipoteza wakati wa kampeni"

John Pambalu: Mwanachama CHADEMA

"Sijawahi kuona TAKUKURU imeshughulika na Rushwa za kwenye Siasa.Tumeshuhudia mara kadhaa matukio ya aina hiyo, mfano kuna Mwaka Mtu mmoja alikamatwa akiwa na begi la Fedha na hatukusikia hatua zikichukuliwa."

Moja ya changamoto ya Rushwa ni kuwa aliyepokea na aliyetoa wote wanataka, ndio maana wakati mwingine inakuwa na ugumu kufuatilia.

"Sheria ya gharama za Uchaguzi ipo kama nadharia, hakuna njia ya kuiwezesha Mamlaka kukukamata kwa kuwa wewe mhusika unajua jinsi ya kujikadiria, unajaza fomu mwenyewe bila Mtu kukusimamia".

"Unaweza kubuni umetumia kiasi fulani cha Fedha kumbe umetumia zaidi ya hiyo, hivyo ni vigumu kulidhibiti hilo."

"Mtu mmoja akifanya vitu pasipokuwa na makubaliano na Vikao wakati wa uchaguzi akilenga kuwapa ‘feva’ Wajumbe hiyo nayo ni Rushwa"

"Kumekuwa na kelele katika Uchaguzi wa CHADEMA uliopita, Mwenyekiti amekuwa mkali kuhusu suala hilo na tunaamini kuna hatua zitachukuliwa"

Kamala Dickson (Mdau)

"Watu wa Mtandaoni wanaweza kuwa na ‘influence” katika Jamii kwa kutegemea na aina ya ujumbe ambao wanauwasilisha, hivyo kama kuna Mtu ameitumia Mitandao kufikisha ujumbe unaotakiwa sioni kama ni tatizo na haiwezi kutambulika kuwa ni Rushwa"

"Kuna wakati nilienda kugombea Ubunge, mpinzani wangu ambaye alikuwa ni Waziri alikuwa anategemewa na Wajumbe wengi, walimtegemea kwenye kuwalipia ada Watoto wao, alikuwa akimiliki Vikundi vya Wanawake"

"Hali hiyo ilisababisha mimi ambaye nilikuwa Kijana niliyetoka Chuo wabaki wananishangaa na kunicheka, maana yake ni kuwa nafasi ya Vijana kuwa Wabunge au Madiwani ni ndogo"

Entesh Melaisho: Twaweza - Mzungumzaji

"Sheria zilizopo kuhusu Rushwa ni kama zimekuwa na faida kwa makundi fulani ya Watu, ndio maana inaonekana kuna aina ya watu au kundi fulani hawaguswi na Sheria hizo"

"Sheria kuhusu Rushwa zipo na zinafahamika kwa wachache, hazifuatwi na kwa maana hiyo imekuwa ni hali ya kawaida"

"Mbali na kutafuta mbinu za kudhibiti Wajumbe kwenye Chaguzi lakini pia sisi wenyewe tunatakiwa kubadilika na kutambua kuwa Rushwa ni mbaya na inatupoteza wenyewe"

"Kuzuia Rushwa, AZAKI zinaweza kusimamia na kupigia kelele uwepo wa Sheria bora ambazo zinaweza kutumika kupunguza au kuondoa mazingira ya Rushwa"

"AZAKI zinaweza kutumika kutoa Elimu zaidi kuhusu suala la Uwajibikaji na Haki za Kiraia, kupitia Elimu hiyo Wananchi wanaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuwafanya Viongozi wawajibike na kutimiza majukumu yao hata kama wametoa Rushwa"

Christina Kapama: Wajibu - Mzungumzaji

"Vijana wakiweza kutengenezewa dhana ya Uwajibikaji na Siasa Safi inaweza kusaidia kuwaondoa katika ile fikra au dhana ya kuwa Rushwa ndio kila kitu"

" Tuna Sheria kuhusu Rushwa lakini zinakosa meno, hazioneshi namna gani changamoto za kifedha zinazowakuta vijana zinaweza kutumika kuwasaidia kushiriki kwenye Chaguzi bila Rushwa kuhusika"

"TWAWEZA na JamiiForums ni kati ya Taasisi ambazo zimekuwa zikitoa mafunzo kwa nia ya kutoa Elimu kuhusu Uwajibikaji na kujitambua kwa Vijana lakini changamoto inayotokea ni kuwa washiriki wanakuwa hawapo tayari hadi wanapoona kuna ahadi ya kitu fulani watapata watakaposhiriki"

Othuman Chuma (Mdau)

