Pre GE2025 Rushwa na Uchaguzi: Ni kwa kiasi gani Vijana wanashindwa kugombea nafasi za Uongozi kutokana na Rushwa?

Pre GE2025 Rushwa na Uchaguzi: Ni kwa kiasi gani Vijana wanashindwa kugombea nafasi za Uongozi kutokana na Rushwa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Noma sana, kwa maoni yako Mkuu tunawezaje kudeal na hili?
Watanzania wengi hawapendi rushwa Lissu leo ni mashuhuri sababu moja wapo ni kupinga rushwa. Serikali ni lini tumeona kiongozi yeyote ana kesi ya rushwa. Yaani kila mahali ukienda ni rushwa lakini tatizo hao viongozi kwanza hawajachaguliwa na wananchi pili wenyewe ni wala rushwa
 
TAKUKURU mnawaonea tu. Wakiwakamata wanasisiemu wanaambiwa wako upande wa upizani, bila shaka mnakumbuka uchaguzi wa 2015 mpaka DG wa TAKUKURU akatumbuliwa, vilevile TAKUKURU wakiwakamata wapinzani wanatuhumiwa kutumiwa na sisiemu so tukubaliane kwamba mapambano dhidi ya rushwa ni political will ya kiongozi wa juu zaidi ya hapo mtawalalamikia TAKUKURU kila leo
 
Watanzania wengi hawapendi rushwa Lissu leo ni mashuhuri sababu moja wapo ni kupinga rushwa. Serikali ni lini tumeona kiongozi yeyote ana kesi ya rushwa. Yaani kila mahali ukienda ni rushwa lakini tatizo hao viongozi kwanza hawajachaguliwa na wananchi pili wenyewe ni wala rushwa
Wapo viongozi wamewahi kushtakiwa kwa rushwa, Mramba aliyewahi kuwa waziri wa fedha. Lakini pia ukiingia kwenye website ya Mahakama ya mafisadi zipo kesi zinazoendelea na zilizowahi kutolewa maamzi ingawa swala la kupambana na rushwa kwa viongozi wa kubwa wa kiafrika ni kazi ngumu, refer kilichotokea wakati ule Afrika kusini mpaka iliyokuwa TAKUKURU ya kule ikafutwa ni kwasababu iligusa maslahi ya wakubwa wa kule
 
Yaani unaongelea viongozi wa Mkapa ambaye alikuwa Raisi kuanzia 1995-2005 miaka mingapi imepita! 20!!. Leo hii kuna rushwa yakunuka nani kafikishwa mahakamani
 
Minadhani ni muda sahihi sasa kila mtu kujitambua na kuwa mzalendo kwaajili ya kujenga nchi,

Kuhusu suala la rushwa kuna baadhi ya wananchi wenyewe wanalifurahia hasa wa hali ya chini

Mfano, uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa kuna baadhi ya maeneo watu waligoma kupiga kura mpka wape pesa,

Sio umuhimu wa kuilaumu Takukuru kila mtu ajitambue yeye mwenyewe

Aone kama hicho anachopokea ni rushwa na sio kitendo chema, ikiwa katika hali hiyo hakuna wa pokeaji hata watoaji watapungua

Ila kuna baadhi ya watu kwa muda huu wana subiri kupokea rushwa washibishe matumbo yao.

Yote kwa yote tujitambue.
 
Yaani unaongelea viongozi wa Mkapa ambaye alikuwa Raisi kuanzia 1995-2005 miaka mingapi imepita! 20!!. Leo hii kuna rushwa yakunuka nani kafikishwa mahakamani
Kwani mahakama ya mafisadi ilianzishwa wakati wa Mkapa?
 
Kwani mahakama ya mafisadi ilianzishwa wakati wa Mkapa?
Mafisadi hawawezi kuzuia mafisadi. Yaani mahakama ya rushwa ndiyo inaongoza kwa rushwa!!!!. Raisi hayupo serious na rushwa na hajali huo ndiyo ukweli. Nyie mkisubiria wapinzani pekee nchi yetu mtabaki na mifupa tu
 
Yaani unaongelea viongozi wa Mkapa ambaye alikuwa Raisi kuanzia 1995-2005 miaka mingapi imepita! 20!!. Leo hii kuna rushwa yakunuka nani kafikishwa mahakamani
Ndio maana nikasema swala la kupambana na rushwa ni la utashi wa kiongozi wa juu, vinginevyo rushwa itaendelea na mtaendelea kuwalaumu TAKUKURU. kwa mfano katika mswada wa marekebisho ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya 2023 TAKUKURU ilipendekeza itungwe sheria ya kuifanya kuwa Taasisi huru na DG asiteuliwe na Rais na pia isiwe chini ya Ofisi ya Rais lakini Serikali ilikataa na kile kifungu kikaondolewa, sasa jiulize Serikali inaogopa nini? Je hapo kuna nini kimejificha
 
Back
Top Bottom