"Vijana tunatakiwa kuwa na chombo cha Baraza la Taifa kwa ajili ya kutuwakilisha na kutusemea, chombo hicho kitasaidia kutoa elimu ya kupambana na Rushwa na jinsi ya kudhibiti"

Musa D. Njoghomi (Mdau)

"Rushwa imekuwa changamoto kubwa na kuwatia Vijana hofu ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Ili tuweze kuwavutia vijana waweze kushiriki tunatakiwa kuwa na njia ya kudhibiti Rushwa, jambo gumu ni kuwa katika suala la Rushwa mtoaji na mpokeaji wote wanakuwa wanufaika ndio maana yule wa pembeni (Kijana) kwake inakuwa ngumu kufanikiwa"

Aristodi Furia (Mdau)

"Rushwa huwa inaanzia ngazi ya Familia, mara nyingi Vijana wanapokuwa wadogo, wanakua wakiangalia kile kinachofanywa na Wazazi, Walezi au wakubwa wao. Kama tunashindwa kudhibiti Rushwa kuanzia ngazi ya Familia ni ngumu kudhibiti nje ya Familia"

"Vyombo ambavyo vinadhibiti Rushwa vinatakiwa kuboreshwa na kupewa nguvu kuanzia ngazi ya Mtaa kupanda hadi Taifa, bila kufanya hivyo tukitegemea ngazi ya Taifa huku chini kunakuwa kunaoza"

Assenga Assenga (Mdau):

"TAKUKURU hawafanyi kazi ya kuzuia rushwa kwenye masuala ya Uchaguzi, inawezekana nao ni wanufaika wa hayo yanayokuwa yanaendelea"

"Taarifa nyingi za matumizi ya Fedha za uchaguzi sio za kweli, kiasi kinachotumika na kile kilichoandikwa kwenye fomu ni tofauti kwa kuwa wanaojaza wanafanya hivyo kuwafurahisha wanaotaka kuona zimejazwa vile wanavyotaka wao"

"Rushwa imekuwa sehemu ya mchezo katika Maisha yetu ndio maana mbali na kwenye Uchaguzi hata Maisha mengine pia ipo. Unaweza kukuta ndugu yako amekamatwa na Askari Polisi, suala lake lina dhamana lakini ili kuipata unalazimika kutoa 'kitu kidogo'"

Thobias Mgisha (Mdau)

"TAKUKURU inahusika kudhibiti Rushwa lakini imetokea mara kadhaa hata wao wenyewe wanatuhumiwa kuhusika na Rushwa, upande mwingine Viongozi wetu wengine nao wanatuhumiwa kuhusika na Rushwa, matokeo yake inakuwa jamii iliyoathiriwa na Rushwa"

Stanslaus Lambat (Mdau)

"TAKUKURU wanapaswa kuonesha wanachukua hatua, inawezekana wanachukua hatua lakini Watu hawaoni kama wao wanatimiza hicho wanachotakiwa kukifanya"

Mtoto wa Maria Mwahi (Mdau)

Tanzania haijawahi kuwa na Uchaguzi ambao haukuwa na Rushwa, Uchaguzi unafanyika lakini wanaoshinda ni wale ambao Mamlaka inahitaji washinde bila kujali uhalali wa Kura
 
TAKUKURU wanatuangusha sana, rushwa zinafanywa nje nje wamute kama hawapo vile
 
Watoa rushwa wakubwa ni CCM, TAKUKURU hawana ubavu wa kuwagusa.
 
Mama 'Abduli' anagawa 'zawadi' kama peremende kila mtu kimyaaaaa.... kuna mwanga kweli wa rushwa kuisha wakati wa uchaguzi?
 
Mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji uwazi, hatua thabiti na usimamizi madhubuti. Bila nguvu za kisheria na uwajibikaji wa kweli kwa taasisi kama TAKUKURU, rushwa itaendelea kuwepo
 
No money no politics, politics is about solving problems. Ushahidi angalia Sugu kabla hajawa Mbunge alipauka, Heche alipauka, Pambalu amepauka
 
Rushwa imekuwa kikwazo kikubwa katika mchakato wa uchaguzi, hasa ndani ya vyama vya siasa. Hii si tu inavuruga mchakato wa Kidemokrasia, bali pia inazima ndoto na juhudi za Vijana ambao wangependa kuona mabadiliko chanya katika uongozi wa Vyama na taifa kwa ujumla

Katika Mjadala kuhusu Rushwa na Uchaguzi, tutajadili changamoto wanazopitia Vijana wakemea Rushwa ndani ya Vyama pamoja na masuluhisho yake

Usikose kujiunga nasi leo Januari 28, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums.

Ili kushiriki mjadala huo kupitia XSpaces bofya hapa: Mjadala XSpaces, pia unaweza kushiriki kwa kubonyeza kwenye banner inayoonekana kwenye screen yako ambayo itakupeleka moja kwa moja kwenye XSpaces ya JamiiForums

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

RAHMA MWITA: Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari - ACT Wazalendo

"Sheria ya Rushwa ipo lakini kiuhalisia vitu vinavyotokea kwenye uhalisia ni tofauti, kuna mambo mengi yanaibuliwa kila siku na hakuna kinachofanyika. Hali kama hiyo inafanya watu wengine waanze kukata tamaa ya kutokuwa na Moyo wa ushiriki."

"Suala la kuona Mtu anatoa Rushwa na kisha anafanikiwa ni jambo la kawaida na hiyo inakatisha au inawavunja Moyo Vijana. Kiuhalisia mambo ni magumu, ni kama vile tumeamua kuweka tick kwenye boksi lakini uhalisia ni tofauti."

"Wakati mwingine wanaotoa Rushwa ni Vijana. Mimi ni Kijana na nipo kwenye ngome ya Vijana, kuna wengine unawasikia wanasema "Mimi nimetumia (Tsh) Milioni 50 kupata nafasi hii" Kinachoendelea ni kama tumeamua kuifanya Rushwa kuwa jambo la kawaida."

"Maisha yetu yalivyo tumeifanya Rushwa kuwa sehemu ya Maisha yetu, hiyo ni kwasababu Watu waliopita nyuma yetu walikuwa wanafanya hivyo vitendo na ndio maana hata Vijana wa sasa wanaona bora waendeleze kilekile walichokikuta."

"Tunapoelekea, itafikia hatua Watu wataanza kujichukulia Sheria mkononi kutokana na Mazingira ya Rushwa yanayoendelea na kusababisha upendeleo kwa upande fulani."

JOHN PAMBALU: Mwanachama CHADEMA

"Sijawahi kuona TAKUKURU imeshughulika na Rushwa za kwenye Siasa.Tumeshuhudia mara kadhaa matukio ya aina hiyo, mfano kuna Mwaka Mtu mmoja alikamatwa akiwa na begi la Fedha na hatukusikia hatua zikichukuliwa."

Moja ya changamoto ya Rushwa ni kuwa aliyepokea na aliyetoa wote wanataka, ndio maana wakati mwingine inakuwa na ugumu kufuatilia.

"Sheria ya gharama za Uchaguzi ipo kama nadharia, hakuna njia ya kuiwezesha Mamlaka kukukamata kwa kuwa wewe mhusika unajua jinsi ya kujikadiria, unajaza fomu mwenyewe bila Mtu kukusimamia".

"Unaweza kubuni umetumia kiasi fulani cha Fedha kumbe umetumia zaidi ya hiyo, hivyo ni vigumu kulidhibiti hilo."
Juzi hapa wananchi wekataaa 'zawadi' za Kawawa wala hatujaona hata TAKUKURU kujishika.

Rushwa inakuwa Rushwa ikihusisha wapinzani au vidagaa, ikiwa ni mwanasiasa mkubwa kutoka CCM huwezi sikia TAKUKURU ikisema kitu
 
Subiri ikikaribia Oktoba watakavyokuwa wanatoa matamko hewa kuhusu rushwa kwenye uchaguzi kujifanya wako kazini sasa
 
TAKUKURU inatakiwa ijitafakari upya.

Tabia ya kukamata wala rushwa wadogo wadogo alafu kuacha kushughulika na rushwa kwenye chaguzi zetu sio poa.

Natamani kuona wakiwa active kudhibiti rushwa kisawasawa kwenye Uchaguzi mkuu ujao
 
Nyuki wamekimbia uzi bana😂🤣🤣🤣 kama hawaoni vile. Nabubujikwa machozi ya huzuni🤣😆😆
 
Hii ina maana TAKUKURU wanatumiwa kama ngao kwa baadhi ya watoa rushwa
Ndio maana yake, utawaona tu upinzani wakijichanganya au vile vidagaa ambavyo havina connection... kama wale trafiki ambao walidakwa wanachukua mia2 mia2
 
Rushwa imekuwa kikwazo kikubwa katika mchakato wa uchaguzi, hasa ndani ya vyama vya siasa. Hii si tu inavuruga mchakato wa Kidemokrasia, bali pia inazima ndoto na juhudi za Vijana ambao wangependa kuona mabadiliko chanya katika uongozi wa Vyama na taifa kwa ujumla

Katika Mjadala kuhusu Rushwa na Uchaguzi, tutajadili changamoto wanazopitia Vijana wakemea Rushwa ndani ya Vyama pamoja na masuluhisho yake

Usikose kujiunga nasi leo Januari 28, 2025, kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums.

Ili kushiriki mjadala huo kupitia XSpaces bofya hapa: Mjadala XSpaces, pia unaweza kushiriki kwa kubonyeza kwenye banner inayoonekana kwenye screen yako ambayo itakupeleka moja kwa moja kwenye XSpaces ya JamiiForums

========================================

MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA

RAHMA MWITA: Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari - ACT Wazalendo

"Sheria ya Rushwa ipo lakini kiuhalisia vitu vinavyotokea kwenye uhalisia ni tofauti, kuna mambo mengi yanaibuliwa kila siku na hakuna kinachofanyika. Hali kama hiyo inafanya watu wengine waanze kukata tamaa ya kutokuwa na Moyo wa ushiriki."

"Suala la kuona Mtu anatoa Rushwa na kisha anafanikiwa ni jambo la kawaida na hiyo inakatisha au inawavunja Moyo Vijana. Kiuhalisia mambo ni magumu, ni kama vile tumeamua kuweka tick kwenye boksi lakini uhalisia ni tofauti."

"Wakati mwingine wanaotoa Rushwa ni Vijana. Mimi ni Kijana na nipo kwenye ngome ya Vijana, kuna wengine unawasikia wanasema "Mimi nimetumia (Tsh) Milioni 50 kupata nafasi hii" Kinachoendelea ni kama tumeamua kuifanya Rushwa kuwa jambo la kawaida."

"Maisha yetu yalivyo tumeifanya Rushwa kuwa sehemu ya Maisha yetu, hiyo ni kwasababu Watu waliopita nyuma yetu walikuwa wanafanya hivyo vitendo na ndio maana hata Vijana wa sasa wanaona bora waendeleze kilekile walichokikuta."

"Tunapoelekea, itafikia hatua Watu wataanza kujichukulia Sheria mkononi kutokana na Mazingira ya Rushwa yanayoendelea na kusababisha upendeleo kwa upande fulani."

JOHN PAMBALU: Mwanachama CHADEMA

"Sijawahi kuona TAKUKURU imeshughulika na Rushwa za kwenye Siasa.Tumeshuhudia mara kadhaa matukio ya aina hiyo, mfano kuna Mwaka Mtu mmoja alikamatwa akiwa na begi la Fedha na hatukusikia hatua zikichukuliwa."

Moja ya changamoto ya Rushwa ni kuwa aliyepokea na aliyetoa wote wanataka, ndio maana wakati mwingine inakuwa na ugumu kufuatilia.

"Sheria ya gharama za Uchaguzi ipo kama nadharia, hakuna njia ya kuiwezesha Mamlaka kukukamata kwa kuwa wewe mhusika unajua jinsi ya kujikadiria, unajaza fomu mwenyewe bila Mtu kukusimamia".

"Unaweza kubuni umetumia kiasi fulani cha Fedha kumbe umetumia zaidi ya hiyo, hivyo ni vigumu kulidhibiti hilo."

"Mtu mmoja akifanya vitu pasipokuwa na makubaliano na Vikao wakati wa uchaguzi akilenga kuwapa ‘feva’ Wajumbe hiyo nayo ni Rushwa"

"Kumekuwa na kelele katika Uchaguzi wa CHADEMA uliopita, Mwenyekiti amekuwa mkali kuhusu suala hilo na tunaamini kuna hatua zitachukuliwa"

KAMALA DICKSON (Mdau)

"Watu wa Mtandaoni wanaweza kuwa na ‘influence” katika Jamii kwa kutegemea na aina ya ujumbe ambao wanauwasilisha, hivyo kama kuna Mtu ameitumia Mitandao kufikisha ujumbe unaotakiwa sioni kama ni tatizo na haiwezi kutambulika kuwa ni Rushwa"

"Kuna wakati nilienda kugombea Ubunge, mpinzani wangu ambaye alikuwa ni Waziri alikuwa anategemewa na Wajumbe wengi, walimtegemea kwenye kuwalipia ada Watoto wao, alikuwa akimiliki Vikundi vya Wanawake"

"Hali hiyo ilisababisha mimi ambaye nilikuwa Kijana niliyetoka Chuo wabaki wananishangaa na kunicheka, maana yake ni kuwa nafasi ya Vijana kuwa Wabunge au Madiwani ni ndogo"
Tatizo la Tanzania sio rushwa ya uchaguzi ni RUSHWA KWENYE KILA KITU.
 
Back
Top Bottom